Kwanini Wakristo na Waislamu wa zamani walichukulia utumwa kama jambo la kawaida ni sio uovu?

Kwanini Wakristo na Waislamu wa zamani walichukulia utumwa kama jambo la kawaida ni sio uovu?

Ulaji nyama ni sehemu ya evolution ya binadamu, ulaji nyama kwa kiwango kikubwa ulileta mabadiliko makubwa katika ubongo na mwili mzima wa binadamu ulipelekea mabadiliko makubwa zaidi, kula nyama kwa binadamu ni moro of necessity than just a choice, tafiti mbalimbali zinaonyesha watoto vegan au watu vegan hukabiliwa na changamoto mbalimbali za afya zitokanazo na ukosefu wa virutubisho.
Wewe unavyotetea ulaji nyama ndivyo hivyo hivyo watu walivyotetea utumwa, wakapigana mpaka vita kuutetea.

Lakini miaka ilivyoenda, moral consciousness ya dunia imeongezeka mpaka leo unawashangaa kwa nini walitetea utumwa.

Huwezi kuelewa somo la ubaya wa kula nyama leo kwa sababu muda wa kuelewa somo hilo kwa watu wengi haujafika bado.

Wajukuu wa wajukuu wako watakushangaa ulivyokula nyama leo kama wewe unavyowashangaa watu waliotetea utumwa.
 
Ila sio Africa yote,,mfano Ethiopia na misri ukristo uliingia kabla hata ya wazungu kuja Africa
Ethiopia na Misri waliupata Ukristo wapi kama sio kupitia maingiliano na Roman Empire??
 
Mungu anaweza akaruhusu upate majaribu au chamgamoto kama hizo lakini akaja kukutoa baadae na kukuinua zaidi akakurudishia zaifi mara dufu kama utakuwa na imani thabiti kwake,kama utakuwa mnyenyekevu,utaendelea kumuomba.
Sababu za kuruhusu watu wake wapitie magumu /majaribu changamoto mbalimbali ikiwemo utumwa,magonjwa n.k
zipo nyingi ila hiyo ya kutenda dhambi ni moja wapo.
Mfano YUSUFU /JOSEPH aliuzwa utumwani Misri lakini hakumuasi Mungu na pindi anauzwa hakuwa amemuasi Mungu alikuwa na imani kwa Mungu na mtumwa mnyenyekevu na mwaminifu.Mungu alikuja kumfanya waziri mkuu wa misri.
Mungu aliruhusu ndugu zake wamuuze utumwani lakini hakumuacha,sasa kwq sababu utumwa ulikuwa na utamaduni wa watu wa zamani,ile kuwa humble ilimfanya apendwe na slave masters wake hata gerezeni alipewa unyampala sasa asingekuwa mtumwa mtiifu ,asingeoata favour na Mungu anatuagiza tuwe humble watu wote wakati wote.tumtumaini Mungu atatuokoa katika hali zote hata utumwani waisraeli waliomba Mungu akasikia kilio cha waizraeli akamtuma Musa aende kwa FARAO wa misri ili awatoe watu wake .
Japo pia kumuasi Mungu kuna maana hata upagani ukishakuwa mpagani wale watu watu wanao abudu miungu ni wamemuasi Mungu,na makosa hayo wanaweza wakaadhibiwq hata kizazi chao cha nne.
Mana kuabudu miungu ni laana inayoweza kuathiri hata vizazi vyako vijavyo.
Acheni Sababu za kitoto...so waafrica tutainuliwa lini
 
Utumwa ungalipo sema kwa sasa hatuchapwi viboko adharani
 
Wewe unavyotetea ulaji nyama ndivyo hivyo hivyo watu walivyotetea utumwa, wakapigana mpaka vita kuutetea.

Lakini miaka ilivyoenda, moral consciousness ya dunia imeongezeka mpaka leo unawashangaa kwa nini walitetea utumwa.

Huwezi kuelewa somo la ubaya wa kula nyama leo kwa sababu muda wa kuelewa somo hilo kwa watu wengi haujafika bado.

Wajukuu wa wajukuu wako watakushangaa ulivyokula nyama leo kama wewe unavyowashangaa watu waliotetea utumwa.
Nimesoma kuhusu utumwa, sijaona watetezi wake wakihusianisha na evolution ya binadamu, utumwa ulikuwa ukihusianishwa na races, dini, social order na baadaye sana suala la mabadiliko ya uchumi.
 
Ethiopia na Misri waliupata Ukristo wapi kama sio kupitia maingiliano na Roman Empire??
Ukristo wa Ethiopia na Misri ulitoka direct mashariki ya kati,, kuna mitume walifika hadi Ethiopia, ndo maana wakoloni walivyofika walipata shida Ethiopia maana walishakua mbele kuliko nchi nyingine za Africa, hata ufalme wao mtawala alikua lazima awe mkristo fatilia Tewahedo catholic church Ethiopia utapata historia yake
 
Mashariki ya kati ilikuwa sehemu ya Roman Empire tangu Yesu anazaliwa.
 
Mashariki ya kati ilikuwa sehemu ya Roman Empire tangu Yesu anazaliwa.
Roman Empire imekuja kuukubali ukristo badae kabisa , na tayari kuna maeneo tayari kanisa lilishaanza kazi,,mitume walitawanyika kwenda kueneza injili na kuanzisha makanisa sehem mbali mbali kabla hata warumi hawajakumbatia ukristo
 
Nimesoma kuhusu utumwa, sijaona watetezi wake wakihusianisha na evolution ya binadamu, utumwa ulikuwa ukihusianishwa na races, dini, social order na baadaye sana suala la mabadiliko ya uchumi.
Kwanza kabisa, sababu yoyote ya kutetea utumwa inafanya argument yangu kuwa valid.

Point ni kwamba, moral consciousness ya dunia wakati huo ilikuwa haijafika juu kiasi cha kupinga utumwa categorically, kwa sababu yoyote.

Hilo linatosha kusimamisha point yangu.

Lakini pia, ukiongelea evolution ya binadamu hapo hapo ndipo habari nyingine za races zimetokea, kuna watu wengi wametetea utumwa kwa kusema watu weusi si watu kamili, ni kama manyani fulani bado hawaja evolve kuwa watu kamili, sasa utasemaje utumwa ulikuwa based on races na si evolution?

Huelewi wapi?
 
Usisahau pia kutaja andiko linalosema, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Mathayo 7:12 Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Ukristu haukuutuza utumwa, bali ulikuwa ukiwaongoza Wakristu waliokuwa wakiishi katika tajamani za kitumwa (civilization of slavery), kwenda katika njia bora zaidi ya hapo.

Ndiyo maana Paulo Mtume anasema pamoja na kwamba zamani Mungu aliruhusu mambo haya, sasa anawaagiza watu wote waufuate mwenendo bora (Matendo 17:20).
Wale watumwa waliokuwa wakikamatwa na kusafirishwa kwa meli kwenda America Kaskazini na Kusini walikuwa wanafanyiwa civilization??
 
Kwanza kabisa, sababu yoyote ya kutetea utumwa inafanya argument yangu kuwa valid.

Point ni kwamba, moral consciousness ya dunia wakati huo ilikuwa haijafika juu kiasi cha kupinga utumwa categorically, kwa sababu yoyote.

Hilo linatosha kusimamisha point yangu.

Lakini pia, ukiongelea evolution ya binadamu hapo hapo ndipo habari nyingine za races zimetokea, kuna watu wengi wametetea utumwa kwa kusema watu weusi si watu kamili, ni kama manyani fulani bado hawaja evolve kuwa watu kamili, sasa utasemaje utumwa ulikuwa based on races na si evolution?

Huelewi wapi?
Tunaweza kujadili utumwa kwa hoja ya evolution kwamba races za binadamu zinatofautiana katika evolution lakini katika uzi mwingine, huu uzi hapa ni mahususi kwa watu wa kidini kutaka kuelewa perspective ya dini hasa za Abrahamic katika utumwa.
 
Kwa nini unalazimisha uzi huu uwe wa kidini wakati kiuhalisia kuna watu waliamini utumwa kuwa sahihi kwa sababu Waafrika ni kama manyani na hawaja evolve kufikia kuwa watu?

Kwa nini unataka ku ignore ukweli na kulazimisha upande fulani tu?

Huelewi kuwa kuegemea upande wa dini ni moja ya sababu watu waliukubali utumwa, waliona vitabu vya dini vimeukubali utumwa na hivyo utumwa ni kitu cha kawaida, wakasema "hata kwenye vitabu vya dini utumwa upo, na Mungu kasema watumwa wawe watiifu kwa mabwana wao". Baadaye walivyokuja kuelimika wakaona hizi ni imani za kijinga, utumwa haufai?

Zaidi, sababu yoyote ile ambayo imewafanya watu watetee utumwa huko nyuma ni sababu ambayo inaonesha the moral consciousness of the world at that point haikuwa kubwa kiasi cha kuwafanya watu waukatae utumwa.

Kwa hivyo, hapo kama watu waliukubali utumwa kidini au kwa evolution si muhimu, kitu muhimu ni kwamba waliukubali utumwa.

Mbona unataka kufanya a non issue (kwa nini waliukubali utumwa) iwe issue wakati sababu yoyote iliyowafanya waukubali utumwa maana yake ni kuwa the moral consciousness of the world ilikuwa haijafikia kevel ya kuukataa utumwa?

Mbona kama una fail ku argue logically na unataka kufanya non issues ziwe issues?
 
Achana na Waisraeli,
Zungumzia Waafrika, Wazungu, Waarabu, Wahindi n.k ambao hawakuwa "watu wake"
TUKISEMA UKWELI BILA UPENDELEO.
Tukizungumzia historia ya utumwa Afrika na dini tutakubaliana.
DINI ilitumiwa na mabeberu/mabepari kututawala waafrika na kutuingiza utumwani .
Wale wamissionaries waliotumwa na kufadhiliwa na nchi zao za kikoloni waliotuletea dini Afrika wamissionaries walikuwa ni vitangulizi vya ukoloni kama wapelelezi badhi yao sio wote,na walitumia dini kutu BRAIN WASH ili kututawala kutuingiza utumwani kwa maslahi yao.
Hawakufuata mafundisho ya dini waliyoihubiri kuhusu upendo,kupendana,binadamu wote ni sawa tumeumbwa na Mungu kwa mfano wake tupendane tusibaguane tuheshimiane utu wetu.
Na hata baadae sababu ya kukomesha biashara ya utumwa ni baada ya mapinduzi ya viwanda huko kwao na kuona sasa wanatumia mashine hawahitaji tena watumwa nguvu kazi za watumwa.
Ndio wakajifanya ni humanitarian sababu haki za binadamu kiunafiki ila si kutoka moyoni wala si wanachomaanisha.(WALIKUWA KIMASLAHI YAO UBINAFSI/UBEPARI)
Japo dini waliyotuletea ni sahihi mafundisho sahihi ya Mungu
,ila waliotuletea waliyatumia kwa manufaa yao ni kama sasa manabii wa uongo wanaotumia dini kuuza mafuta ya upako na mchanga wa upako na kupiga hela za sadaka na michango ya waumini wo.
 
Kwa nini unalazimisha uzi huu uwe wa kidini

Zaidi, sababu yoyote ile ambayo imewafanya watu watetee utumwa huko nyuma ni sababu ambayo inaonesha the moral consciousness of the world at that point haikuwa kubwa kiasi cha kuwafanya watu waukatae utumwa.
Mora consciousness ni sababu mojawapo tu, utumwa ulisababishwa na mambo mengi na ulimalizwa kwa sababu mbalimbali mojawapo muhimu zaidi ikiwemo ya uchumi, huu uzi nimetaka kupata perspective ya kidini kuhusu utumwa kama mungu alichukulia ni uovu au jambo la kawaida kwa kipindi hicho.
 
Back
Top Bottom