Mkuu ndio maana haya yangu ya mwisho niliandika dini kuu zote zilikuwa na expansionism na haya ndio matokeo yake. Hata hivyo hakuna sehemu Wakristo walienda kuanzisha vita, vita yao ilikuwa ni response ya wao kupigwa na kuonekana mabwege. Hadi Constantinople inapigwa wapo tu kisha unawaita wenye fujo.
Watu kama Mehmed II walishaapa kuufuta Ukristo ndio maana Wakristo hata mahasimu waliungana. Hadi Spain ilikuwa ishakuwa dini nyingine, crusader ilianza pale dini moja ilipoamua kuweka chini unyonge na kutumia nguvu.
Hizo tawala za Kirumi kueneza Ukristo ni within their territorial integrity hata kama yalikuwa makoloni. Na dini moja ilisaidia kuondoa upinzani wa kiimani kwa mtawala hivyo sioni kama lilikuwa ni jambo la kiimani pekee lililofanikisha ueneaji.
Hata Siege of Masada ilitokea baada ya Wayahudi kuacha unyonge bora wafe ila hawaachi dini. Medieval times hakukuwa na ustaarabu ukikaa kinyonge unapotea
Nakusoma vizuri mkuu. Lakini kama hoja ni kujilinda (Self-defense/Responsive Aggression) basi hata Uislamu una haki kuitumia hoja hii kujilinda. Mwanzoni kabisa Uislamu unaanza kuhuburi wa mtume Muhammad S.A.W wapagani waliwaua sana Waislamu hadi wengine kukimbilia Afrika Egypt na Ethiopia ambako wafalme wa Kikristo waliwapa hifadhi.
Dini ya Ukristo katika historia imepitia vipindi vikubwa vitatu ambavyo vimeshuhudia mabadiliko ya mpangilio wa dini, uongozi wa kidini, mabadiliko ya kiumini na mabadiliko ya kifalsafa/kimapokeo. Tusipoyanyumbua haya hatuwezi kupata nini haswa kilipelekea Ukristo ukawa kama ulivyo leo:
Kipindi cha kwanza cha Ukristo, kilianza mnamo karne ya kwanza baada ya Yesu kupaa ambapo wanathiolojia wanaamini ni mwaka 34 AD. Kipindi hiki dini ya Ukristo ilikuwa inaongozwa na Mitume wa Yerusalemu na kanisa lilikuwa halijajitenga na Sinagogi. Kwenye Biblia hapa ni kuanzia kitabu cha Matendo ya Mitume 1-10 (Book of Acts).
Kuanzia sura ya kwanza hadi ya kumi ya kitabu cha Matendo ya Mitume, washirika wote wa Ukristo walikuwa ni Wayahudi tu. Falsafa yao ilikuwa ni ileile iliyojikita kwenye mafundisho ya Bwana Yesu, kwamba Mpende Adui Yako, Geuza Shavu la Pili, Ukinyang'anywa Joho toa na Kanzu kabisa. Wakristo walikuwa ni watu walioteswa sana na kuuwawa na Wayahudi na Wapagani.
Kitabu cha Ufunuo wa Yohana (The Book of Revelation), kiliandikwa mwaka 90 AD. Zile zilikuwa ni barua kwa makanisa ya Kikristo yaliyokuwepo Anatolia/Uturuki. Mtume Yohana aliandika kuyaonya makanisa sana saba kwamba waendelee kwenye njia yao hiyohiyo ya kivumilia mateso mpaka kufa, bila kufanya lolote lile kutaka kujitetea.
Kitu ambacho lazima nikubali ni kwamba, tofauti kabisa na Uislamu dini ya Ukristo iliweza kuenea tokea karne ya 1 hadi 3 kupitia kuuwawa na kuteswa na wafalme wa dola la Rumi. Kinachostaajabisha kidogo ni kwamba kadiri ambavyo wafalme wa Rumi waliongeza kuwaua wakristo ndivyo Wakristo waliendelea kuhubiri injili bila woga hadi kuwafanya warumi wengi wavutiwe na kuwa Wakristo.
Martyrdom was a main pillar of Christianity for a consecutive period of three hundred years. Wewe ukijiunga na Ukristo basi unaagana kabisa na familia yako, maana muda wowote unaweza kutupwa kwenye uwanja wa simba au kuchomwa moto hadharani.
Kama nilivyosema hapo mwanzoni, mwaka 412 AD baada ya mfalme Konstantino kushinda vita ya daraja la Milvi (Battle of the Milvian Bridge), ndipo Ukristo ukaanza kubadilika kuanzia muundo, wauamini na falsafa. Ukristo uligeuka kuwa kijidini (a cult) hadi kuwa dini ya taifa la Roma.
Konstantino aliufanya Ukristo kuwa dini halisi yenye ngazi za kiutawala ( A formal religion with Ecclesiastical Hierarchy). Wakristo wengi walipewa vyeo vikubwa ndani ya dola la Rumi, na askofu wa mji wa Roma akawa na ushawishi mkubwa juu ya mfalme na makanisa yote yaliyokuwa ndani ya dola la Rumi (Ecclesiastical Authority).
Kitendo cha kuunganisha dini na dola kilizaa matatizo kwasababu sheria nyingi za dini zilikuwa ni za dola pia, na zinatiliwa mkazo na dola (Religious Laws were enforced by state apparatus). Hivyo wale ambao walikuwa siyo Wakristo wakabaki na uamuzi wa aidha wawe wakristo au watengwe na kunyanyaswa. Ili kupata fursa, upendeleo na vyeo warumi wengi wakawa wakristo.
Mkuu
T14 Armata niliahidi ntarudi, sasa naomba niandike kwa ufupi mno na kutoa mifano.
ENTER THE PAGAN PERSECUTION: Kuna ushahidi wa kutosha unaonesha kwamba Konstantino alianza kuvunja mahekalu ya wapagani na kujenga makanisa. Kuna askofu mmoja aitwae Eusebius alikuwa anasifia kabisa jinsi ambavyo Konstantino alivunja hekalu la mungu Asclepius.
Heri Konstantino, Theodosius alikuwa ana balaa zito mno katika watawala wakristo wa dola la Rumi. Huyu ndiyo alikuwa Nero wa wakristo. Kiufupi alipiga marufuku kabisa hata kufanya ibada na kutoa sadaka kwa miungu ya kipagani. Ukisoma The Theodocian Code utaona misimamo ya wakristo ilivyokuwa kuwa hatari.
Jingine, aliweka amri kwamba watu waende kazini kwenye siku zenye ibada za kipagani. Ukipinga tu ilikuwa inakula kwako. Akafika mbali zaidi kupambana hata na wakristo wenzake waliopinga mafundisho ya utatu mtakatifu.
MABADILIKO YA KIFALSAFA/KIMAPOKEO
Ukiwasoma wanafalsafa wa kwanza wa kanisa (Church Fathers) kama wakina Thomas Aquinas na Augustine of Hippo, ambao maandiko yao yamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wakristo utaogopa na kushanga. Kiufupi, hakuna kujilinda ila ni unazi mtupu (Fanaticism).
Ukisoma kazi za Thomas Aquinas kama Summa Theologica, amendika mambo ambayo yako kabisa kinyume na mafundisho ya Bwana Yesu na mitume wake. Mle ndani amesema watu wanaokufuru, wazushi au wanaopingana na mafundisho ya kanisa (Blashphemers and Heretics) hawatakiwi kutengwa na kanisa, bali pia kuuwawa.
Haya ni maneno yake Mtakatifu Thomas Aquinas "Heretics deserve not only to be separated from the Church by excommunication, but also to be severed from the world by death."
Papa Paulo wa tatu (Pope Paul III)alivyokuwa ameanzisha chombo cha kupambana na wapinga Ukristo (The Inquisition) alitumia falsafa ya Aquinas. Hata Jesuits wanatumia hii falsafa kuhalalosha mauaji yao maovu duniani kote.
Kiufupi, kama ilivyo kwenye Uislamu kwamba mtu akibadili dini auwawe basi hata katika Ukristo iko hivyo-hivyo. Maelfu ya watu walipoteza maisha kwasababu ya hizi mambo. Wafransiskani na Wadominikani walichinjana mno mnamo karne ya 8 kisa walipishana falsafa za kimapokeo.
Mkuu ukisema kwamba Wakristo walipambana ili kujilinda utakuwa unasahau kwamba vita ya miaka thelathini (Thirty Years War, 1618-1648) baina ya falme za kiprotestanti na kikatoliki zilitokana na kupishana mafundisho na siyo kujilinda.
==========================
Ukisoma mafundisho ya Bwana Yesu Kristo, hakuna sehemu aliruhusu Wakristo kutumia upanga au silaha. Hakulazimisha watu wamfuate. Ndani ya karne mbili Wakristo wameishi kwa kuonewa na kuuwawa na Warumi bila kujilinda, na Ukristo ukaendelea mno.
Hili la kujilinda kwa majambia na magenge ya wauaji kama Jesuits, Parabalani, Path-Finders, Knight Templers, Crusaders n.k linathibitisha kwamba Ukristo hauna tofuati kabisa na dini zingine.