Sitaki ku-justify mwanaume kuwa na wanawake wengi (zaidi ya mmoja) lakini pia tufikirie kidogo suala lifuatalo.
Uwiano wan wanaume kwa wanawake ni karibia sawa japo wanawake wanazidi kidogo. Tujiulize inawezekana vipi mwanaume kuwa na wanawake wengi kama uwiano haupishani sana? Mwanaume anapata wapi wanawake wengi kwa ajili yake peke yake?
Ukweli ni kwamba kati ya hao wanawake wengi wa mwanaume mmoja, pia wana wanaume wengine. Kwamba nao wanawake wana wanaume zaidi ya mmoja kwa maana hiyo. Hili suala liangaliwe kwa pande zote mbili.
Tofauti iliyopo ni kwamba mwanamke hawezi kuolewa rasmi na zaidi ya mwanaume mmoja. Mwanaume muislamu anaoa rasmi hadi wanne. Mkristo anaoa rasmi mmoja lakini kuna vidumu kadhaa pembeni. Vidumu hivyo pamoja na mke wakati mwingine, vina wanaume wengine. Ngoma ni 50/50!