NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
hata Yesu alivyoomba alifumbua macho huku akiangalia juu mbinguni .. YOHANA 17:1
Usiku wa juzi nikiwa nikiwa kwenye maandalizi ya kulala, kama kawida yangu huwa ni lazima nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya, utimamu na amani aliyonipa. Kwa siku hio kabla ya kulala nikajiuliza swali kwanini huwa tunafumba machoo wakati runaomba? Binafsi imekuwa ni utamaduni kabisa ni lazima nifumbe macho nikiwa naomba kabla ya kulala, kabla ya kula, kuanza na kumaliza safari, n.k.
Nimefanya uchunguzi na kubaini kwamba hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia iliyotutaka tufunge macho bali tuelekeze imani yetu kwa muumba wetu pale tunapomuomba.
Nadhani kufunga macho iwe ni pale tu ambapo mtu yupo mazingira yanayomuondoa umakini akifungua macho na ikibidi azibe pia masikio endapo kuna makelele yanayomtoa umakini, lakini katika sehemu iliyo na utulivu hasa tunapoomba vyumbani usiku tulivu wakati wa kulala na kanisani mda wa kuomba ambao panakuwa kimya iwe hiari tu.
Hadi sasa naomba kwa kufungua macho na wala sijaona tatizo lolote, haya mambo ya kuomba kwa kufunga macho yawe ni uchaguzi tu wa mtu mfano kwa wale wanaoshindwa kuweka umakini wanapoomba hasa wakiwa sehemu ambazo hazina utulivu.