Mawazo mazuri sana, japo tafakari hili:
Mwanafunzi anasoma masomo yote hadi kidato cha pili na kuruhusiwa kuchagua michepuo anapoingia Kidato cha tatu, hasa kutokana na ukomavu wa kifikra katika huo umri(wastani wa miaka14-16)
Nataka pia nikuaminishe kuwa huu umri umefanyiwa tafiti kwamba ni mda maalumu wa kijana kuweza kujua anapenda nini kwa maana ya kwamba anaweza kufanya nini -huku akishauriana na academic mentors wake
Huu umri ni rahisi kujua mtoto ni talented katika eneo lipi, na chini ya umri huo mtoto huwa anapenda kila kitu akidhani anaweza kufanya kila kitu. Kupenda profession haina uhusiano wa moja kwa moja kwamba unaweza kuisoma
Hoja hii itakuwa na nguvu kama zitakuwepo tafiti kuonyesha kwamba kutokana na ukuaji wa teknolojia ya upashanaji habari, ama mabadiliko ya ukomavu kiuelewa, mtoto akiwa primary std 7 anakuwa amekomaa vya kutosha kuweza kuchepua.