Kwanini wanaume huwa na michepuko?

Kwanini wanaume huwa na michepuko?

mtu kaoa juzi tu hata wiki mbili hazijaisha,anatongoza na kutoa ahadi kedekede,

lakini ukweli ni kwamba yupo kwenye ndoa,

mie najiuliza tatizo ni nini hasa kwa hawa kaka zetu?

Kutulia na mke mmoja hamuwezi?

Badilika tafadhali.

haya maneeeno walinenaga wazeee wa zamanii ukiwa mujanja kuchapiana ni siri ya ndaaani sasa nyieee mwashangaaa nini? Hakuna jipya chini ya jua.

Maisha yenyewe ni mafupi tuacheni tunakula utamuuu, wengne hatuna wake/waume tunapata utaaamu.
 
Hongera kwa hilo
 
Nina hakika kuwa kwa wanawake ni asilimia kidogo sana,
Na mpaka aamue kufanya hivyo mume atakuwa amemtesa vya kutosha,
Wanawake wameumbiwa uvumilivu na sio wanaume.

Hizo pete wala siku hizi hazifichwi tunaonyesha live sooo kila m1 anajua kuna boya anamiliki hii ngoja nimchanganyie madesa yeye si anajifanya busy sisi tunakaza hizi bolt&nut mpk zifikie mwishoooo.
 
Wanaume wenyewe hawa wanaosema mboga moja hainogi!!
Kweli Mungu anahitajika kuingilia kati

Mwacheni Mungu aandae ukumu zake hausiki kwa hili. Figa 1 tangu lini likatenga sufuria jikoni? na wee bidada kisimani ukienda lazima uwe na kidumu coz unaweza beba ukaeeeeendaaa na safari kufka karibu na ulipo ukajikwaa ndoo ikadondoka huoni kidumu kitakusaidia!
 
Hizo pete wala siku hizi hazifichwi tunaonyesha live sooo kila m1 anajua kuna boya anamiliki hii ngoja nimchanganyie madesa yeye si anajifanya busy sisi tunakaza hizi bolt&nut mpk zifikie mwishoooo.

Kama kwako hilo ni sahihi endelea wala usiache,
Wewe ni mtu mzima na uko responsible kwa matendo yako
 
Mwacheni Mungu aandae ukumu zake hausiki kwa hili. Figa 1 tangu lini likatenga sufuria jikoni? na wee bidada kisimani ukienda lazima uwe na kidumu coz unaweza beba ukaeeeeendaaa na safari kufka karibu na ulipo ukajikwaa ndoo ikadondoka huoni kidumu kitakusaidia!

Uamuzi ni wako,tafakari chukua hatua
 
MKE NA NYUMBA NDOGO NANI WA MUHIMU ZAIDI?

Nimepata swali hili kutokana na kisa hiki nilichokishuhudia:

Hivi majuzi kuna mwanamke alipewa taarifa kuwa mume wake alikuwa na kimada sehemu Fulani(almaarufu kama nyumba ndogo) mwanamke huyo aliamua kwenda kushuhudia ikiwa kinachosemwa ni cha kweli au watu tu wasioitakia mema ndoa yake pendwa,kufika huko alikuta kuwa kilichosemwa ni kweli mtupu tena hamna chumvi,kwa wivu wa mapenzi kwa mumewe (tena wanasema uchungu wa mume aujuae mke!) mwanamke Yule aliamua kuisogelea nyumba ndogo ya mumewe ili kuivagaa lakini kabla hajatimiza lengo lake tayari mume wake alishafika karibu yake kwa ajili ya kuilinda nyumba ndogo yake isipigwe na mama watoto wake watatu!!!!!!!!!!!!!!!!

Kibaya na cha kusikitisha mume huyo hakuishia tu kudhibiti mke wake bali pia kumpiga makofi kadhaa na kumzuia kwa hali na mali kutoisogelea nyumba ndogo yake,ambayo na yenyewe ilikuwa ikimjibu mwenye mali kwa jeuri zote,jambo lililopelekea mke kuondoka akiwa na uchungu mkali na maumivu ya mapenzi ndani ya moyo huku nyuma akifuatiwa na mumewe msaliti,ambaye mara baada ya kufika nyumbani alianza kumshambulia kwa maneno ya kejeli bila hata walau kuomba msamaha kwa usaliti alioufanya kwa siku hiyo,mke akaongezewa maumivu juu ya maumivu.(nadhani sote tunaelewa jinsi mapenzi yanavyoumiza na kwa hiyo tunaelewa vizuri kabisa jinsi mwanamke huyu alivyokuwa akihisi kwa wakati huo)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kisa hiki kilinipa maswali kadhaa kwa wanaume wenye nyumba ndogo:

1.Hivi ni nani bora zaidi kati ya mke wa ndoa na nyumba ndogo?

2.kama ni nyumba ndogo,umuhimu wake uko wapi kuushinda ule wa mke anayejua usiku umelalaje,umeamkaje na kukuzalia watoto kwa moyo mmoja licha ya uchungu mkali?

3.assume ndo wewe sasa unamfuma mkeo ana mwanamume mwingine na mkeo anaanza kukuponda na kumtetea Yule mwanaume mwingine,hiyo imekaaje?utajisikiaje?unahisi itakuwaje baada ya hapo? utachukua hatua gani mkifika nyumbani?

4.kama utaumia,unapomfanyia mkeo kisa kama hicho unafikiri yeye anahisi vipi?au unaamini kabisa hana hisia ila ni jiwe?au unaamini kuwa kwa wewe ni halali kabisa kumtenda hivyo ila sio yeye?

5.hivi nini unachokosa kwa mke na kukipata kwa nyumba ndogo?

6.kama kuna unachokikosa umewahi kujaribu kukaa chini na mkeo na kumweleza akupe unachokosa?

7.ikiwa ni wewe mwenyewe tu umejitune kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,hivi inashindikana kuonyesha heshima licha ya kuwa na nyumba ndogo?

8.ikiwa umeshindwa kuonyesha heshima na mambo yako kujulikana na mkeo kufika eneo husika ukiwa na nyumba ndogo yako,hivi unahisi kupungukiwa ikiwa utaamua kuwa upande wa mkeo walau mara moja?walau kuthibitisha yale maneno yako uliyoahidi ya kumpenda nyakati zote kwenye shida na raha siku ya ndoa yenu?

Najua wapo baadhi ya wanaume walio na nyumba ndogo na wasio nazo pia, kwa hiyo karibuni wote tuchangie mawazo yetu kuhusu hili suala kwa wale wenye nazo watupe majibu ya:

Ni nani bora wake zao majumbani au nyumba zao ndogo? na nini kinawapelekea kuwa na hizo nyumba ndogo?ikiwa nyumba ndogo ni muhimu zaidi,umuhimu zaidi wa nyumba ndogo unatokana na nini?

Na kwa wasio nazo pia nao wanakaribisha kutueleza

Wanawachukuliaje wanaume wenzao walio na nyumba ndogo na kuzithamini zadi nyumba ndogo kuliko wanavyowathamini wake zao?

Karibuni wana MMU.
 
Mke ana thamani sana kuliko nyumba ndogo ndo maana akaolewa.

Kosa la baadhi ya wanawake ni kutokuukubali ukweli kuwa mwanaume hajawahi kutosheka na mwanamke mmoja. Kosa alilolifanya huyo mwanamke ni kwenda kuvamia poozeo la mmewe linalomfariji mara anapotaka faraja mbadala.

Mwanamke mwenye busara za kutosha ahangaiki kumfuatilia mmewe, kama mmewe anamtimizia mahitaji yote ya kimwili, kikojoleo, na kifamilia. Ni kujitafutia presha bure tu.

Mpe pole huyo mama, mwambie akome kumfuatilia mwanaume rijali, atakufa bure aache wanae wanateseka.
 
Huyu mwanamme mshenzi tuu wa tabia,hata iweje huwezi kumpiga mkeo wa ndoa mbele ya huyo mzinzi mwenzie,anadhani hiyo nyumba ndogo inamuona wamana? wanaume wengine hata busara hawana.......
 
Yani ndo umejiuliza maswali yote hayo kwa kisa hicho tu...! mi sina jibu bhana
 
Hata kama kutoka nje ya ndoa kupo lakin huy jamaa kazd, huwez kumdhalilisha mkeo kias hcho, na itakuweje na yeye akiamua kuishi liwalo na liwe akaanza kukuletea wanaume mbele yako?? Dah! Hiii hatareee mura ayaa!
 
Miss Blue G kwa kuzingatia namba 6 kwa thread yako hivi unafikiri kila kitu unachokipata nje unaweza kukaa chini na mkeo kumuomba naye akupatie? Uzuri nyumba ndogo zinajua fika kabisa kuwa kwa heshima ya ndoa ilivozoeleka kuna baadhi ya vitu mke hawezi mpa mumewe. Naye ndo anavitumia ili kuziba pengo la anachokimisi mwanaume.

Mchepuko is inevitable. Take it from me.
 
Last edited by a moderator:
kwanza shikamoo babu mpendwa afu nimekumisije jamani??????????bibi mzima lakini?

haya back to the topic my babu hapo kwenye red miaaaaa nimeipenda hiyo kwa wewe kutambua bibi ana thamani kuliko vidosho vyako vingine.

ila hapa kwenye blue nina swali kwako,huo ukweli wa kuwa mwanaume hajawahi kutosheka na mwanamke mmoja ni ukweli unaotokana na nini?kimaumbile,ndivyo walivyoumbwa au ni jinsi tu wanaume wengi walivyojiwekea?

na hapo kwenye kijani hivi wewe hata kama bibi anakutimizia mahitaji yako yote basi huna haja ya kumfatilia?hata arudi saa nne usiku?apigiwe simu usiku wa manane na sauti ya kiume?hata usikie tetesi kuwa unaibiwa? nini maana ya kuwa mume na mke? ni kujaliana tu pale mnapokuwepo nyumbani au hata kutaka kujua ikiwa mwenzio yu salama hata akiwa mbali na wewe?

na mwishowe hapo kwenye pink unaonaje na wewe nikikwambia ukome kumfuatilia bibi kwani na yeye ni mwanamke rijali na hivyo utaishia tu kuwa na presha?
Mke ana thamani sana kuliko nyumba ndogo ndo maana akaolewa.

Kosa la baadhi ya wanawake ni kutokuukubali ukweli kuwa mwanaume hajawahi kutosheka na mwanamke mmoja. Kosa alilolifanya huyo mwanamke ni kwenda kuvamia poozeo la mmewe linalomfariji mara anapotaka faraja mbadala.

Mwanamke mwenye busara za kutosha ahangaiki kumfuatilia mmewe, kama mmewe anamtimizia mahitaji yote ya kimwili, kikojoleo, na kifamilia. Ni kujitafutia presha bure tu.

Mpe pole huyo mama, mwambie akome kumfuatilia mwanaume rijali, atakufa bure aache wanae wanateseka.
 
Mahusiano ya kimapenzi sio pai, kuna mwingine atalinda nyumba ndogo, mwingine angeweza timuka, mwingine angebembeleza mkewe.

Kwa hiyo, hatuwezi hukumu wanamme wote kwa sinario hii tu. Lakini nishaona mtu pia katikisa familia sababu ya kuilinda nyumba ndogo yake. Kisa? Eti nyumba kubwa ni korofi. Hii inajustify cheating? No way, kama ni korofi basi aachane nayo.
 
nimeipenda sana hiyo attitude yako promiseme be blessed nothing like a wife hata uumwe vipi atakuwa na wewe,usiku kucha unaumwa yeye ndo anahangaika na wewe umwa serious uone kama hao nyumba ndogo wana hata muda na wewe,kiukweli wao wako after your pouch your wallet kwa sababu unawaweka mjini.be blessed mzee na endelea kumrespect mke wako hivyo hivyo.
Huyu mwanamme mshenzi tuu wa tabia,hata iweje huwezi kumpiga mkeo wa ndoa mbele ya huyo mzinzi mwenzie,anadhani hiyo nyumba ndogo inamuona wamana? wanaume wengine hata busara hawana.......
 
Last edited by a moderator:
Yani ndo umejiuliza maswali yote hayo kwa kisa hicho tu...! mi sina jibu bhana
Price nimeshangazwa kidogo na response yako!!!but any way naomba nikuulize haya:
umeolewa?kama ndiyo,umewahi kuwa cheated na mmeo? kama ndiyo,umewahi kudhalilishwa au kupigwa na mmeo mbele ya kimada wake?

kama hujaolewa,unahisije kuona wanawake wenzio wanaoteseka sana ndani ya ndoa zao? unahisjie mwanamke mwenzio akipigwa au kudhalilishwa na mume wake? je unaumia na kujiuliza mara mbili mbili ndoa yako pia iakuwaej siku moja au unahisi wewe hayawezi kukupata?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom