Yuko wapi Halid Chokoraa? Wapi Diouf,wapi Charles Baba?
Namkumbuka mpiga kinanda wa T.O.T Band Kadie Katanga,ilikua hatari sana. Sijui bado yuko hai au vipi lakini jamaa alikua mkali sana.
Itoshe tu kusema mara baada ya muziki wa dansi ule wa Bendi kama Vijana,Washirika,Bimalee,Tancut Almas,Maquiz, OSS, nk kufa katika soko la muziki wa Dansi zilibaki bendi mbili yaani Msondo na Sikinde. Lakini Bendi za kizazi kipya zikachukua nafasi na walifanya kazi kubwa mno,hiyo ni miaka ya 1999 hadi angalau mwaka 2007. Wanamuziki wafuatao wametoa mchango mkubwa sana katika bendi hizo. Nao ni Banza Stone(R.I.P), Ally Choki,Muumini Mwinyijuma,Roggart Hega,Amina Ngaluma(R.I.P),Hamis Amigolas(R.I.P), Hadija Mnoga, Charles Baba,Nyosh el Saadat,Harid Chokoraa,Bashiru Uhad,Badi Bakule,Luiza Nyoni/Mbutu, Jesca Charles,Msafiri Diouf,Rashid Mwezingo,Pauline Zongo kutaja wachache.
Bendi hizo ni Twanga Pepeta(African Stars), Tam Tam,Muungano Band,FM Academia,T.O.T Band, Akudo Impact,Bambino Sound kutaja chache.
Kwa sasa hata hizo bendi zilizokuja kuchukua nafasi ya Bendi kongwe kama vijana Jazz nazo ndo zinakufa,tatizo sijui ni nini! Twanga wako kimya,T.O.T kimya,FM Academia nao ni kama kimya.
Sent using
Jamii Forums mobile app