Kwanini Wahindu wanawachukia sana Waislam ambao ni ndugu zao na kuwapenda Wakristo na Wabudha?

Kwanini Wahindu wanawachukia sana Waislam ambao ni ndugu zao na kuwapenda Wakristo na Wabudha?

Hawa wahindi wa india ambao ni waamini wa dini ya kihindu wanawachukia sana waislam wanakwambia wangeweza wangewateketeza kwa bomu kama lile la USA kwenda Japan

Hii chuki inatokana na nini? Tukumbuke hawa wote ni wahindi jamii moja

Zamani kutokana na hii chuki kulipelekea waislam kujitenga na kuunda nchi yao ya Pakstan
Ila kuna waislam walibaki kwenye nchi yao ya asili ya India na kupelekea mgogoro hadi leo

Hawa wahindu wanaupendo wa dhati kwa wakristo na wabudha ila hawataki kuwasikia wahindi ambao ni waislam

Na ukichunguza kwa kina wahindi wengi waislam walikimbilia Africa na nchi nyingine kutokana na hizi chuki

Nchini India jamii za kiislam zinaishi kwa wasiwasi sana na ukibainika muislam anaona binti wa kihindi anaweza kufa kifo cha kutatanisha

Cha ajabu kule Pakstan jamii ya kihindi inachuki na ukristo kuliko wahindu

Sijawahi kushuhudia huu uhasama wa kidini nchi yeyote zaidi ya India
Dini ya chuki ipo, na inajulikana
 
Shida ni Mafundisho ya Dini ya Uislamu, Waislamu wanafundishwa kwamba Mtume Muhammad (SAW) ndiyo wa mwisho kwa maana hiyo hakuna mwingine hivyo basi binadamu wote ni lazima wamkubali na kumfwata, shida inaanzia hapo, tatizo la India ni kwamba Uislamu hauutambui Uhindu na Waislamu wanaamini kwamba watu wote mwishowe ni lazima wawe Waislamu.

Hata Ukristu ulikuwa hivyo zamani lkn tofauti ni kwamba Ukristu unabadilika na muda wakati Uislamu uko vile vile, hivyo siyo India tu hata hapa Tanzania ni swala la muda tu kabla hakijanuka, kwa sababu ya kuamini hivyo nilivyoandika hapo juu, kwa maana nyingine kwa Muislamu kama wewe siyo Muislamu kwa upande wake ni kwamba ubinadamu wako una mapungufu au kasoro hata kama hatokwambia usoni lkn deep inside anaamini hivyo, …

Wapi uisilamu umetutaka kuwalazimisha mtoke katika imani yenu? Hebu tunaomba hiyo aya inayolazimisha
Imani nikitu hatari sana nihisia za ndani kabisa kwa mwanadamu kwa hiyo kila mtu anacho amini hapo ndio utata unakuja mwingine kulazimisha kuamini asicho kiamini mwisho mauaji, chuki na kutengana

MUNGU ATUNUSULU KWA TAIFA LETU.

Kama hujui uliza kwanza.

Ukitaka aya Nitakuletea
 
Shida ni Mafundisho ya Dini ya Uislamu, Waislamu wanafundishwa kwamba Mtume Muhammad (SAW) ndiyo wa mwisho kwa maana hiyo hakuna mwingine hivyo basi binadamu wote ni lazima wamkubali na kumfwata, shida inaanzia hapo, tatizo la India ni kwamba Uislamu hauutambui Uhindu na Waislamu wanaamini kwamba watu wote mwishowe ni lazima wawe Waislamu.

Hata Ukristu ulikuwa hivyo zamani lkn tofauti ni kwamba Ukristu unabadilika na muda wakati Uislamu uko vile vile, hivyo siyo India tu hata hapa Tanzania ni swala la muda tu kabla hakijanuka, kwa sababu ya kuamini hivyo nilivyoandika hapo juu, kwa maana nyingine kwa Muislamu kama wewe siyo Muislamu kwa upande wake ni kwamba ubinadamu wako una mapungufu au kasoro hata kama hatokwambia usoni lkn deep inside anaamini hivyo, …
Ukristo unabadilika kutokana na miaka inavyoenda ndio maana papa anahalalisha ndoa zajinsia moja !!!??
Dini zipo nyingi ila Uislam ndio dini ya halali hili halina ubishi ingawaje ukimuona mtu anakulazmisha kua muislam huyo anamatatizo yake binafsi kama muislam ila sio tatizo la uislam
Kama wewe unaona dini yako sio dini pekee na ya maana kwamtazamo wako kwanini usiwe budha ukawa mkristo c kwasababu unaamini kua ukristo ndio dini yakweli
Mliaminishwa mashuleni kwenu kuoa wake wanne ni illegal leo munaaminishwa ushoga na usagaji ni halali(uislam kwakujua hili ukaeka wake wanne)
Waislam ndugu zao waislam hao wahindu waaabudu ng'ombe cjui jua wakatafte ndugu zao
Shida yenu mnauchukia ukweli lakini tutawapa tuuu
Mwisho uislam haujabadilika nahautabadilika mpaka kiama mkitupenda mkituchukia huo ndio ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukristo haujawahi kuamini kwamba ni lazima kila mtu amuamini Mungu wao. Wapi Ukristo uliwahi tumia nguvu kueneza injili?

Wahindu ni dini kongwe kuliko Uislamu. Mtume kazaliwa kakuta Wahindu wapo na mambo yao kina Krishna sijui ng'ombe na Budha. Mara Waislamu wakaenea mpaka maeneo ya Wahindu na kutaka kubadili tamaduni. Uislamu haujui kuadapt tamaduni za eneo husika ndio maana hadi Botswana wanakula tende na kuvaa kanzu, wa Bolivia watafanya hivyo, wa Honduras watafanya hivyo, wa Burma hivyo. Wakati tende ni asili ya Waarabu hata kabla ya Uislamu kuwepo zililiwa, usingekuwepo muujiza wa kuwalisha vanilla zao lililokuwa Mexico tu hapa duniani. Kanzu kabla ya Uislamu kuwepo zilivaliwa, wasingevaa mashuka ya kimasai kwani wangeyatoa wapi? Hata kuhiji ni ukouko Uarabuni, wasingehiji Venezuela hawakuwa hata wanaijua.

Dini inampasa mtu kutumia lugha moja ambayo haijazinduliwa na dini hiyo ila ni utamaduni wa Waarabu. Mwishowe jamii zenye tamaduni imara na za kale zaidi zinapata ugumu kuukubali Uislamu. China, Japan, India wote wana historia ya maelfu ya miaka na imani zao. Leo uwaambie kufuga ndevu, kufunga mwezi mtukufu, kuoa wake wanne na mambo ya sunna wanakushangaa. Fujo inakuja pale unapowalazimisha.

Dini kuu zote ni dini za watu waliokuwa na expansionism na wauaji. Kama Wahindu wangekuwa na expansionism watu wengi duniani wangekuwa Wahindu
Bila yashaka unamuongelea s.a.w ila nani alokwanbia uislam umeanza enzi ama wakati wa s.a.w
Uislam ulikuepo kabla ya s.a.w na ukawepo wakat wake na upo hata baada yake s.a.w
Hakuna dini inayoiona dini nyengine kua sahihi nandio maana kuna dini zaidi ya moja sababu kila mtu anaamini anavyoona yeye inafaa kuamini
Mwisho:-hakuna haki ya muislam kumuua asie muislam kwa namna yeyote ile iwayo wanaojiripua na kuua watu wakiwa wametia nia yakufanya hvyo kabla hawajatekeleza wanakua sio waislam nawatafufuliwa wakiwa makafir
UISLAM DINI SAHIHI ZAIDI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni uislamu.

Uislamu ni ngumu kua compatible na jamii nyingine kwa amani.

Waislamu hujiona wao ndio wenye haki kuliko jamii nyingine. Waislamu hujiona wananyanyasika kuliko jamii nyingine.

Waislamu hawana jambo dogo la kutumia tu akili. Kumbuka mtoto aliwahi kukojolea quran mbagala walitaka kumuua bila kuwaza kua huyu ni mtoto na reasoning yake bado ndogo, wao walitaka kumuua.

Waislamu hudharau tamaduni za jamii nyingine hivyo kusababisha migogoro isiyoisha, mfano, wao tu ndio wanataka wawe wanachinja, wengine wakichinja ni kosa. Kwamba tamaduni za jamii nyingine ni za hovyo ila utamaduni wa kiarabu ndio sahihi.

Kosa lingine la uislamu ni kwamba utamaduni wa kiarabu ama wa mashariki ya kati uko embeded kwenye uislamu, hivyo ni ngumu kutofautisha kati ya uislamu na uarabu. Sasa wao wakienda mahala wanataka walazimishe utamaduni wa kiarabu kwa tamaduni za watu wengine.

Ukishaona dini ambayo wenyewe hawaelewani kwa sababu ya dini basi ujue hiyo dini ni Magumashi. Iran haielewani na Saudi Arabia kwa sabau ya kidini. Hawa washia hawa wasuni. Yaani tofauti zimeingia hadi kwenye siasa.

Alkaida haelewani na talibani, Janjaweed haelewani na mujahideen, Isis haelewani na Alkaida, alshababu haelewani na alikaida, talibani haelewani na alshababu wakati wote wanamtetea mungu mmoja. Na hawaelewani kwa hatua ya kuuana, wakikutana damu inamwagika, wanachinjana.

Hii dini ni tatizo.
 
Kwann kiongozi wa dini ya kiislam aliagiza kuuwawa kwa salman km hiyo dini haispot mauaji?
Kwani kufa kwa Imam ndiyo mwisho wa ibada?

Magufuli alipofariki Afande Sele alirusha clip yake ya huzuni mpaka akaghafilika na kumtusi Mungu.

Mmoja mwa miongoni mwa masheikh nchini Tanzania alicharuka na kumuombea dua mbaya.

Yeye ni kiongozi na ana sehemu yake kwenye jamii lakini jawabu lake lilikuwa sahihi kwa Afande Sele? Hapana! Tulijua Sheikh ana mahaba na Mungu makubwa tu ila nae ameghafilika kutokana na kuona kipenzi wake Mungu kutamkwa vibaya. Ikawa imekwisha hiyo!

Hivyo, kuna mengine yanayosemwa na viongozi kutokana na wao jinsi wanavyolipokea binafsi. Kuna mengine kiongozi anayawasilisha baada ya kukaa shura na wenzake na kutoa tamko la ujumla kwa jamii yake.

Na hali hii hata kwenye siasa inafahamika. Mfano Biden alivyokuwa Poland alisema Putin anapaswa aondolewe madarakani. White House ilikanusha hii taarifa kwa kujibu kuwa huo si msimamo wa WH bali ni wa Biden binafsi.

Tafsiri yake viongozi nao wanateleza! Nao ni binadamu. Muda mwengine wanaghafilika kulingana na uzito wa taarifa wanazozipokea. Ila muhimu kwa Waislamu elimu yao ipo wazi. Na haistaajabishi maamuma kuwa na elimu kubwa zaidi kuliko viongozi wao. Na ndivyo jamii ya Kiislamu ilivyo! Hivyo usishangae wakimkosoa kiongozi wao. Muhimu heshima na kutambua nafasi yake viwemo.

Mungu ndiye mjuzi zaidi.
 
Kama tatizo lingekuwa Waislamu kwani Dubai wengi wao ni wa dini gani na msuguano kama huo umeuona?

Qatar napo kuna Wahindi wengi msuguano kama huo umeuona?

Kuwait kuna Wahindi wengi msuguano wa namna hiyo umeusikia?

Kote huko Wahindi wana nyumba zao za ibada.

Kuna kipindi ilikuwa ni mwezi wa Ramadhani futari iliandaliwa kabla ya kuswali magharibi ili baada ya swala watu wale. Kwa ghafla kundi la nyani likavamia na kula futari. Kumaliza swala nyani wanakula futari.

Viongozi wakasema tusiwafukuze! Wakaenda temple ya karibu kuwaambia kuna suala limetokea kwenye nyumba yetu ya ibada tunaomba mtusaidie kuli tatua. Walipofika wakakuta nyani wanakula futari, walifurahi sana! Wakalipia gharama ya chakula chote kwa ujumla. Sikujua ina maanisha nini! Kuuliza nikaambiwa ile temple nyani ni mungu wao! Tungeliwakimbiza laiti wangelituona ingelikuwa mtafaruku mkubwa! Wahindu wana miungu mingi! Kuwa makini na kila kiumbe ukiwa kwenye jamii yao hususani India.

Kwa Waislam kuna dhehebu linaloitwa Salafi. Salafi nao wamegawanyika; kuna wa moto kiasi na wa moto kabisa. Hawa chao ni sahihi cha kwako si sahihi, ukimfuata upo sahihi usipomfuata umepotea. Hawa ndoa zao wanafungishana wao tu! Wengine wanafika mbali kabisa asie Muislam kwao wanamuona amekuja bahati mbaya duniani. Fahamu pia; mpaka Waislamu dheheb la Sunni kwa upande wa Salafi wanawaona Sunni wamepotea hivyo utapewa majina mabaya kweli.

Sasa Muhidu mwenye dini nyingi na miungu mingi wawe ndani ya jamii moja na Salafi unategemea nini? Chuki itakuwepo baina yao na uhasama mkubwa!
Nimejifunza jambo
 
Wewe buana unachekesha

Wewe unamamlaka gani ya kuutambua ukafkri?
Au mnalishana matango
Vipi wewe icho kitabu cha quran kilichoitwa satanic verses kwann mlitangaza kumuua uyo sakman? Hamuon kuwa mnajpiga makof kwa ujinga?
Bw. Mkubwa! Mimi sizungumzi kwa fikra iliyojengwa baada ya kile kilichowasilishwa na vyombo vya habari na majarida mbalimbali ndipo akili ibebe majumuisho na kutoa jicho la mustakabali hiki kitu kipo hivi!

Haya masuala ya kielimu! Mustakabali wake na minong'ono yake inapaswa kubebwa na jahazi lilojengwa kwa elimu. Na captain wake awe ni mjuzi haswa wa kukiendesha kwani inahitajika ujuzi wa kielimu ili safari iwe salama.

Mimi nazungumza kwa nilichokisoma, wewe unazungumza kwa kusikia kutoka vyombo vya habari, majarida na kwa baadhi ya viongozi wa dini nyenginezo wanaobebwa na msukumo wa chuki.

Mungu aniongoze mimi na wewe tuwe na moyo wa upendo. Kwani njia rahisi na fupi ya kufika kwa Mungu ni upendo.
 
Ukristo unabadilika kutokana na miaka inavyoenda ndio maana papa anahalalisha ndoa zajinsia moja !!!??
Dini zipo nyingi ila Uislam ndio dini ya halali hili halina ubishi ingawaje ukimuona mtu anakulazmisha kua muislam huyo anamatatizo yake binafsi kama muislam ila sio tatizo la uislam
Kama wewe unaona dini yako sio dini pekee na ya maana kwamtazamo wako kwanini usiwe budha ukawa mkristo c kwasababu unaamini kua ukristo ndio dini yakweli
Mliaminishwa mashuleni kwenu kuoa wake wanne ni illegal leo munaaminishwa ushoga na usagaji ni halali(uislam kwakujua hili ukaeka wake wanne)
Waislam ndugu zao waislam hao wahindu waaabudu ng'ombe cjui jua wakatafte ndugu zao
Shida yenu mnauchukia ukweli lakini tutawapa tuuu
Mwisho uislam haujabadilika nahautabadilika mpaka kiama mkitupenda mkituchukia huo ndio ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulichoandika ndicho nilichomaanisha more or less, lkn labda unasahau kwamba Uhindu una muda zaidi India klk Uislam, Uislamu haufikishi hata tu miaka elfu mbili 2000 hapa Duniani wakati Hinduism ina > 4 000 years India sasa huwezi tu kuja kusema kwamba Dini yako ambayo ni mpya < 2000 years ni bora kuliko uliyoikuta na wote uliowakuta ni lazima waifwate Dini yako mpya, hilo haliwezekani, …
 
Dini ya kiislamu ni dini pekee ambayo imeletwa na Mungu since memorial, tokea mtu wa kwanza kuja ulimwenguni baba yetu Nabii Adam A.S., Isipokuwa Mungu aliileta kutokana na relevation tofauti tokea miaka hiyo ambapo sisi waislamu tunatambua zama nne muhimu ambazo ni zama za Taurat, Injil, Zaburi, na ya mwisho kabisa ndio hii Qur-an ambayo ameteremshiwa Nabii Muhammda S.A.W, ambapo yeye ndio Mtumwe wa Mwisho katika ulimwengu huu.

Unaposema Wahindi ni dini kongwe kuliko waislamu tutakushangaa sana bora ungeleta maandiko kuhusu ukongwe wa dini na mila za kihindi kwamba zilikuwepo kabla ya Nabii Adam A.S.,
"Dini pekee iliyoletwa na Mungu..."
Dini nyingi sana hudai hivi.

Imagine Wahindu wangekuwa wanataka tuwaue watu wote wanaochinja ng'ombe
 
Kama tatizo lingekuwa Waislamu kwani Dubai wengi wao ni wa dini gani na msuguano kama huo umeuona?

Qatar napo kuna Wahindi wengi msuguano kama huo umeuona?

Kuwait kuna Wahindi wengi msuguano wa namna hiyo umeusikia?

Kote huko Wahindi wana nyumba zao za ibada.

Kuna kipindi ilikuwa ni mwezi wa Ramadhani futari iliandaliwa kabla ya kuswali magharibi ili baada ya swala watu wale. Kwa ghafla kundi la nyani likavamia na kula futari. Kumaliza swala nyani wanakula futari.

Viongozi wakasema tusiwafukuze! Wakaenda temple ya karibu kuwaambia kuna suala limetokea kwenye nyumba yetu ya ibada tunaomba mtusaidie kuli tatua. Walipofika wakakuta nyani wanakula futari, walifurahi sana! Wakalipia gharama ya chakula chote kwa ujumla. Sikujua ina maanisha nini! Kuuliza nikaambiwa ile temple nyani ni mungu wao! Tungeliwakimbiza laiti wangelituona ingelikuwa mtafaruku mkubwa! Wahindu wana miungu mingi! Kuwa makini na kila kiumbe ukiwa kwenye jamii yao hususani India.

Kwa Waislam kuna dhehebu linaloitwa Salafi. Salafi nao wamegawanyika; kuna wa moto kiasi na wa moto kabisa. Hawa chao ni sahihi cha kwako si sahihi, ukimfuata upo sahihi usipomfuata umepotea. Hawa ndoa zao wanafungishana wao tu! Wengine wanafika mbali kabisa asie Muislam kwao wanamuona amekuja bahati mbaya duniani. Fahamu pia; mpaka Waislamu dheheb la Sunni kwa upande wa Salafi wanawaona Sunni wamepotea hivyo utapewa majina mabaya kweli.

Sasa Muhidu mwenye dini nyingi na miungu mingi wawe ndani ya jamii moja na Salafi unategemea nini? Chuki itakuwepo baina yao na uhasama mkubwa!
Naaaam
 
Run my friend run
FB_IMG_16525068853789588.jpg
 
Shida ni Mafundisho ya Dini ya Uislamu, Waislamu wanafundishwa kwamba Mtume Muhammad (SAW) ndiyo wa mwisho kwa maana hiyo hakuna mwingine hivyo basi binadamu wote ni lazima wamkubali na kumfwata, shida inaanzia hapo, tatizo la India ni kwamba Uislamu hauutambui Uhindu na Waislamu wanaamini kwamba watu wote mwishowe ni lazima wawe Waislamu.

Hata Ukristu ulikuwa hivyo zamani lkn tofauti ni kwamba Ukristu unabadilika na muda wakati Uislamu uko vile vile, hivyo siyo India tu hata hapa Tanzania ni swala la muda tu kabla hakijanuka, kwa sababu ya kuamini hivyo nilivyoandika hapo juu, kwa maana nyingine kwa Muislamu kama wewe siyo Muislamu kwa upande wake ni kwamba ubinadamu wako una mapungufu au kasoro hata kama hatokwambia usoni lkn deep inside anaamini hivyo, …
Kwa Tanzania ni ngumu Sana hii kutoa, hebu fikiria viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo wanashirikiana mpaka wanacheza mpira kwa pamoja, ni nani wa kuhamasisha hizo chuki Kama viongozi wetu wanashirikiana?
Hata hivyo Imani ya dini kwa mtazamo wangu inapungua Sana kwa pande zote hivyo Basi issue ya dini haiwezi ikamsababishia mtu amdhuru mwenzake
Ila kama baadhi ya Imani ikitengwa kwenye mema ya nchi kwa ajili ya imani yao, basi hata Kama watu ni waislamu jina au waikristo jina chuki itatokea
 
Salafi wamegawanyika makundi anuwai.

Niliposema kundi la moto zaidi namaanisha aina ya kundi nje ya kile walicho masheikh ( Sheikh Ibn Taymiya, Sheikh Ibn Qayyim, Sheikh Muhammad bin Abdul Wahab, Sheikh Ibn Baaz, Sheikh Alban, Sheikh Ibn Uthaymeen, Sheikh Fawzan) ni batili.

Nimekutana nao hawa! Kipo kitabu kilochoandikwa na Sheikh Muhammad Al Yaqoubi (kwa lugha ya Kiingereza Refutation of ISIS) aina hii imezungumziwa.

Aina hii haikubaliani na chochote kilicho nje ya masheikh niliowaainisha. Mtazamo wao nje ya hao masheikh hakuna dini na ndani ya hao Masheikh hakuna dini. Kwa mantiki hiyo watakuita Khulafi, mtu wa bidaa na wanafika mbali huambia wenzao wanafanya shirk! Hufika mbali huwatenga na kuwatoa kwenye Uislam kabisa na wana jazba kubwa!

Binafsi mimi ni shahidi wa mwenyewe nimekutana nao mimi. Ndio aina ya Salafi niliokutana ninaowazungumzia.
Kwanza Usalafi ni mmoja tu. Na kuugawanya kama wanavyofanya baadhi ya watu hasa wasomi wa Kimagharibi kwenye mapote mfano "Quietist Salafism" au "Salafi Jihadist" ni makosa.

Na hutakuta Salafi eti anasema nje ya Masheikh uliowataja wewe hakuna Dini. Hapo utakuwa unamaanisha kuwa hao "Masalafi" unaowazungumza hawachukui kutoka kwa Imaam Ibn Kathir, Ibn Qudama, al-Khatib al-Baghdadi, Ibn Asakir, Ibn al-Jawzi, Ibn Rajab al-Hambali, Adh-Dhahabi, Imaam Ibn Hajar al-Asqalaani, Imaam Suyuuti, Imaam Mahmud Shukri al-Alusi, Imaam Shawkaani, Imaam Ibn Jarir at-Tabari, Imaam Ibn Khuzaimah, Imaam at-Tahawi, Ibn Abil-Izz al-Hanafi, Imaam Ibn Hazm, Qadhi 'Iyad na wengine weeeengi mno (Allah awarehemu wote) na awahifadhi walio hai.

Pia, Isis na wengine mfano wao sio Masalafi, bali ni Makhawaarij (sijakisoma hicho kitabu cha "Refuting Isis" bado).

Na hao Isis na mfano wao, hawawakubali kabisa baadhi ya Wanachuoni uliowataja. Hawamkubali Shaykh Ibn Uthaymeen, Ibn Baaz, Albani (Allah awarehemu)wala Al-Fawzaan(Allah amhifadhi). Itakuwa huwajui vizuri hao.

Kuna tofauti kati ya Makhawaarij na Masalafi. Bahati nzuri Masalafi wenyewe hujipambanua kwa watu wao ni nani na Da'awah yao wanaifafanua.

Na mwisho kabisa, Masalafi kusema watu fulani ni Watu wa Bida'a wanafanya hivyo kwa dhulma? Na je watu wanaofanya shirki wakiambiwa kuwa wanafanya shirki wanaonewa? Ni makosa kusema hivyo? Mtu akifanya shirki hasa kiukweli na shirki yake ikakemewa ni makosa? Na kuhusu kuwatoa watu katika Uislam, katika watu wanaochunga mipaka, misingi na masharti mno katika kukufurisha, Masalafi wanaongoza. Ni waadilifu mno katika hili. Hutoona wakimkufurisha mtu maalum bila ya kufuata masharti ya Kishari'ah. Ajabu ni kwamba baadhi ya wanaowasingizia Masalafi kuwa wanawatoa watu katika Uislam (bila ya haki) nao hufanya hivyo hivyo, tena kwa ujinga au matamanio tu.

Nakukumbusha ndugu yangu post #10 ya uzi huu ulipomjibu mtu aliyesema kuhusu wanaojilipua, japo aliandika kuwakejeli Waislam, wewe ukasema "Huyo si Muislam!" Huko nako si kumtoa mtu katika Uislam? Ama mimi sijaelewa?

Ni hayo tu. Allah atuongoze sisi na wewe ndugu yangu Hammaz Katika njia iliyonyooka.

Na Allah anajua zaidi.
 
Wahindi ni wapumbavu kama tulivyo waafrika,kuwa na uhasama na dini ambazo zimeletwa na wengine ni ujinga wa kiwango cha lami.

Mwingereza ndio chimbuko LA ugomvi huo-na alifanya hivyo ili iwe rahisi kuitawala India.
na Tz nan aliwafundisha watu kwenda amboni na kibiti ? mna ttzo hkn namna ya kujidefend , popote mlipo hamkubalik kwa tabia yenu ya kutoheshimu iman za watu
 
Kuna uelewa mbaya juu ya kila wanao jilipua kuwa Ni waislamu kwasababu Tu Wana majina ya kiislamu au mavazi ya kiislamu....au inchi wanazo toka.

Lkn pia sio kila wanao jilipua wanapigana Vita ya kidini....kuna wengine wahuni ambao hata Dini hawaijui wanafuata matamanio Yao Tu.

Kwanza Uislamu unasema kuwa anayeua mtu mmoja basi ni Sawa Sawa na kama ameua watu wote na mwenye kuokoa Maisha ya mtu mmoja ni Sawa Sawa nakuokoa Maisha ya watu wote....kuna ambao Wanapaswa Kuuwawa Kwa haki...mfano kama umeua nafsi Kwa makusudi basi nawe itabidi uuwawe...kwani ktk kulipiza kisasi kuna kuwa na Uhai mzuri...Kwa maana watu wataogopa kuuwana ovyo.

Sasa waislamu Kwanza wanaruhusiwa kupigana Tu endapo maadui wameanza chokochoko dhidi ya waislamu...na kwahiyo watapigana kuondoa udhalimu na kusimamisha haki katika jamii na endapo hao madhalimu wakasilimu amri nakuacha basi waislamu nao wanatakiwa waache kupigana.

Vile vile katika hiyo Vita waislamu hawatakiwi kuwapiga makundi maalumu...kama wazee,wanawake na watoto isipokuwa wanaume mashababi ambao ndio hushika silaha....na kama haitoshi haitakiwi kuharibu mazao wala kuwapiga wanyama....sasa hapo ndo utaona tofauti ya wahuni ambao wanajificha nyuma ya Uislamu...wao wanavaa mabomu na kuua watoto,wakina mama nawazee na watu wasio na hatia...hao sio waislamu wanao ijua Dini Bali ni wahuni Tu.

Hiyo ndio Hali halisi linapokuja swala la Dini ya kiislamu
Umemaliza kila kitu MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom