Adilinanduguze2
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 1,386
- 1,919
Umejitahidi kutoa hoja ingawa zote zina mapungufu nilichopenda hukutumia lugha mbovuUkristo haujawahi kuamini kwamba ni lazima kila mtu amuamini Mungu wao. Wapi Ukristo uliwahi tumia nguvu kueneza injili?
Wahindu ni dini kongwe kuliko Uislamu. Mtume kazaliwa kakuta Wahindu wapo na mambo yao kina Krishna sijui ng'ombe na Budha. Mara Waislamu wakaenea mpaka maeneo ya Wahindu na kutaka kubadili tamaduni. Uislamu haujui kuadapt tamaduni za eneo husika ndio maana hadi Botswana wanakula tende na kuvaa kanzu, wa Bolivia watafanya hivyo, wa Honduras watafanya hivyo, wa Burma hivyo. Wakati tende ni asili ya Waarabu hata kabla ya Uislamu kuwepo zililiwa, usingekuwepo muujiza wa kuwalisha vanilla zao lililokuwa Mexico tu hapa duniani. Kanzu kabla ya Uislamu kuwepo zilivaliwa, wasingevaa mashuka ya kimasai kwani wangeyatoa wapi? Hata kuhiji ni ukouko Uarabuni, wasingehiji Venezuela hawakuwa hata wanaijua.
Dini inampasa mtu kutumia lugha moja ambayo haijazinduliwa na dini hiyo ila ni utamaduni wa Waarabu. Mwishowe jamii zenye tamaduni imara na za kale zaidi zinapata ugumu kuukubali Uislamu. China, Japan, India wote wana historia ya maelfu ya miaka na imani zao. Leo uwaambie kufuga ndevu, kufunga mwezi mtukufu, kuoa wake wanne na mambo ya sunna wanakushangaa. Fujo inakuja pale unapowalazimisha.
Dini kuu zote ni dini za watu waliokuwa na expansionism na wauaji. Kama Wahindu wangekuwa na expansionism watu wengi duniani wangekuwa Wahindu
1. Hoja yako ya kwanza ni ile hoja kongwe ya kibubusa(old dogma)
Kwamba Ukristo haukuenea kwa Upanga. Hii ni hoja dhaifu sana ktk ulimwengu wa sasa huitaji kuwa Mwanahistoria kulijua hilo unahitaji udadisi zaidi
- Soma chanzo cha Crusades kuanzia mwishoni mwa karne 8 mpaka karne ya 12
- Tafuta Documentaries na Makala kuhusu Crusades
2. Hoja yako ya pili kubwa ni kuwa Buddiism, Hinduism na Confuciusim ni dini za zamani kuushinda uislam kitu ambacho sio cha kweli
Na hii ilikuwa mbinu ya muda mrefu ya European Orientalists ku limit uislam tokea wakati wa Mtume Muhammad SAW tu. wakaupa jina la Mohammedanism kitu ambacho si sahihi, labda kama unazungumzia kitu kingine, lakini unapozungumzia Uislam ulianza kwa Nabii Adam AS mpaka kufikia kwa Muhammad SAW. Na hii hata ukienda Tandale kwa Ustaadh yoyote atakwambia hivyo
Mind you vitendo vya ubaguzi ambavyo vimekuwa vikitendwa na Wahindu na Mabudha vimekuwa vikichochewa zaidi na SIASA wanasiasa wanajua na wanaogopa kwamba hizo dini zikisambaratishwa na Uislam watakosa ngao ya kujificha
Kitu kingine nimekiona umetaja Tende, Kiarabu, Ndevu na Vazi la Kanzu.
Mtu yeyote mwenye elimu butu ya Sayansi Jamii anajua kwamba kila imani/itikadi HUSAFIRI na utamaduni wake hakuna imani inayosambaai bila kufuatana na Utamaduni wake, kwa mfano ktk Ukristo utaona;
- Mahitaji ya Christmas Trees & Flowers during Christmas
-Uvaaji wa Suti hata kwenye joto
-Matumizi ya Lugha ya Kiingereza na Kilatini
3. Umezungumzia kuwa hizo dini za Hinduism, Buddhism na Confusions kuwa zenyewe hazina expansion agenda
Umeshindwa kuelewa kuwa contents za dini hizi ziko Limited kwa watu fulani wa eneo fulani TU.zimekosa sifa ya UNIVERSALITY Kwa wa mfano Hinduism hiyo utambulisho wake tu umebeba identity ya kabila fulani tu ambao wako karibu na maeneo yanapakana na Hindus River
Wewe Mzulu Mluguru au hata Mhindi ambaye sio wa kabila la Hindu hiyo dini inakuhusu nini
Na ndio maana zimedumaa pale pale zikiwa na mtaji mkubwa wa UBAGUZI NA UADUI
Kwa kumalizia tu haya hebu Google
-Zakir Naik
-Salum Boss/ WEREVU MNO AU WAJINGA MNO
- Bad Muslim, Good Muslim,,,,,,,,,,, Prof Mahmoud Mamdani