Kwanini wananchi wakihojiwa kwenye vyombo vya habari, kero zao wanaziwasilisha kwa rais na sio kwa viongozi wa mkoa au wilaya?

Bruno Jewel

New Member
Joined
Sep 28, 2023
Posts
4
Reaction score
2
Kumekuwa na tabia inayoendelea kushika kasi kwenye nchi yetu ya wananchi kutaka au kuwasilisha kero zao na matatizo yao moja kwa moja kwa rais, wakati huo viongozi wa mikoa na wilaya wapo na wameaminiwa na rais kumuwakilisha.

Swala hili limeshika kasi sana katika nchi yetu ya Tanzania. Swali ni; je viongozi wa mikoa na wilaya mbali mbali wamefeli kutekeleza kazi zao au hawawatendei haki wananchi? Je, hili swala linaonyesha taswira gani kwa nchi kwa ujumla?
 
Kila kitu ni mama wengine wote mazombi tu. Hii tabia alianzisha jiwe ila maza nae anaendelea nayo. Wanapenda sifa za kijinga
 
Kumekuwa na tabia inayoendelea kushika kasi kwenye nchi yetu ya wananchi kutaka au kuwasilisha kero zao na matatizo yao moja kwa moja kwa rais, wakati huo viongozi wa mikoa na wilaya wapo na wameaminiwa na rais kumuwakilisha.

Swala hili limeshika kasi sana katika nchi yetu ya Tanzania. Swali ni; je viongozi wa mikoa na wilaya mbali mbali wamefeli kutekeleza kazi zao au hawawatendei haki wananchi? Je, hili swala linaonyesha taswira gani kwa nchi kwa ujumla?
Kwa vile wanasikia viongozi wao kila mmoja anatamka kuwa kila kitu kimefanywa na Rais, na pesa imetolewa na Rais etc. Kwa maana hiyo, matatizo yao yanatatuliwa na Rais. Lazima wakiwa na tatizo wanalielekeza kwake.
 
Swala hili limeshika kasi sana katika nchi yetu ya Tanzania. Swali ni; je viongozi wa mikoa na wilaya mbali mbali wamefeli kutekeleza kazi zao au hawawatendei haki wananchi? Je, hili swala linaonyesha taswira gani kwa nchi kwa ujumla?

Hao viongozi wadogo wenyewe kila wakupanda majukwaani, wanamsifia Rais mwanzo mwisho kuwa ndiye mtatuzi wa kero kadha wa kadha...

Hivyo wananchi washajua ya kwamba viongozi wadogo wadogo hawa ni kanyaboya tu...
 
Back
Top Bottom