Mtihani wa kwanza ni kukumbuka hiyo tarehe yenyewe ya kuzaliwa. Nimewahi achwa kwasababu ya kusahau birthday ya mtoto mzuri, nikashindwa kuwa wa kwanza kumu-wish happy birthday; yaani ile ng'ombe eti ilitegemea mie niamke saa 6:01 usiku "nimuimbie hepi besidei tuyu"!!
Nafikiri wanaume wengi hatuko vizuri/ hatuweki kipaumbele kwenye kukumbuka na kusherehekea siku za kuzaliwa, hatuoni mantiki ya kutumia muda na pesa tulizozipata kwa shida kusherekea sherehe ambayo haina manufaa. Kuna sisi wengine tunasahau hadi majina ya katikati ya wapenzi wetu,... au ukiulizwa "Ivi mpenzi wako amezaliwa wapi?" milioni inawekwa mezani ila huwezi kujibu.
Angalau ni vigumu kwa wanaume wengi kukumbuka "vitu vidogo vidogo visivyo vya msingi"... kama siku ya kuzaliwa.