Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Biblia ni falsafa ngumu:Lakini biblia ipo wazi siyofumbo gumu kulicompare na maisha kama mnavyotuaminisha .
Ufukara haujawahi kutajwa kwa maana hiyo unayoisema kwenye biblia mkuu.., maandiko yamefafanua kabisa ufukara ni nini
Rejea swali lako, utasemaje kuhusu Yesu kuwaambia watu,
Mt 5:3-12
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Je, Mungu anataka tuwe wenye huzuni? Mbona andiko jingine linasema, "furahini katika Bwana"?
Katika falsafa ya kiimani ufukara au umaskini unaozungumziwa ni ule wa Roho, siyo mali. Na ufukara wa Roho, ni ile hali ya kujiona wakati wote umepungukiwa, na hivyo kuishi kwa kumtegemea Mungu. Utajiri wa Roho humaanisha kuwa umejitosheleza kila kitu, na hivyo Mungu hana nafasi katika maisha yako.