Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Mhe. Kinana anazungumza na waandishi wa habari Dodoma. Katika mambo aliyozungumza ni kudai tume itakuwa huru, kudai Rais ana nguvu kwenye kila tume ya uchaguzi Duniani na kudai Chadema wanamepewa uhuru siku chache na wanahubiri chuki.
Katika haya yote hakuna linaloonekana kuungwa mkono X na Instagram wala facebook. Kila mtandao uliopost habari zake wachangiaji wengi wamekosoa na kumshauri astaafu atuachie nchi yetu
Hoja yangu; je hakuna wanachama wa CCM wanaotumia mitandao ya kijamii? Je ukimya wao unamaanisha nini kwa chama chao?Kwanini wameimarika sana katika kuwapuuza viongozi wa chama chao?
Kwanini chama tawala kinakuwa na wanachama wengi wasioweza kutoka adharani na kukitetea? Siku hizi hata kuvaa t-shirt za chama imekuwa nongwa na aibu...wanachama wanavaa ukumbini wakitoka wanaweka kwenye mabegi!
CCM wanaoana hii ni hali ya kawaida?