Kwanini wahitimu wengi nchini Tanzania lugha ya Kiingereza ni tatizo! Hii ni hadi kwa waalimu na viongozi wakubwa tu!

Kwanini wahitimu wengi nchini Tanzania lugha ya Kiingereza ni tatizo! Hii ni hadi kwa waalimu na viongozi wakubwa tu!

Mkisha kua mahiri kwenye kiingereza, msituletee vita ya kilugha, kama ilivyo pale Cameroon kati ya wanaozungumza kiingereza na wale wanaotaka kifaransa!!!
 
Habari wakuu

Mimi binafsi nimejaribu kuangalia mwenendo wa watanzania, elimu yetu na kujua lugha ya kimataifa (Kiingereza) ambaya usipoijua kwa dunia hii ya sasa basi unapoteza fursa nyingi sana hapa duniani na kuonekana mtu ambaye hujasoma (kukaza) (,"kitu ambacho sio kweli kwa upande mwingine")

Kwanza kabisa wote tunajua kuwa Tanzania lugha yake ya taifa ni kiswahili, hivyo basi, kabla ya kiswahili kuna lugha ya kikabili ambayo huanza kutumia (kiha, kisukuma, kipare n. K).
-Hio ndio lugha ya kwanza kabisa Mtoto anayokutana nayo katika hatua za ukuaji, kumbaka mtoto anapokuwa na umri wa miaka (0-10) anakuwa na uwezo mkubwa wa kujifunza lugha yoyote (hata kihind, kikorea, kiarabu n. K) na kuongea kiurahisi sana bila kutumia nguvu yeyote. Anavyozidi kukua anazidi kupoteza uwezo kujifunza lugha mpya, hapa inabidi atumie mbinu mbalimbali (more practices), japo lugha mama hatoweza kuisahau.

Maisha yetu watanzania, Mtoto anazaliwa lugha ya kwanza kisukuma, hiyo lugha anatumia kama mawasiliano kila sehemu, anakuja kujua kunakishwahili anapoanza darasa la kwanza, (hapa ndipo walimu wanafanya kazi ya kuwambia watoto speak kiswahili). watu wa kijijini hapa watanielewa, miaka yote saba anasoma masomo kwakiswahili anamaliza la saba (15year) kiingereza hajui.

-Anaanza form one ndio anakutana na speak english, (kumbuka huu ni wakati ambao binadamu yeyote inamuwia ngumu sana kujua lugha unless otherwise awe ana practice more frequence kuongea na wenzake), mbaya zaidi hana hao wenzake wa kuongea nao, hata wakitoka shule nyumbani ni kuongea kilugha +kiswahili (kwa mbali, kijijin wanajua). Anakalili masomo, physics, chemistry, civics anafaulu huyoo advance.

Advance hawafundishi kuongea kiingereza, anakalili huko shaaa one ya pcb hadi chuo, chuo hakuna kukosoana hujui Kiingereza, unakalili madesa ya lecture shwaaaa gpa kalii 4.6, shaa unaomba kazi secta yeyote unapata shavu, huko ndiko unaenda kukumbuka kuwa lugha ya Kiingereza hujui.

hayo ndio maisha halisi ya wasomi wetu Tanzania. lugha ya Kiingereza bado ni tatizo.Lugha ya Kiingereza itaendelea kuwa tatizo tu. Hakuna namna, hakuna solution, kama unasolution weka hapa
Pamoja na sababu nyingine nyingi, pia kuna tatizo la mapuuza. Tuna tabia ya kupuuzia mambo madogo madogo mengi kiasi kwamba tumeona ni kawaida kabisa. Naomba nitolee mfano kwenye uandishi wako.

"Watanzania" sio "watanzania"
"Kiswahili, Kiha, Kisukuma, Kipare, English" sio "kiswahili, kiha, kisukuma, kipare, english"
Unaweka mabano kila kona hata sehemu zisizostahili.
Neno "Advance" ulipolitumia wala halijaleta maana yoyote kimantiki, mpaka mtu ajiongeze tu ndio akielewe.
 
Lugha ya Kiswahili toka tupate Uhuru viongozi wa Kitaifa wamekuwa wanaitumia Kisiasa na wala si Kiuchumi.
Tunatakiwa kikitangaza Kiswahili kwa gharama /hasara ya vinaja wanaokuwa au kuzaliwa.
Viongozi wa juu hawajali njisi Kijana wa Kitanzania anavyoabika huko mbeleni kimataifa inapofika wakati wa Kuchangia mada mbali mbali za Kimataifa kwa Lugha ya Kiingereza.
Hayati Mwalimu Nyerere pamoja na kusoma Kiingereza ukubwani lakini pia alikuwa bingwa wa kuongea kwa Kiswahili. Hii ilikuwa ni Karama ya aina yake na hadi leo katika Afrika hajatokea Rais anayeweza kuongea kiingereza cha Kisiasa, Historia, Dini, Sheria n.k kama Nyerere.
 
Back
Top Bottom