Kwanini wakatoliki wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara na siyo ya utajiri kama vile Mungu alivyosema atatubariki?

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Ndugu..

Ufukara tunajua ni laana na hakuna mtu anayetaka wala kutamani kuwafukara, Mungu mwenyewe alisema atatubariki na utajiri unatoka kwake na tukimuomba atatupatia na kutujazilishia vya kutosha.

Pia Yesu alisema ukiomba jambo lolote kwa jina lake atalifanya hali kadhalika tukaambiwa sadaka yako ilipo ndipo na moyo wako utakapo kua.

Sasa unapo wasikia na kuwaona wakatoliki wakisali rozari .

KWENYE MATENDO YA FURAHA,. utaona wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara ambao ni moyo wa kimasikini kupita kiasi huku wakisahau kwamba Yesu akisema mtu awazavyo moyoni mwake ndivyo alivyo na pia alituambia tuulinde moyo maana ndipo zitokapo chemchem za uzima ,

1: Kwanini hawa wakatoliki basi wanaomba Mungu awajalie Moyo wa ufukara kwanini hawautaki utajiri kutoka kwa Mungu ila wao wanataka wawe mafukara?

2: Je, wana sali na kuamini kitu wasicho kijua?

3: Je, huko Roma- vatican ni kwamba wameweka maombi ya mtego kwa waumini wa kikatoliki ili kuwafunga maisha yao wabakie kua mafukara huku wao wakijitajirisha na kuneemeka na sadaka zao pamoja na harambee za kila kukicha?

Naomba kuwasilisha
 
Attachments

  • Screenshot_20250204-114846~2.jpg
    Screenshot_20250204-114846~2.jpg
    133.8 KB · Views: 4
Atujalie moyo wa ufukara" ina maanisha kuomba neema ya kuwa wanyenyekevu, kutokutegemea mali za dunia, na kuwa na moyo wa kusaidia wengine bila ubinafsi. Au kutokutegemea majini kwenye uchaguzi 🙂🙂

Na si hivyo unavyo fikiria kichwani mwako ✍️✍️.
 
Kuomba moyo wa ufukara na kuomba kama ulivyo andika ni vitu viwili tofauti

Moyo wa ufukara maana yake ni umasikini uliopitiliza kupita kiasi

Ila kwanini kama wanaomba wanachokimaanisha kama wewe ulivyosema kwanini wasikiombe direct kwa Mungu namna hii kwa kusema hivi kumuomba Mungu neema ya kuwa wanyenyekevu, kutokutegemea mali za dunia, na kuwa na moyo wa kusaidia wengine bila ubinafsi. Au kutokutegemea majini kwenye uchaguzi 🙂🙂.
 
Mt 5:3-12​

Mt 5:3-12 SUV​

BHNSUVNenoSRUV
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
 
Jiulize...
Ni mafukara?
Na dhehebu lao lina ufakara?!

Ufukara ni tendo mtambuka,
Kwa lugha nyepesi ni kujishusha..
Mkuu kujishusha siyo hivyo, kujishusha ni kunyenyekea hebu angalia hapa kuhusu huo ufukara

Methali 24:34​

BHNSUVNenoSRUV
Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.

Yobu 30:3​

Katika ufukara na njaa kali walitafutatafuta cha kutafuna nyikani sehemu tupu zisizokuwa na chakula.
 
Hiyo dini imepoteza mwelekeo,tokea papa aseme kukoboana si issue ,sijawahi waamin tena
 
Mt 5:3-12​

Mt 5:3-12 SUV​

BHNSUVNenoSRUV
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Amesema masikini wa roho na siyo fukara wa roho. Pia hajasema wenye moyo wa ufukara ila amesema heri walio masikini wa roho

Pia elewa kunatofauti kati ya umasikini na ufukara na kunatofauti kati ya moyo na Roho
 
Umepewa kifungu unaanza kurukaruka kama maharage jikoni. Ufukara ndio umaskini, moyoni ndio rohoni ni maneno yanayotumika interchangeably. Na ndio maana huwa tunasema jamaa ana moyo/roho nzuri ama mbaya, ya wivu ama ya ubinafsi nk
 
"heri ya walio maskini wa roho maana ufalme wa mungu ni wao".....ego/kiburi katika vyote quality roho yako iepukane na kiburi ambacho kinaleta kujitweza,na kujiona wewe ndo bora kuliko wengine tupo duniani kujifunza,kumiliki na kujitoa /kujitolea ukiwa nakiburi au kukosa umaskini wa roho hutaweza kujifunza,hutaweza kumiliki sababu roho yako inaona inacho kila kitu hata ukaribu na nguvu ya mungu,hutaweza kujitolea sababu umejitweza kupita kiasi...japokuwa mimi sio mkatoliki ila huo ni mtizamo wangu
 
Mkuu kujishusha siyo hivyo, kujishusha ni kunyenyekea hebu angalia hapa kuhusu huo ufukara

Methali 24:34​

BHNSUVNenoSRUV
Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.

Yobu 30:3​

Katika ufukara na njaa kali walitafutatafuta cha kutafuna nyikani sehemu tupu zisizokuwa na chakula.
Naona unatwanga wajukuu wa Dagon The Fish god.
 
Kuomba moyo wa ufukara na kuomba kama ulivyo andika ni vitu viwili tofauti

Moyo wa ufukara maana yake ni umasikini uliopitiliza kupita kiasi

Ila kwanini kama wanaomba wanachokimaanisha kama wewe ulivyosema kwanini wasikiombe direct kwa Mungu namna hii kwa kusema hivi kumuomba Mungu neema ya kuwa wanyenyekevu, kutokutegemea mali za dunia, na kuwa na moyo wa kusaidia wengine bila ubinafsi. Au kutokutegemea majini kwenye uchaguzi 🙂🙂.
Biblia haisomwi kama gazette la Mwananchi, inabidi uisome taratibu kisha uichambue kilichopo ndani yake.

Siyo kila mtu anaweza kusoma na kuilewa Biblia kama ilivyo kupiga chenga hapo kwenye kipande...

Moyo wa ufukara
. "Usijione mungu mtu baada ya kupata utajiri au kiasi Fulani cha mali, bali jione upo Sawa na wengine ambao hawana kwa wakati huo"
 
Lakini biblia ipo wazi siyofumbo gumu kulicompare na maisha kama mnavyotuaminisha .

Ufukara haujawahi kutajwa kwa maana hiyo unayoisema kwenye biblia mkuu.., maandiko yamefafanua kabisa ufukara ni nini
 
Back
Top Bottom