Misaada ya kugawa pesa misikiti na kufuturisha watu ? umewahi kuona Bakhresa akigharamia schoolarship ya watoto masikini kwenda kusoma ? labda wa kwenda kusomea uislamu Saudi Arabia..
Nchi hii toka ipate Uhuru hakuna mtu muhimu kushinda Bakhresa, jamaa single handed katatua matatizo kibao ya watanzania. Kama unahisi Msaada ni mpaka mtu akupe hela basi upo mbali sana.
1. Bidhaa zake anajinyima faida ili wafanyabiashara wadogo wapate faida. Kabla ya Bakhresa watu walikua wakiuza soda wanapata sh 50 tu, angeweza kujitajirisha mwenyewe ila akaja akauharibu huo mfumo na kuleta soda mtu anapata faida 180, Coka na Pepsi wakalalamika, ikabidi Serikali ipange bei ila outcome yake mpaka leo watu wakiuza soda wanapata angalau 100. Si soda tu bidhaa ambazo yeye ni Monopoly kama ice-cream zake alikua pasu pasu anagawana na wale wenye Vibaskeli unanunua I've cream 250-300 unauza 500, usione tu watu mtaani wanauza Bidhaa za Bakhresa wanapigwa na Jua, zina Faida especially kama huna Mtaji. Na hili pia lina reflect net worth ya Bakhresa, net worth yake inaongezeka kidogo mno kureflect faida ndogo anayoweka.
2. Soko la Filamu Tanzania, Kabla ya Bakhresa lilikua mfu, watu wanafanya Sanaa ila hawapati hela, sasa hivi kawainua wengi, Kasponsor Filamu nyingi na series.
3. Mpira Tanzania Kabla ya Bakhresa kila. Mtu alikua hautaki mpaka Super Sport waliukataa ila sasa hivi ameifanya ni katika Ligi tajiri Africa.
4. Usafiri wa Maji Kwenda Zanzibar enzi hizo kila siku unaskia Boti zinazama watu wanakufa, sasa hivi usafiri ni wa kisasa na unaenda kwa amani kabisa. Na ameingia tena kwenye biashara ya vivuko.
5. Amekua Akifanya Innovations mbalimbali na kubuni vitu vipya havi exist soko la Tanzania etc.
Cha muhimu zaidi Angalia Sekta ambazo Bakhresa anawekeza zote zinahitaji zaidi Informal education, anamgusa moja kwa moja Mtanzania wa kitaa kuliko Matajiri na wasomi wachache. Huu ni msaada mkubwa kuliko angetoa scholarship kwa maelfu ya watu.