Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini ENGINEERS wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni nini hasa?

View attachment 1517904

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba;

Moja (1) Siku ya Ijumaa ilee ya wiki iliyopita nilimsindikiza mjomba wangu mmoja kule kariakoo kwenda kununua kipuri (spare) moja ya mshine ya kusagia unga kwa ajili ya kupeleka kijijini kwao kwa maana hii ndio biashara yake miaka nenda rudi.

Sasa baada ya kufika katika duka la baba mmoja mtanzani mwenye asili ya bara la asia (al maaruf kama mhindi) tukakuta ni kweli anayo spare ile ila zipo za aina tatu. Moja ni kitoka nchini Singapore, nyingine nchini China na ya tatu ni kutoka nchini Ujerumani. Sasa yeye akawa anamsisitiza mjomba wangu kwa lafudhi ya Kiswahili cha kihindi "chukua hii baba ipo genuine kabisa fresh from german" basi uncle akanunua, akalipa kisha sisi haoooo tukarudi zetu home.

Mbili (2) Vile vile inasemekana kwamba, mtu akianza kuendesha gari za Kijerumani kama vile Mercedes Benz, BMW, Audi au VolksWagen kwa namna zinavyokuwa nzito na kutulia sana barabarani, mtu huyo kamwe hatotamani tena maishani mwake kuendesha gari za Kijapan kama vile Toyota na Nissan.

View attachment 1518897

Tatu (3) Bila kuishia hapo, huku mitaani pia mara nyingi kumekuwepo na msemo maarufu kwa mfano utamsikia mtu akijigamba kwa rafiki yake kwamba "daaah mwanangu hii pasi tangia niinunue huu ni mwaka wa 8 sasa na sijawahi kuipeleka kwa fundi, chuma cha mjerumani hiki mzee baba"

Nne (4) Msafari wa Rais wa Russia ndugu Vladmir Putin umejaa gari za kijerumani tupu. Kuanzia BMW motorcycles; and Mercedes G-Class, Mercedes E-Class, S-Class mpaka BMW 5 Series. Tazama picha ya msafara wa Putin hapo chini.

View attachment 1517923

Sasa kwa kuzingatia scenario hizo zote nne (4) ndio nikajawa na maswali mengi sana akilini mwangu kwamba WHY ARE GERMANS SO GOOD AT ENGINEERING?

Kuna baadhi ya watu hapa watakuja kusema ninaisifia sana Ujerumani kwa maana ninauza vitabu vyao hahahahaaaaaa

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

View attachment 1518291

PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
Simply
Angalia mfumo wao wa elimu. Kwa wanaofeli masomo wanaingizwa ktk mfumo wa Grundess Diploma..... huko ndo wanapikwa vizuri mno
 
Unajua hawa jamaa babu zao ndio waliogundua aina zote mbili za engine (petrol na dezeli).Kwa wale waliopitia"Thermodynamics" mtakuwa mnakumbuka "Otto cycle" na "Diesel cycle", Hawa mababu Nikolaus Otto na Rudolf Diesel walikuwa Wajerumani hivyo vizazi vilivyo kuja baada ya hapo vimeendelea kuboresha hiyo teknolojia toka wakati huo (karne ya 19) ndio maana magari na mitambo yao ina ubora wa hali ya juu
Hata diesel electric locomotives zinazotoka kwao ni Complex mno tofauti na za wamarekani. Miaka ya Nyuma ziliwahi nunuliwa locomotives hapa kwetu toka kwao hao jamaa Kufanya fuel pump timing tu ni balaa ukikurupuka injini huwashi.
 
Wakuu zaidi ya magari yao Mercedes Benz,BMW Audi VW ni products zipi za Kijerumani zinatamba duniani? Wengine dunia imetuacha nyuma
Wana vichwa vya treni (Diesel electric locomotives) bora sanaa kuliko zinazotoka kwa GE au EMD huko USA pia wana engine za Motoren Und Turbanien (MTU) zinafika mno utendaji wa kazi katika Boat kubwa na Mashine za Migodini pia mashine za kuchongea vipuri (Lathe machine) zinazotoka kwao ni nzuri mno.
 
Wana vichwa vya treni (Diesel electric locomotives) bora sanaa kuliko zinazotoka kwa GE au EMD huko USA pia wana engine za Motoren Und Turbanien (MTU) zinafika mno utendaji wa kazi katika Boat kubwa na Mashine za Migodini pia mashine za kuchongea vipuri (Lathe machine) zinazotoka kwao ni nzuri mno.
Mkuu, hakika jamaa wapo vizuri sana na hii yote inatokana na misingi ya elimu bora waliyoijenga kwa miaka mingi sana.
 
Vifaa vya ndege ni noma, hasa jet engine hao ni nyoko! Mchina ameshibdwa kukopi, wataalamu wanasema haikopiki,lazima akuvujishie au uschratch
Ni kweli kabisa sikupingi hapa kwetu vilikuja vichwa vya treni toka kwake kwa reli ya kati lakini vilikuwa vina nguvu mno kuliko vilivyokuwepo kutokana na kuwa vilikuwa na high technology kwa wakati huo leo hii hatuna hata kimoja na vilikuja miaka ya 90. Kwahiyo kuiba technology ya hawa jamaa ngumu mno.
 
Hii system safi sana. Si ndio kama VETA huku kwetu?
Ni kama veta pasee lakini wapo deep. Na hao wakitoka hapo ni wabunifu, mafundi na mainjinia.... wakimaliza hiyo diploma wanaweza kuendelea na mfumo wa universities.


VETA ikiboreshwa inaweza kuwa gateway ya kuelekea kwenye maendeleo makubwa ya kiteknolojia...
 
I am also wondering why Tanzania engineers are of the poorest quality. Look at tanesco engineers. Look at Tanroad engineers. Kukiwa na barabara ya kutengenezwa maengineer wa Tanroad watafuatilizia mule mule ilipo barabara iliyobuniwa na wananchi. Mfano. Mbezi Goba Mbezi beach. Mbezi Maramba majumba sita. Buza kwa Mpalange to Buza kwa lugola.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]dah we jamaa Mungu anakuona kwamba wanafuatilizia mulemule walipopita wananchi.
 
Hili swali nilipata majibu yake jana kutoka kwa babu
Babu anasema miaka ya nyuma kusomea ufundi wowote mf. Uashi, useremala n.k ilikuwa unasoma miaka 3 alafu unatakiwa uzunguke kwenye karakana mbalimbali kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 3 tena ili kupata ujuzi tofautitofauti inaitwa (Wandergeselle) hii ilisaidia mtu kujifunza vingi hadi sasa bado ipo lakini kwa kiasi kidogo sana, pia ili uruhsiwe kufungua ofisi yako ni lazima uwe una elimu ya juu zaidi kwenye huo ufundi inaitwa Meister (ukuu ama utaalamu) na hiyo kuipata kwa miaka hiyo ilihitaji hata zaidi ya miaka kumi baada ya kusoma ufundi wa kawaida na waliyofungua ofisi kwa siri bila kuwa na Meister walifilisiwa na adhabu zilitolewa kwao hivyo tangu hapo ukawa ni muendelezo wa watu kauhakikisha wanafanya vitu kwa ubora wa hali juu.
Niemandika mengi yanaweza kumchanganya msomaji unaruhusiwa kuuliza tena.
Na hapa ndipo Siri ya wenzetu kufanikiwa malengo yao ilipo

Sheria kali kwa watakaokiuka ujuz uliofuata mtiririko sahihi siyo kupata ujuzi kupitia fundi maiko au maiko college

Tuige hapa tutatoboa hatujachelewa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom