Kwanini wanapoteuliwa na kutumbuliwa ni wale wale? Hakuna watanzania wengine wenye sifa na maono?

Kama mtu hapafomu sehemu inabidi atolewe kwenye mfumo sio kuhamishwa post.
Serikalini hawana kipimo cha "performance", serikalini "performance" yako inapimwa na mashushushu walio kuzunguka. Kikulacho ki nguoni mwako.

Fitina, majungu, kurogana, kukandiana, unafik, kuchekeana na kupongezana kiuongo uongo ndivyo vilivyojaa kila idara ya serikali. Kila uchawi na mabaya unayoyajuwa na usiyoyajuwa wewe yapo huko.
 
Ndiyo maana inchi imejaa mariasili lakini wananchi wake choka mbaya
 
Ndiyo maana inchi imejaa mariasili lakini wananchi wake choka mbaya
maliasili

Kuchoka kwako hakuhusiani na serikali, ni wewe unashindwa kuziona fursa.

Wezi wa serikalini wote wanatafuta watu wa kuwafanyia kazi na biashara zao nje ya serikali, halafu vijana kwa ujinga wao wanatafuta kazi serikalini badala ya kutafuta kazi kwa wezi wa serikalini. Hao kazi zao ni kugawana nao faida, siyo mshahara.
 
Siyo kweli huoni wezetu waarabu wanavyonufaika na mali zoo za asili?
 
Moja ya jambo linalojitokeza kwenye mikeka ya uteuzi na kutumbua ni kujirudia kwa majina. Tumekuwa tunawaapisha watu walewale kila siku na hivyo hata maono yamebaki ni yale yale...
hao ni wateule kama Taifa la Israel. Akitolewa anapumzika tu. Anarudi tena
 

Kama mashushu wamesema unavuruga kwanini usiwekwe kando badala ya kuhamishwa post?

Maza akiambiwa mtu fulani hafai na yeye akakubali kwamba hafai inabidi amuweke kando mazima sio kufanya reshuffling kila siku. Unazunguka mule mule unategemea kupata matokeo tofauti?
 
Huwezi kupata mabadiliko yoyote kama Unatumbua na kuteua watu wale wale.
 
Kwa namna hii unaweza come na ka pepa title vicious cirlce of ministerial portifolio : tanzania case study.
Utapata fund akiaya nani
 
Hujuwi aliyeondolewa ndiye shushu mwenyewe. Utajuwaje? Kamaliza kazi moja anapelekwa kwenye kazi nyingine.

Mambo ya serikali wawachie serikali, ndiyo maana watu wanakula viapo vya kulinda siri. Kiapo cha kulinda siri, ukikiuka na kuvujisha siri hukumu yake ni kuuliwa, unakua ni msaliti. Hata uondolewe serikalinoi, kiapo hicho hakiishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…