Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa anybody!.
pongezi zetu kwake kwa sisi baadhi yetu, ni pongezi bonafide genuine, kumpongeza kwa dhati kabisa kwa mazuri anayolifanyia taifa letu na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote licha
- Pascal Mayalla ni Mtanzania, anayekidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa na rais kushika wadhifa wowote kama U DC!. Siku zote nimekuwa nikisema sihitaji uteuzi, ila kuna mwana jf mmoja akauliza kama ikitokea ghafla mara pap... Pascal Mayalla umeteuliwa DC, Jee Utakataa?. Nilishindwa kujibu!, Ukiteuliwa ukikataa utaonekana ni mtovu wa nidhamu!. Ili kuzuia utovu wa nidhamu, ni vizuri uki declare interest wazi, openly na publically, Pascal Mayalla hahitaji uteuzi wa kuwa DC!.
- Kwenye uteuzi wa Majaji wapya, mmoja wa majaji wapya ni mwandishi wa habari binti, tulimpokea pale RTD, tukamfundisha kazi, akaenda kusoma sheria, akawa wakili wa kujitegemea juzi kateuliwa Jaji. Mimi pia nimesoma sheria, tena LL.B yangu ni LL.B (HONS) ya UDSM, hivyo ninakidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa kuwa Jaji, lakini naomba kukiri, siwezi kumhukumu mtu kifo, hivyo siwezi kuwa Jaji na naomba nisiteuliwe kuwa Jaji!.
Japo Kuna Wengi Wanapenda Uteuzi, Lakini Kuna Watu wa Ajabu!, Hawataki Kabisa Uteuzi wala Kazi za Malipo Manene!.
Kuteuliwa wadhifa wowote na rais wa JMT ni heshima kubwa, hivyo wateuliwa hufurahi kuheshimishwa, hivyo kuna wengi wanautamani sana u DC, U DAS, DED RC etc, amini usiamini, kuna watu fulani ambao hawazimikii kabisa uteuzi wowote wa ubwete!, au kazi za malipo manene!. Watu hao sio tuu ni wazuri at what they do, but they love what they do, and they are the best at what they do, ukiwateua watu hawa na kuwa u DC, japo u DC ni cheo kikubwa, lakini uki compare watakacho fanya kwenye U DC compared to what they do, it's a waste!. Just imagine unamchukua mtu kama Profesa wa Chuo Kikuu kama Prof. Shivji, ateuliwe DC!.