Miguel255
Member
- May 13, 2020
- 35
- 115
Msiba wa binadamu ni jambo la kuhuzunisha na kusikitisha hata kama aliefariki humjui. Kwanini? Kwasababu binadamu tofauti na viumbe wengine tumepewa upeo wa kuona uzito wa kuondokewa na binadamu mwenzetu, imefikia hatua hata baadhi ya watu wakiona msiba unapita karibu yao basi husimama hii ni ishara ya kuheshimu kitu kile.
Unajua hata jeshini, akifariki mwanajeshi mwenye cheo kidogo zaidi mfano Private basi atapigiwa saluti na wanajeshi wote waliohudhuria msiba huo hata mameja na makanali.
Hii yote ni akili tuliyopewa na M/Mungu ya kutambua kwamba msiba si jambo la kulichukulia poa. Inatupasa tuhuzunike, tuomboleze na kuyaenzi yale yote mazuri aliyoyafanya marehemu wakati wa uhai wake.
Sasa cha kushangaza hivi karibuni, taifa la Tanzania kumeibuka na hali fulani hivi fikirishi. Kumezuka tabia ya watu wengi kufurahia na kusherehekea vifo vya watawala wao au viongozi wao. Kwa mtazamo wa juu juu, hali hii inaweza kuonekana kama wananchi wamekuwa makatili au wamekosa utu. Hata hivyo, ukichunguza kwa kina, furaha hiyo mara nyingi kama si mara zote huwa ni kielelezo cha maumivu na mateso yalisobabisha hasira iliyokusanywa muda mrefu dhidi ya viongozi wao
Imefikia hatua hata post ya msiba kwenye kurusa rasmi ya serikali inafungiwa sehemu ya kutoa maoni (comment) kwanini?
Sababu zinaweza kuwa nyingi ila moja wapo ni kutowapa nafasi raia kutoa maoni yao na maoni yanayozuiwa hapa ni yale ya kufurahishwa na tukio hilo.
Hili swala si la kulichukulia poa, kwa ushauri wangu serikali na watawala wote wanapaswa kuangalia namna ya kutibu hili tatizo. Chuki kati ya wananchi na viongozi imezidi kuwa kubwa. Watu hawana imani tena na wale wanaowaongoza.
Hii ikizidi unajua nini kitatokea? Tutaanza kuishi kama wanyama, simba akimla swala, nyani huendelea na mishe zake kama hakuna kinachotokea
Kipindi nasoma sekondari siku moja kiongozi mmoja hivi alikuwa mchomaji vibaya mno hio siku aliumwa alafu ilikuwa usiku. Aise jamaa alipiga sana kelele lakini hakuna alieamka kumsaidia hata alielala juu yake (double decker) hakuamka.
Alikuja kusaidiwa na mlinzi na viongozi wenzake baada ya kuamshwa na mlinzi. Ila people zengine ziliuchuna na sio kwamba walikuwa wamelalala hapana.
Sasa hii jamii ndo inayoenda kutengenezwa kitaifa. Yaani itafika hatua nyumba ya mbunge inawaka moto alafu hakuna mtu ataeshughulika kuuzima. Watu wataendelea na mambo yao kama hakuna kilichotokea.
Kitaifa hili ni janga na linapaswa kutokomezwa. Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa kina sana. Katika pitapita zangu mtandaoni group moja hivi la waendesha pikipiki mmoja wao alisema kuna siku alipata request alipomkaribia mteja aligundua ni polisi baada ya kumuona na gwanda, jamaa alicancel na akasepa zake polisi baada ya kuona trip canceled kumpigia jamaa akasema sipakii polisi mimi.
Pengine bora nchi ikose mvua lakini sio utu. Hili tatizo linazidi kuota mizizi na lisipotibiwa mapema tutakuja kustuka kumeshakucha.
Rai yangu kwa viongozi, kufungia comments si tiba ya hili tatizo. Watanzania sio wakatili na ni watu wenye utu sana, viongozi wanapswa kujua hizi chuki walizonazo majority zinasababishwa na nini?
Wasiseme kwamba watu wamepandikizwa chuki na wanaharakati wa kulipwa. Watanzania wana akili zao timamu kama hakuna sababu ya kuchukia uongozi wasingechukia ila wameichukia kwasababu fulani fulani.
Sasa hizo sababu ziwekwe wazi zisifichwe na zitibiwe.
Nawasilisha