Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
 
Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
Yohana 4:23
"Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii."
 
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli

Kwani zinazosali ni kanzu?
 
Kobazi watanuna,wao ni sheria na kanuni za tamaduni kiarabu kuanzia kuvaa hadi kula,ila mioyo yao iko mbali na imani,sio unaona pwani na visiwani kunavyoongoza kwa ustable marriages na kutinduana mitaro jumlsha ugaidi na upedophile ndio utapata jibu.
 
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
Kanzu si vazi la ki=dini, ni fashion ya mavazi kwa mashariki ya kati na uarabuni

"In the Mishnaic period, and even in some Islamic countries until the mid-20th century, Jewish men commonly wore tunics instead of trousers"
 
Wakati ule vazi la heshima lilikua ni kanzu wakati huu vazi la heshima ni suti,
Kwamaana hiyo mwandishi alieandika kitabu Cha luka 20:46 ingekua ndo yupo wakati huu angeandika hivi,
jihadharini na walimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia suti, hata yesu kipindi anakuja ingekua ndo wakati huu angevaa suti sio kanzu tena.
 
Hiyo picha ya profile ni yako?
Chonde chonde usiitamani hiyo picha bana. Hujasoma huu uzi?
 
Pia izingatiwe mazingira ya huko Mashariki mwa kati hayaendani na ya huku, Sasa unakuta makobaz yameng'ang'ania kanzu eti yafanane na muarabu
 
Chonde chonde usiitamani hiyo picha bana. Hujasoma huu uzi?
Wewe una shida gani?
Kwani mtu akiulizia kwamba hicho picha ni yako amekutamani.
Mbona uko negative sana?
 
Nimekutahadharisha tu, mkuu maana dunia hii inaelekea mwisho.
 
Mavazi hasa ya wanawake ibadani ni machukizo,

Unaoingia ibadani na nguo ya kubana kimini, halafu utwambie Mungu haangalii mavazi, unasahau kuwa ibadani kuna watu wenye macho ya nyama yenye kuona uchi wako.

Wanawake badilikeni, acheni mavazi ya kikahaba,

Vaa, funika uchi wako ndio ibada yenye maana.
 
Mwisho wa wapi mkuu?
Mwisho wake. Huna habari kwamba dunia hii itakunjwa kama karatasi na kuchomwa moto? Soma Ufu 6:14 na 2 Petro 3:10–12
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mwisho wake. Huna habari kwamba dunia hii itakunjwa kama karatasi na kuchomwa moto? Soma Ufu 6:14 na 2 Petro 3:10–12
weka time frame vizazi vijavyo vifanye reference
 
Back
Top Bottom