Wagalatia 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
¹⁷ Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
¹⁸ Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
¹⁹ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
²⁰ ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
²¹ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.