Yohana 4:23Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
Kwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?
Yesu aliishi katika jamii ya Wayahudi iliyokuwa na mila na desturi za mavazi. Katika mazingira hayo, kuvaa mavazi meupe ya aina ya kanzu ilionekana kuwa ni ishara ya usafi, utakatifu, heshima na ibada.
Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila kilichofanywa na Yesu kama sehemu ya utamaduni wa Wayahudi ni lazima kifuatwe kama agizo la kiroho kwa Wakristo wote duniani.
Katika mafundisho yake, Yesu hakusema kwamba ni lazima kuvaa kanzu au mavazi meupe wakati wa kusali. Badala yake, alionya dhidi ya unafiki wa kujionyesha kwa mavazi ya dini, huku moyo ukiwa mbali na Mungu; ndiyo sababu alionya akisema:
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu.” (Luka 20:46)
Agano Jipya linaweka mkazo kwenye mavazi ya kiroho. Ndio sababu Wakristo wanaitwa kumvaa Kristo na kuvaa utu mpya, yaani tabia takatifu badala ya kuwekeza nguvu katika mavazi ya nje kama njia ya kujisogeza kwa Mungu:
“Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)
“Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.” (Wakolosai 3:12)
“Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.” (1 Petro 3:3-4)
Hivyo basi, vazi la kanzu nyeupe halina uzito wa kiroho kwa Wakristo wa Agano Jipya. Kile kinachomfanya mtu akubalike mbele za Mungu ni moyo wake, sio vazi lake.
"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu." (Mathayo 5:8)
Kwahiyo ndugu yangu, uwe huru kuvaa vazi lolote kanisani, mradi tu liwe la kusitiri mwili na lisilete kikwazo kwa wengine katika ibada au maisha ya kiroho. Hivyo basi ukipenda kuvaa suti kama ya Rais Trump, ruksa. Ukipenda kuvaa kanzu ya bluu, ni sawa kabisa. Hakikisha tu saa ya kuabudu, umwabudu Mungu katika roho na kweli
Kanzu si vazi la ki=dini, ni fashion ya mavazi kwa mashariki ya kati na uarabuniKwanini Wakristo hawavai kanzu nyeupe saa ya kusali kama Yesu alivyofanya?

Hiyo picha ya profile ni yako?Labda tuwaombe wenyewe watuambie
Wazungu ndo wenyeweustable marriages na kutinduana mitaro
Chonde chonde usiitamani hiyo picha bana. Hujasoma huu uzi?Hiyo picha ya profile ni yako?
Wewe una shida gani?Chonde chonde usiitamani hiyo picha bana. Hujasoma huu uzi?
Ukimtazama mwanamke kwa kumtamani, tayari umefanya naye uzinzi moyoni. Jifunze hapa jinsi ya kushinda tamaa hiyo
Ukimtazama mwanamke kwa kumtamani, tayari umefanya naye uzinzi moyoni. Yesu Kristo alitoa onyo hilo zito kuhusu dhambi ya uzinzi usioonekana kwa macho ya kawaida lakini unaotekelezwa ndani ya moyo wa mtu. Katika Mathayo 5:28 anasema hivi: "Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa...www.jamiiforums.com
Mwisho wa wapi mkuu?Nimekutahadharisha tu, mkuu maana dunia hii inaelekea mwisho.
weka time frame vizazi vijavyo vifanye referenceMwisho wake. Huna habari kwamba dunia hii itakunjwa kama karatasi na kuchomwa moto? Soma Ufu 6:14 na 2 Petro 3:10–12