Kwanini wakazi wengi wa Dar es Salaaam mna roho mbaya?

Kwanini wakazi wengi wa Dar es Salaaam mna roho mbaya?

Wasukuma wana roho nzuri sana, nlikaa shinyanga miaka flan ya 2009, huo ukarimu wao siyo wa nchi hii.

Ila mjini lazima uje kwa booking maisha mjini siyo kama ya mkoani hata pilipili tunanunua.

Unakuta mtu kapanga chumba sebule, ana mke na watoto, halafu eti wewe unakuja mjini unataka ukafikie kwake tena muda mwingine hujamwambiia tu unampa taarifa uko kwenye basi.

Huu ndiyo mwanzo wa kukimbiwa. Mjini hali tete, kuna jamaa ni mlinzi aliniambia analipwa 90000 kwa mwezi na ana mke, nikajiuliza ana survive vipi dar, sasa mtu kama huyo ukitoka mkoani eti ufkie kwake ni kumwongezea umaskini.
Kwa maisha hayo lazima awe na hasira akiona mgeni
 
Niko hapa mbagala nimepanga chumba kimoja ,godoro ,fen ,jiko ,ndoo za maji ,vyombo ,kitanda ,viatu,nguo , mke na watoto wawili kila kitu ni humu humu ...

Chumba kimoja baba ,mama ,na watoto ...

Sihitaji mgen hapa kwangu ,
 
Dar hakuna mashamba ya kulima mahindi tunanunua unga dukani we unataka uchekewe ili ukae muda mrefu
 
Niko hapa mbagala nimepanga chumba kimoja ,godoro ,fen ,jiko ,ndoo za maji ,vyombo ,kitanda ,viatu,nguo , mke na watoto wawili kila kitu ni humu humu ...

Chumba kimoja baba ,mama ,na watoto ...

Sihitaji mgen hapa kwangu ,
Kiufupi familia yako ni STORE KEEPERS
 
Nikija bara nimeenda kwetu nitafikia kwetu. Nikienda mkoa mwngne nitafikia lodge au hotelini.
Mimi uwa sipendi kufikia kwa watu ili niwe huru na nisiingilie mfumo wao wa maisha.
Hakika
 
kwani lazima uje nyumbani kwangu ? ...we fikia Lodge tuonane juu kwa juu....mambo ya kufuatana majumbani ni ya kipumbavu sana....yaishie huko huko porini kwenu
 
Mazingira hutengeneza tabia/mitazamo ya maisha. Dar hakuna mashamba ila maduka tu. So mwenye familia anaishi kwa kubajeti chakula cha familia. Akiongezeka mtu, maana yake mfuko unatoboka zaidi. Sisi mikoani, unagunia zako ndani za mpunga na mahindi. Wageni wakija, unavuta tu gunia, peleka mashineni, msosi wa kutosha. So huna jam na wageni. So, kimsingi watu wa dar ni victim wa mazingira.
 
Dar kugumu sana watu wengi wanaoishi dar Wana stress za maisha hivyo lazima wawe wachoyo saana pia hela ni ngumu sana kwa dar
 
Back
Top Bottom