Kwanini Wahindu wanawachukia sana Waislam ambao ni ndugu zao na kuwapenda Wakristo na Wabudha?

Sawa, usichanganye Utalii na kuishi, UAE ni nchi ya Kiislamu na ukitaka kuishi huko wana masharti na kanuni za Kiislamu ambazo ni lazima uzifwate!
Nakushauri usome kwanza kabla ya kuandika unachotaka kukiwasilisha. Nakupatia sehemu ya ufafanuzi wa sheria za UAE. Kwa ufafanuzi zaidi tembelea hata google utaelewa zaidi. Kwani si busara kuweka mjadala suala ambalo lipo wazi.
Ni kama nchi yetu si unafahamu vyanzo vikuu vya tulipochopoa na kuunda sheria zetu ni wapi(?).. Halikadhalika ndivyo kwa UAE.
 

Attachments

  • Screenshot_20220813-223822.png
    41.6 KB · Views: 13

Ukisoma hicho ulipost kinasema kwamba UAE inafwata Sharia law, sasa kuna kipi kingine cha kujadili hapo? Sharia = Uislamu!
 
Kila kona ya hii dunia Dini ya kiislamu ni shida. Inapigwa vita na wazungu , wachina na wahindi na shida ni ile ile waislamu wanataka kulazimisha dini yao ifuatwe kwa nguvu kitu ambacho akikubaliki kwa dunia ya saiv ambayo dini ni hiyari ya mtu.
Uislamu unaujua? Sheria gani inasema lazima ufuatwe? Mbona mnajiropokea tu
 
Kama huna ujuzi na kitu ni bora ukakaa kimya kuliko mtu mzima kujidhalilisha kama hivi

Haya wewe mtu mzima mwenye ujuzi sema kwa nini Waislamu na Wahindu hawapatani na wanagombana? Kwa nini India na Pakistani ziligawanywa wakati zilikuwa nchi moja?
 
Ukisoma hicho ulipost kinasema kwamba UAE inafwata Sharia law, sasa kuna kipi kingine cha kujadili hapo? Sharia = Uislamu!
Mimi ni Muislam. Nimeusoma Uislam na bado naendelea kuusoma Uislam.

Ukisema unafuata sharia kwa maana muungozo wako wote wa masuala ya mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla utafuata muongozo wa sharia ambazo ni za Kiislam. Nazo zinatoka kwenye:

-Quran
-Sunna
-Ijtamaa (ya wanawazuoni)
-Qias

Na hapo hakuna mbadala wa kutumia sheria nyengine zaidi ya hizo.

UAE chanzo chao kikubwa cha sheria zimetoka kwenye sheria za Kiislam. Hii sentensi unaielewa Bw. ndugu? Na ndiyo maana kuna option hata kwa masuala ya ndoa ikiwa mtu ni mkazi wa UAE lakini si raia wa pale ana uhuru wa kuchagua sheria za nchini kwake zimuhukumu. Nenda Saudi Arabia pendekeza hilo nafikiri watakupatia majawabu mazuri.

Ama kwa mfano mwengine: Ni kama sisi Tz vyanzo vyetu vya sheria tumetoa kwenye sheria za kiislam za kijadi n.k

Sijui umenielewa?

Nakushauri Bw. ndugu, tembelea hata google kuhusu mfumo wa sharia kwa UAE utaelewa kwa mapana.
 
Chanzo kikuu na uadui wa Waislamu na Wahindu nchini India ni Ukoloni wa Uingereza waliyokuwa wakiwatawala. Hao ndiyo walisababisha sumu ile waliyoipandikiza, iwe kichocheo cha uadui hadi leo hii. Walitumia sera yao ya DIVIDE AND RULE wakawagawanya kwa makundi kwa mujibu wa dini zao na sababu nyingine za kisiasa, waliwafanya wasiwe na umoja ili waendelee kuwatawala vyema.

Chuki kubwa ilizaliwa baada ya kuwagawa hivyo na ndiyo hiyo inayowatafuna hadi leo hii, ila kabla ya ujio wa mkoloni hakukuwa na uhasama baina yao.


=====

Huku Afrika hii sera yao imepelekea ukabila mkubwa sana baina ya watu wa nchi moja, wakoloni waliamua kuvunja umoja wa watu ili wasiweze kuungana dhidi yao kwenye utawala wao. Tanzania yenyewe tungeingia pabaya sana kwenye uhasama huu wa kikabila, kama isingekuwa kupigwa vita mapema.

Huko India walilenga imani zao maana ndiyo zilikuwa kila kitu, na huku wakalenga kabila kwani ndiyo zilibeba nguvu kubwa. Matokeo ya sumu yao ndiyo chuki ipo hadi leo hii
 
Kuna uelewa mbaya juu ya kila wanao jilipua kuwa Ni waislamu kwasababu Tu Wana majina ya kiislamu au mavazi ya kiislamu....au inchi wanazo toka.

Lkn pia sio kila wanao jilipua wanapigana Vita ya kidini....kuna wengine wahuni ambao hata Dini hawaijui wanafuata matamanio Yao Tu.

Kwanza Uislamu unasema kuwa anayeua mtu mmoja basi ni Sawa Sawa na kama ameua watu wote na mwenye kuokoa Maisha ya mtu mmoja ni Sawa Sawa nakuokoa Maisha ya watu wote....kuna ambao Wanapaswa Kuuwawa Kwa haki.

Mfano kama umeua nafsi Kwa makusudi basi nawe itabidi uuwawe...kwani ktk kulipiza kisasi kuna kuwa na Uhai mzuri...Kwa maana watu wataogopa kuuwana ovyo.

Sasa waislamu Kwanza wanaruhusiwa kupigana Tu endapo maadui wameanza chokochoko dhidi ya waislamu...na kwahiyo watapigana kuondoa udhalimu na kusimamisha haki katika jamii na endapo hao madhalimu wakasilimu amri nakuacha basi waislamu nao wanatakiwa waache kupigana.

Vile vile katika hiyo Vita waislamu hawatakiwi kuwapiga makundi maalumu...kama wazee,wanawake na watoto isipokuwa wanaume mashababi ambao ndio hushika silaha na kama haitoshi haitakiwi kuharibu mazao wala kuwapiga wanyama.

Sasa hapo ndo utaona tofauti ya wahuni ambao wanajificha nyuma ya Uislamu...wao wanavaa mabomu na kuua watoto,wakina mama nawazee na watu wasio na hatia...hao sio waislamu wanao ijua Dini Bali ni wahuni Tu.

Hiyo ndio Hali halisi linapokuja swala la Dini ya kiislamu
 
Ndio nimeuliza wapi walilazimishwa. Una mtoto alilazimishwa kuitwa George au Anna? Kama umekubali taratibu za dini husika unawezaje sema umelazimishwa
 
Haya wewe mtu mzima mwenye ujuzi sema kwa nini Waislamu na Wahindu hawapatani na wanagombana? Kwa nini India na Pakistani ziligawanywa wakati zilikuwa nchi moja?
Pitia post #34 siku nyingine kama kitu hukijui bora ukae kimya kuliko kuleta chuki zako za kidini
 
Ndio nimeuliza wapi walilazimishwa. Una mtoto alilazimishwa kuitwa George au Anna? Kama umekubali taratibu za dini husika unawezaje sema umelazimishwa

Ndiyo, ilikuwa ni lazima kuwa na jina la Kizungu bila ya hilo jina hakuna kubatizwa na bila kubatizwa hakuna kwenda Shule ilikuwa hivyo wakati wa Ukoloni ambapo walikuwa wanaeneza Ukristu,

ofcourse leo hii inaonekana kama hiari kwa maana imeshazoeleka lkn mwanzoni haikuwa hivyo ilikuwa ni lazima uchukuwe Jina la Kizungu ili uwe mkristo na kubatizwa na hivyo ndivyo Watanzania walivyopata majina ya Kizungu, haikuwa hiari au unafikiri Wazee wa kijijini walijuaje kama kuna jina kama Elisabeth au Edward hadi kumpa mtoto wao?
 
Huo ni uzembe na udhaifu wa jamii yako. Dini ni tamaduni za watu wengine, wakija kuleta marupurupu ya tamaduni zao kupitia dini lazima ukubali taratibu zao.

Ni licence agreement uliingia nao, ungeona sio haki usingesoma kwao. Kulazimisha vile ni kwakuwa imani yao inaona ndivyo ilivyo sahihi kama ambavyo miungu ya Kimasai ilikuwa inaona albino ni mkosi, kama ungeenda kujiunga nao ungetakiwa kuamini hivyo
 
Sasa hao wanaofanya hivyo ndiyo wahuni wa kwenye dini!

Uislamu umekataza kumshambulia mtu kisa kakutukana! Hata Mtume alipoulizwa na Arab jamii ya Bedui ya kuwa umetujia na nini? Mtume alianza amekuja na ubinadamu kwanza...

Ni kweli kwenye Quran kuna kifungu kinachomruhusu muislam kujitoa muhanga na endapo atafanya hivyo atapewa mabikra 72 akifika ahera? Hii ni kweli au stori tu za mitaani?.
 
Lakini kiongozi wa dini ya kiislam huko iran aliagiza huyo mwandishi auwawe maiti ipelekwe iran
Sasa hao wanaofanya hivyo ndiyo wahuni wa kwenye dini!

Uislamu umekataza kumshambulia mtu kisa kakutukana! Hata Mtume alipoulizwa na Arab jamii ya Bedui ya kuwa umetujia na nini? Mtume alianza amekuja na ubinadamu kwanza
 
Ameshindwa kuweka wazi kuwa lazima uishi kwa kufuata uislam
Sawa, usichanganye Utalii na kuishi, UAE ni nchi ya Kiislamu na ukitaka kuishi huko wana masharti na kanuni za Kiislamu ambazo ni lazima uzifwate!
 
Lkn ukiangalia tabia za waislam karibu dunia nzima zinafanana hapo uingereza anasingiziwa kwasababu ya mapungufu ya dini nyengine
Chanzo kikuu na uadui wa Waislamu na Wahindu nchini India ni Ukoloni wa Uingereza waliyokuwa wakiwatawala. Hao ndiyo walisababisha sumu ile waliyoipandikiza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…