Kwanini wahitimu wengi nchini Tanzania lugha ya Kiingereza ni tatizo! Hii ni hadi kwa waalimu na viongozi wakubwa tu!

tafuta pesa acha mpoyoyo mademu wazuri utaishia kuwaona kwenye tv.bado una promote lugha za mabeberu kama vile zitakuletea debe la unga mezani.?
 
tafuta pesa acha mpoyoyo mademu wazuri utaishia kuwaona kwenye tv.bado una promote lugha za mabeberu kama vile zitakuletea debe la unga mezani.?


Wew kilaza situka, hii lugha ya taifa usije kuaibika, hata uwe na pesa kiasi gani utaishia huko chitohori

mwenzako hata vikao vya AU anakimbia kisa kinge......
 
 
Kiingereza ambacho hakina point ndio kipi hicho mkuu
 
Kiingereza ambacho hakina point ndio kipi hicho mkuu

kwaiyo wewe unataka kuniambia kuwa waingereza wote wana point,acha kuaminisha upumbavu wako kuwa wa wengi.Hata zile nchi ambazo kingereza ni lugha ya mama bado vilaza wapo,kwaiyo acha ujinga kuwa kujua kingereza ndo kuyaweza maisha,au ndo kuweza kuwasemea watanzania shida walizo nazo.
 

nazungumzia uwezo wa kuwasiliana na mataifa mengine kwa maslahi mapana ya kwako na taifa kwa ujumla

jikite kwenye maada, tanzania kama una phd hujui Kiingereza lazima tushangae
 
Rais Ramaphosa aliitisha mkutano wa viongozi wa SADC kujadili COVID kwa njia ya mtandao lakini Rais Magufuli akasema hawezi kuudhuria kwa njia ya mtandao ila akapendekeza watu watume hoja kwa maandishi.
 
Hao ni wachache kati ya kundi kubwa lililopo Tanzania
Sahv over 95% ya vijiji Tz ukiongea kiswahili unaeleweka..Hizo lugha mama zinapotea,na wataozipoteza ni hawa watoto wa sahivi... Mimi kama Mimi wazazi wangu walihamia miaka ile kutoka BK kuja Mwanza.Nimezaliwa na kukulia Mwanza hapohapo.Tena pale mjini,mitaa ya Uhuru. Wazazi wangu walienda na Mimi BK siku za sikukuu na penyewe 1 week tunageuza.Hivyo mimi ni kiswahili tu toka nakua hadi hapa nilipo.Nawasilianaje kwa kihaya sasa hapo? Ukinisema nakuelewa ila kukujibu ndo siwezi.Sasa hawa watoto wa karne hii Mama Mzigua,Baba Mhaya wanajulia wapi lugha zao hizi?
 
Inaelekea wewe haujafika vijijini, vijijini kiswahili hakipo na watoto kiswahili kinaishia shule wakifika nyumbani ni kikwao tu, tumeshuhudia kwenye mkutano ya viongozi wanakuwepo watu wa kutafsiri.
 
sasa hapa wizara ya elimu inatakiwa iangalie uwezekano wa kutatua tatizo, dunia ya sasa bila kiingereza jamani utaibika tu hata uwe na pesa kiasi gani
Ni kweli mwishowe mtu anakuwa kiongozi Mkubwa halafu anashindwa hata kuhudhulia mikutano ya kimataifa....... hahahahahahah
 
Ukishaijua ili nn. Kikubwa n lugha inasaidia kuelewana tu. Zipo nchi nyingi tu kiingereza hawakijui na wanauchumi mkubwa tu duniani sisi masikini ndo tunatumia pesa nyingi kwa hizi academy zetu ili watoto wajue kiingereza. Tunazani mtu akijua kiingereza ndio kaelimika sana.
 
hii lugha ni shida hapa tz
chuoni lecturer anafundisha kwa kiswahili yaani notes/kitabu ni cha kiingereza lakini yeye mazungumzo ni kiswahili☺☺☺☺
sasa hapo mwanafunzi atatoka na kitu kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…