Kwanini wananchi wengi wanadai Masoko yanayoungua hayaungui kwa bahati mbaya bali yanachomwa?

Shida ni pale masoko hasa ya wamachinga kuungua kipindi hiki cha Mama
 
Kwenye kuwarejesha ndo tutahakiki lilichomwa au liliungua ni kama kuna kakikundi kamegundua vibiashara vya kisupamarket kinatamani maeneo yaliyochangamka tayari au kinataka kuwalazimisha wananchi wazoee biashara zao waende kwao. Wanatafuta uti wa mgongo wa kujiegemeza
 
[emoji38][emoji38]
 
Huu moto ni ajali za kawaida.

Hakuna ambaye anakusudia kuchoma moto haya masoko ili yaungue watu wapate hasara.

Ndio maana hakuna ripoti yoyote iliyotolewa mpaka hivi leo kuhusiana na vyanzo mbalimbali vya moto kwa sababu jakuna mchawi zaidi y ajali za kawaida tu.

Wanaoamini k2amba moto umetokana na mbinu za watu hao ndio watupe full information.
 
Basi kama hawawezi kuziweka hadharani, hakuna maana ya kutangaza uchunguzi hadharani.
kwahiyo unategemea ipo siku utapata taarifa flani bila kuzifuatilia? nyingine lazima uzifuatilie binafsi
 
Kuna report ya moto umewahi ona? Itakuwa muujiza tukipewa. Wanajua Watanzania ni wa kusahau.
mkuu swala likishapoa hakuna mtu atasimama jukwaani kuja kukweleza kua ilikuwa hivi ilikuwa vile ila report ukiihitaji utaipata mbona wengi huzipata tuu. pia si rahisi zisomwe kwenye vyombo vya habari maana hata hivyo mbombo vya habari kwao inakuwa ssi habari yenyemvuto kwa wengi.
 
ngoja tuone kamati inakuja na nini, tuliofuatilia vyombo mbali mbali vya habari nadhani tutakuwa na kitu hasa tukikumbuka ushuhuda wa mhanga mmoja ambaye yeye alisema yu tayari kuwa shahidi na aliona tukio zima
Kama ulimboka hakuwahi sema chochote baada ya kupona tusitegemee chochote kwa mashuhuda wa hili.
 
we ukitaka kujua kuwa sio bahati mbaya baada ya soko kuungua waliounguliwa na vitu wakitaka kurudi kujenga upya vibanda vyao, wanakatazwa jiulizwe kwanini wakatwaze huku sababu ikiwa eti uchunguzi haujakamilika baada ya mda anapewa mkandarasi linajengwa jengo lingine tofauti na lilikuwepo mwanzo
 
Aiseee
 
Unaweza kutoa mfano mmoja tu sehemu iliyo UNGUA kili jengwa kitu tofauti na kilicho kuwapo awali hasa kwenye masoko au sehemu yoyote ya JUMIIYA ilitujue na sisi.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…