Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

weka time frame vizazi vijavyo vifanye reference
Hakuna timeframe. Yesu anasema tukeshe kwakuwa hatuijui siku atakayokuja. Anaweza kuja hata usiku huu. Kuanzia siku atakayokuja ndio kutakuwa na timeframe ya lini dunia itateketezwa pamoja na wote wasiomcha Mungu.
 
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli

Swali la kipumbavu. Kwa nini hawapandi punda na farasi kama alivyofanya yesu na motume. Umeulizwa swali la kipumbavu sana.
 
Inaonekana umeishia kusoma title tu, mkuu. Soma content ndio utajua kwanini nimeuliza swali hilo.
By the way, nenda kule kwa Wamasai, utaona Wakristo wapanda punda wengi tu.
 
Hakuna timeframe. Yesu anasema tukeshe kwakuwa hatuijui siku atakayokuja. Anaweza kuja hata usiku huu. Kuanzia siku atakayokuja ndio kutakuwa na timeframe ya lini dunia itateketezwa pamoja na wote wasiomcha Mungu.
sasa kama hakuna timeframe --- kwanini unasema "dunia hii inaelekea mwisho"
 
Kwa sababu Yesu alizitaja dalili za kuja kwake na za mwisho wa dunia. Soma Biblia utagundua kuwa dalili hizo almost zote zimeishatimia. Ndio sababu nilikuambia anaweza kuja hata usiku huu.
 
mi nataka uweke timeframe tu vizazi vijavyo vifanye reference
 
Inaonekana umeishia kusoma title tu, mkuu. Soma content ndio utajua kwanini nimeuliza swali hilo.
By the way, nenda kule kwa Wamasai, utaona Wakristo wapanda punda wengi tu.

Umeandika upuuzi tu. Mi nikiona title ya kipuuzi basi nachoka
 
mi nataka uweke timeframe tu vizazi vijavyo vifanye reference
Waswahili wanasema dalili ya moto ni moshi. Ukiona nyumba yako inafuka moshi utasubiri uambiwe timeframe ya nyumba yako kuanza kuungua, au uta-take action saa hiyohiyo kutafuta vizima moto.

Mungu kwa mapenzi yake mwenyewe hajataja timeframe, ila hakutuacha gizani, alitutajia ishara na dalili za kuja kwake, kisha akasema tuonapo mambo hayo yameanza kutimia, tuinue vichwa vyetu kwakuwa ukombozi wetu umekaribia.

Kwahiyo ndugu yangu, kama hujatubu na kumwamini Yesu, fanya hivyo sasa. Ukisubiri timeframe hutaipata na utaachwa, kwa sababu Yesu atakuja ghafla kama mwizi ajavyo usiku. Siku atakayokuja atawanyakua wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini. Soma mada hizi upate timeline(sio timeframe) au undani wa yale yatakayotokea soon:
 
Umeandika upuuzi tu. Mi nikiona title ya kipuuzi basi nachoka
Kuna aina nyingi za uandishi wa mada/titles. Kuna nyakati mwandishi anaweza kuchagua title isiyohusiana kabisa na content kwa lengo maalum. Hivyo kama wewe huwa unaishia kusoma tu title, utakuwa umepitwa na mengi sana ya maana.
 
timeframe unayo ? / huna?
 
timeframe unayo ? / huna?
Inaonekana kama tunaongea lugha tofauti. Mbona nimeeleza kwa undani sana kwamba hakuna timeframe; kuna dalili tu. Na dalili hizo almost zote zimetimia. In other words, muda umeisha.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
Sasa mbona Yesu amelitangaza hivi
Luka 15:22 (Biblia Habari Njema)
"Baba akawaambia watumishi wake, 'Lileteni vazi jema, mlivishe, mweke pete mkononi mwake na viatu miguuni mwake.'"

hapo inaonyesha kuwa kanzu ni vazi la heshima, pia kama ni ishara ya kirejesho cha hadhi na heshima mbele ya familia au jamii na Yesu amesema
katika Mathayo 11:29-30 (Biblia Habari Njema)

29) Jitieni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha kwa roho zenu.
30) Kwa maana nira yangu ni laini, na mizigo yangu ni mwepesi."
 
Asante sana kwa maoni yako. Hapo naona umechanganya masomo mawili tofauti. Habari ya kwanza inamhusu mwana mpotevu. Kumbuka jinsi huyo alivyotapanya mali kiasi cha kutokuwa hata na pesa ya kununua chakula. Aliporudi nyumbani, baba yake alionyesha kuwa bado anamthamini tu ndio sababu akaamuru apewe vazi jipya. Na sisi tukiokoka, tunauvua utu wa kale na kuvaa utu mpya (sawa na vazi jipya).

Habari ya pili inatuambia tujifunze kuwa na unyenyekevu wa moyo kama Yesu. Sio kwa kuvaa kanzu nyeupe. Mafarisayo walikuwa wanavaa kanzu lakini Yesu aliwakemea mara nyingi kwa sababu walikuwa wasafi tu kwa nje lakini mioyo yao ilikuwa michafu.
 
Kwa hiyo vazi halina mchango wowote mbele ya Mungu basi hiyo Imani itakuwa haina matendo sasa
 
Tunapaswa kuvaa mavazi ili kujisitiri mwili tu. Mavazi meupe hayana mchango wowote katika kuondoa dhambi ya mtu.
 
Kwahiyo ukijistiri hupati chochote kwa Mungu naona muda umeenda pumzisha mwili
Kwaheri Mungu akipenda 👋🏽👋🏽👋🏽
 
Kuna aina nyingi za uandishi wa mada/titles. Kuna nyakati mwandishi anaweza kuchagua title isiyohusiana kabisa na content kwa lengo maalum. Hivyo kama wewe huwa unaishia kusoma tu title, utakuwa umepitwa na mengi sana ya maana.
Mwandishi mbovu hufukuza msomaji kuanzia kwenye title. Na mzuri hubuni title ya kuvutia kusoma hbr
 
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli

Ogopa sana watu wanaofanya wema au jambo kwa shinikizo.

Mtu anavaa hijabu lakni anaingiliwa kinyume na maumbile .
Mtu anavaa kanju lakni analawiti.
Mtu hali nguruwe lakni ni mchawi na anatesa watu kwa kuwarushia majini.

Mtu hasikilizi nyimbo za kwaya eti ni dhambi lakni anasikiliza miziki ya kina Zuchu na Diamond .
Wakiambiwa kuna nyimbo za injili uwanja wa taifa hata bure hawaingii lakini Diamond wanamlipa elfu 20 kiingilio.

Walimu wao ni vipofu kama wao
 
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.

Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)

Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)

“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)

Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)

Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli

View: https://www.tiktok.com/@wakeupblaq/video/7383159964912618757?is_from_webapp=1&sender_device=pc
 
Kwani Yesu alisemaje kuhusu hilo?
 
Back
Top Bottom