Kwanini wanashauri usivute gari lenye Automatic Gearbox ukipata break down, badala yake upakie kwenye Flatbed Truck

International standard, kibongo bongo kanyaga twende, unajua wakati mwingine gari linajua kabisa lipo bongo na halipaswi kudeka?
 
Kuna jamaa alikua mbishi, akaivuta ford ranger AT, kutoka Moro hadi Dar, gari ilikua na changamoto ndogo tuu kwenye engine, kufika Dar, engine wakatengeza ikapona, kutest gari, Gearbox haifai. Kakwepa gharama za kubeba, kanunua gearbox mpya
 
wengi humu hamjui hata Jinsi giabox zinavyo fanya kazi.

kimsingi giabox inaambukizwa joto na injini.sasa ikitokea gari imezingua inahitaji kuvutwa kawaida injini lazima iwe off

wengi mnasema ukivuta unaweza kuunguza ama kuharibu giabox coz mzunguko wa oil hamna.

kazi ya oil nikurahisisha gia ziingie thmooth. unapovuta gari ukiweka freegia kwenye gari za auto unaivuta bila wasiwasi

Sabu kwanza oilí itakuwepo kwenye sampo klach zinapojizungusha zinachota oil liyopo kwenye valvu ches.pia mtikisiko wagari wakati inavutwa pia oil inapanda kwenye clutch na kuzilowesha.

kumbuka vyote hivyo vinafanyika injini ikiwa off sasa inaunguaje kwamfano?

gari inaunguza clutch ikiwa unaindesha hukuoil imepungua au imepita mudawake.
 
gari inayo vutwa haiwezi kupata joto hata sikumoja mkuu.

Weka facts mezani usiseme tu haiwezi kupata joto, how?

Kwanini baadhi ya gearbox waliweka secondary oil pump kwenye gearbox?

Humu ndani kuna mtu ametoa mfano wa Ford Ranger naye umeshindwa kumuelewa?
 
Gari yangu ni IST AWD ...Imeandikwa kabisa hairuhusiwi kuvutwa ni lazima ibebwe lasivyo wa disconnect torque converter kwenda tyre zote za nyuma na za mbele
 
wengi humu hamjui hata Jinsi giabox zinavyo fanya kazi.
Wewe ndio mtu wa kwanza humu ambaye unaonekana hujui jinsi Auto gearbox zinavyofanya kazi.
kimsingi giabox inaambukizwa joto na injini.sasa ikitokea gari imezingua inahitaji kuvutwa kawaida injini lazima iwe off
Yes gearbox inaambukizwa joto na engine, ila pia gearbox automatic inazalisha joto jingi kuliko operating temperature ya engine. Hili hata mimi mwenyewe nimeliprove. Gari ikitoka misele ukianhalia kwenye mashine atf temperature huwa ipo juu kuliko coolant temperature.

wengi mnasema ukivuta unaweza kuunguza ama kuharibu giabox coz mzunguko wa oil hamna.
Na huu ndio ukweli.

kazi ya oil nikurahisisha gia ziingie thmooth. unapovuta gari ukiweka freegia kwenye gari za auto unaivuta bila wasiwasi
Wewe unaijua kazi moja ya oil tena tena hata hujaitaja kwa usahihi. Kurahisisha kivipi? ATF ina kazi tatu ambazo ni kutengeneza pressure, kulainisha na kupooza.

Sabu kwanza oilí itakuwepo kwenye sampo klach zinapojizungusha zinachota oil liyopo kwenye valvu ches.pia mtikisiko wagari wakati inavutwa pia oil inapanda kwenye clutch na kuzilowesha.
Yes oil itakuwepo kwenye sump na kama ikipanda kidogo itaishia kwenye kigodoro cha oil filter. Kitu pekee kinachoweza kupandisha Oil ni pump na haizunguki punguza nadharia.

gari inaunguza clutch ikiwa unaindesha hukuoil imepungua au imepita mudawake.
Waliokuambia usiivute kwa speed zaidi ya 40 kama kuna ulazima wakuivuta siyo wajinga.
 
Kuna jamaa alikua mbishi, akaivuta ford ranger AT, kutoka Moro hadi Dar, gari ilikua na changamoto ndogo tuu kwenye engine, kufika Dar, engine wakatengeza ikapona, kutest gari, Gearbox haifai. Kakwepa gharama za kubeba, kanunua gearbox mpya
Gharama ambayo angetumia kupakia hiyo gari haifiki hata robo ya bei ya gearbox.
 
Acha ujuaji weee unavyoonekana wee magari umeyasoma zaidi kwenye vitabu sio kujifunza kwavitendo.

kwani unapo vuta gari kunahaja ya giabox kushift gia mfano 1 kwenda 2 nakuendelea?

halafu giabox inapata moto zaidi kuliko injini kwasababu Haina mfumo wa upoozaji kama injini.

wee jamaa ufundi sijui umejifunzia wapi.hivi unapotaka kupiga oil yagia box unatumia kanuni Gani Ili ujueipo sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…