Kwanini wanalaumiwa Polisi na siyo Hamza?
Ningekuwa na uwezo ningeenda kufanya mazoezi na naamini ningezewa kupunguza 500 gram sema tatizo nahisi ukoo hautakubari
 
Ukizingatia polisi wetu ni milenda wanachati muda wote ndio maana Hamza kawachukulia bunduki2

Wapo bize wakiangalia ngono kwenye simu zao..Kuna siku moja nilishika simu ya mjeda mmoja kuingia browse history yake nilishangaa nilivokutana navo...kuingia you tube...mamaaaaaa balaa nzito...
 
Polisi wanajikuta Mungu watu sana wakikukuta wanakupiga wakati kisheria sio ruhusa hata kama umekosea maana mahakama ndo inahukumu, sometimes inaboa unaona kabisa hapa sitapata haki ndo watu kama kina Hamza wanatokea sasa kuwa liwalo na liwe halafu ni suala la mda tu watakuja wengi watu wamechoka nchi ngumu halafu mtu anakuletea uduanzi fyeka tu shwaiin.
 
Nafikiri ni uonevu wa polisi wetu kwetu sisi wananchi... Mwenyewe walinipora sh 390,000. Sikuona kosa langu,hata leo sijui kwa nini walichukua hizo hela... Lakini nina amani,maana Mungu ameshanilipia.... Hela yangu imerudi,na mengine..
 
Katika pitapita zangu mitaani nimeshtushwa sana na wananchi badala ya kuhuzunika kwa gaidi kuuwa polisi wetu na badala yake wamegeuka wanawalaumu pili kwa matendo yao ya kubambikizia kesi,dhuluma,uonevu,kuchochea chuki,kuuawa raia wawapo mahabusu nk. Hii inaashiria kiti gani mbona si kawaida?

Napata mshituko mkubwa sana kuona rais wamekosa uzalendo wa kuliamini jeshi lao kiasi hiki. Polisi katika hili wajitafakari sana hii siyo kawaida, sasa watafanyaje kazi ikiwa raia hawatawapa Tena ushirikiano?

Lipo tatizo nadhani, hili jeshi linahitaji Reformation tena ya kikatiba kabisa. Recruitment ya polisi iwe ya hali ya juu sana, jeshi kulaumiwa kiasi hiki si kawaida.
Mojawapo ya sababu lukuki za kuchukiwa jeshu hili ni kuwa mkono wa kulia wa CCM (kutumika kutesa wapinzani)..
 
Katika pitapita zangu mitaani nimeshtushwa sana na wananchi badala ya kuhuzunika kwa gaidi kuuwa polisi wetu na badala yake wamegeuka wanawalaumu pili kwa matendo yao ya kubambikizia kesi,dhuluma,uonevu,kuchochea chuki,kuuawa raia wawapo mahabusu nk. Hii inaashiria kiti gani mbona si kawaida?

Napata mshituko mkubwa sana kuona rais wamekosa uzalendo wa kuliamini jeshi lao kiasi hiki. Polisi katika hili wajitafakari sana hii siyo kawaida, sasa watafanyaje kazi ikiwa raia hawatawapa Tena ushirikiano?

Lipo tatizo nadhani, hili jeshi linahitaji Reformation tena ya kikatiba kabisa. Recruitment ya polisi iwe ya hali ya juu sana, jeshi kulaumiwa kiasi hiki si kawaida.
Hii ni kuonesha kwamba raia hawana imani na vyombo vya dola, si polisi, jeshi hata mahakama zetu ni dhuluma tu. Na vyote hivyo vinaendeshwa kisiasa tu. Kwa vile serikali iliyopo inategemea vyombo vya dola kuilinda, na serikali inalinda uhalifu wao.
 
Wakipatikana akina Hamza kumi polisi watahesihu katiba na raia.
Kwa jinsi somo alilotoa HAMZA kwa polisi lilivyopokelewa na raia wema wanaodhulumiwa na polisi kila uchao, tutarajia akina HAMZA wengine kujitokeza. Serikali inatakiwa kuliangalia jambo hili kwa umakini mkubwa. Wakiipendelea polisi kwa sababu inawaweka madarakani, watavuna walichopanda.

Naamini maafisa usalama wana MONITOR maoni ya raia mitandaoni, ili kuishauri vema serikali ya CCM. Kilangila.
 
Zaid ya yote waliogopa angeweza akawa anapiga kelele mahakamani kuwa polisi walimdhulumu madini yake Siri ikafichuka...ndo maana wakaamua wamalizane naye mazima
Tatizo theory hii inakosa logic. Naamini kuna kikosi maalum ndio kilienda baada ya tukio kuanza na wao kupewa taarifa. Sasa ukisema walimmaliza asitoe siri basi inamaana huko polisi kila mtu alikuwa anajua kuwa kuna polisi wamemdhulumu Hamza?! Hilo linaingia akilini?!
 
Mkuu hakukuwa na kikosi maalumu pale...hakuna kikosi maalumu kinaweza kuwa kinarusha risasi Kama wehu...wale polisi walikuwa very disorganized kwenye ile operation...hakukuwa na mwasiliano Kati yao...yaani ni Kama waliamka usingizini tu..wangekuwa wanajua wanachokifanya wala ile operation isingechukua zaidi ya dakika 10 Hamza angewekwa chini ya ulinzi akiwa hai..
 
Tatizo theory hii inakosa logic. Naamini kuna kikosi maalum ndio kilienda baada ya tukio kuanza na wao kupewa taarifa. Sasa ukisema walimmaliza asitoe siri basi inamaana huko polisi kila mtu alikuwa anajua kuwa kuna polisi wamemdhulumu Hamza?! Hilo linaingia akilini?!

Inasemekana mkuu wa operation Kanda maalumu alihusika kwenye hyo dhuluma....sasa inawezekana pia kuwa alitoa maagizo kuwa Hamza asipatikane akiwa hai...
 
Umekosea sana kuandika kuwa '.....raia wamekosa uzalendo wa kuliamini jeshi lao'
Hilo siyo jeshi la raia, hilo ni jeshi la ccm na watawala wake.
Hivi mkuu, hata kama huna macho umekosa hata masikio ya kusikia matendo ya hawa polisi?!
 
Inasemekana mkuu wa operation Kanda maalumu alihusika kwenye hyo dhuluma....sasa inawezekana pia kuwa alitoa maagizo kuwa Hamza asipatikane akiwa hai...
Sijui hapa kwetu, wenzetu wanakitu inaitwa “ Rules of engagement “
Ukishawarushia risasi Polisi, basi hiyo safari inaenda kuishia kwenye kifo, labda kuwe na “clear surrender”.
Sasa kwa kesi hii, jamaa sio tu alishoot bali aliwaua na bado alikuwa anaendelea ku-shoot.
Unamkamataje?!
 
Back
Top Bottom