Kwanini Wakristo sio wafanyabiashara wakubwa na matajiri?

Kwanini Wakristo sio wafanyabiashara wakubwa na matajiri?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kwenye orodha yamatajiri duniani, hata ukiona ana jina la Kikristo tajiri huyo atakuwa ni mpagani, asiyeamini Mungu, haendi kanisani na Wala sio msharika wa Kristo.

Pia unaweza kukuta ni Myahudi. Dini ya Mayahudi na Ukristo ni vitu viwili tofauti sana.

Ukikuta Mkristo ni tajiri mkubwa, anakuwa ametajirikia hukohukp kwenye dini na sio kwa kufanya biashara, mfano T. D. Jakes, Odeyempo, nk.

Kwa bongo tajiri Mkristo aliyekuwa mfanyabiashara ni Mengi peke yake.

Ukipenda kwa matajiri wote utakuta ni Waislam, Wahindu, Islailiya na dini nyingine.

Kitu Gani kinachosababisha Wakristo wasiwe matajiri wakubwa?

Ni wapi wanapokosea?
 
Akili mtu wangu akili.

Wakristo wameharibiwa akili..yaani wanachezewa akili kwa kuaminishwa vitu vya uongo. Mfano wanaamini kuwa kila kitu hupangwa na Mungu.

Pili wanaamini zaidi KATIKA miujiza.

3 Hata kile kidogo wanachopata wanaenda kukigawa kanisani kama sadaka, kikumi n.k
 
Usemacho ni kweli .Na Tofauti ya wakristo na hao wengine ambao si wakristo ni moja Tu Nayo ni hii;

Wakristo walio wengi Wana uchumi mzuri (kipato cha Kati na cha juu)...inclusive economy..Kwa lugha niyingine,sehemu yenye wakristo wengi wanaweza wasiwe matajiri Sana lkn pia wanakuwa Wana maisha mazuri ya kupata three basic needs,food, clothes and shelter bila shida

Hao wengine ambao siyo wakristo anaweza kujitokeza mmoja au hata kumi wakawa matajiri wa kutisha lkn the rest wakawa walala Hoi wa kutupwa(masikini mbwa)..Hiyo ndy tofauti
 
Akili mtu wangu akili.

Wakristo wameharibiwa akili..yaani wanachezewa akili kwa kuaminishwa vitu vya uongo. Mfano wanaamini kuwa kila kitu hupangwa na Mungu...
Mbona wewe ndio kama akili hazikutoshi halafu unawashangaa wakristo..

Mali hutaenda nazo popote, utaziacha hapa hapa duniani, ni kama mapambo tu.
 
Haja ya Wakristo wote ni kuuona Ufalme wa Mungu, sasa kama Biblia imetuambia ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko TAJIRI kuuona Ufalme wa Mungu, wewe unategemea nani anapenda kuwa "Tajiri"? that is not so necessary but the truth is:

Gap kati ya TAJIRI na Maskini ni kubwa zaidi kwa hizo dini nyingine ulizo mention ukilinganisha na Wakristo, kama huamini angalia hapa Tanzania, maeneo ambayo wakazi wake majority ni Wakristo nenda ukalinganishe na maeneo ambayo majority ni Waislam, nenda Lindi na Pwani vijijini uangalie maisha wanayoishi, halafu nenda ukalinganishe na maisha wanayoishi kule Bukoba, au Moshi au Mbeya utapata jibu kwamba ni bora kwenye population majority wakaishi maisha ya wastani, kuliko kuwa na Matajiri wakubwa top 10 halafu common wananchi wote majority wanaishi kwenye vibanda na nyumba za nyasi.

Hata hapo Dar es Salaam, fanya utafiti wakazi wengi wa Buguruni, Temeke na Mbagala, halafu nenda ukalinganishe na wakazi wa Tabata, Mbezi na Kimara utapata majibu yako!
 
Mbona wewe ndio kama akili hazikutoshi halafu unawashangaa wakristo..

Mali hutaenda nazo popote, utaziacha hapa hapa duniani, ni kama mapambo tu.

Pole sana mkuu. Endelea kuamini unachoamini
 
Matajiri wengi waliona shule zin gewapotezea muda,wakristo wengi wanaamini zaidi katika elimu kuliko biashara.wengi wameajiriwa katika sekta rasmi kutokana na vyeti vyao.

Huwezi kuwa bilionea kwa kuajiriwa
 
Kwenye orodha yamatajiri duniani, hata ukiona ana jina la Kikristo tajiri huyo atakuwa ni mpagani, asiyeamini Mungu, haendi kanisani na Wala sio msharika wa Kristo...
Kaka mkubwa with all due respect hawa matajiri makubwa ni mabinafsi na machoyo sana na ndio yaliyotajwa kwenye Bible kuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya tundu la sindano kuliko wao kuurithi ufalme wa Mungu
Haya matajari makubwa hayatengezi network ya wengi wapate hivyo hujikusanyia mpaka kile cha fukara wa mwisho.

Hawa wengine wasioingia kwenye network ya ukwasi wa dunia wana utajiri wa mtandao kuanzia familia, ndugu mpaka watu baki na ndio furaha yao kuona 'wote tunapata'!

JamiiForums mobile app
 
kwamba matajiri wakubwa ni waislam,wayahudi,wahindu na wabudha wakristo awamo!,kweli inafikirisha sana.
 
Back
Top Bottom