Kwanini walimu na wastaafu ndio wahanga wa Utapeli wa QNET, DECI, D9 nk?

Mie hapa wamenishawishi mpaka wameshindwa wameanza kunitukana. Yaani MTU anakuambia anapata mamilioni hata vaa yake inatia mashaka. Kiingilio laki 5 unatoa fedha yako halafu unaanza kuhangaika na madawa Yao.
 

Hahaaa...
Mimi kuna jamaa nafanya nae kazi ameshajiingiza tena eti kafungua account tatu kabisa, zaidi ya 1.5M imeondoka...!
Amenishawishi sana, nikamwambia nasubiri upepo kwako ununue kwanza hiyo prado unayoivutia kasi!
Yaani kila siku kazini anachomoka kwenda kuuza kahawa mtaani!
Kafanikiwa kumchomeka mmoja, sasa kila anayemgusa anamcheki anasema hiiiiiiiiiii....
 
yaani daah ni hatari atalete ushuhuda we subiria mkuu
 
Dah,nilipigwa deci 1,000,000. Na Serikali imetuchunia HD leo. Ndio maana sijui CCM wala Serikali huwaga siwaelewi kabisa
 
Ivi hawa Forever living na wao wanaingia ktk mfumo huo huo wa pyramid scheme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…