MKE NA NYUMBA NDOGO NANI WA MUHIMU ZAIDI?
Nimepata swali hili kutokana na kisa hiki nilichokishuhudia:
Hivi majuzi kuna mwanamke alipewa taarifa kuwa mume wake alikuwa na kimada sehemu Fulani(almaarufu kama nyumba ndogo) mwanamke huyo aliamua kwenda kushuhudia ikiwa kinachosemwa ni cha kweli au watu tu wasioitakia mema ndoa yake pendwa,kufika huko alikuta kuwa kilichosemwa ni kweli mtupu tena hamna chumvi,kwa wivu wa mapenzi kwa mumewe (tena wanasema uchungu wa mume aujuae mke!) mwanamke Yule aliamua kuisogelea nyumba ndogo ya mumewe ili kuivagaa lakini kabla hajatimiza lengo lake tayari mume wake alishafika karibu yake kwa ajili ya kuilinda nyumba ndogo yake isipigwe na mama watoto wake watatu!!!!!!!!!!!!!!!!
Kibaya na cha kusikitisha mume huyo hakuishia tu kudhibiti mke wake bali pia kumpiga makofi kadhaa na kumzuia kwa hali na mali kutoisogelea nyumba ndogo yake,ambayo na yenyewe ilikuwa ikimjibu mwenye mali kwa jeuri zote,jambo lililopelekea mke kuondoka akiwa na uchungu mkali na maumivu ya mapenzi ndani ya moyo huku nyuma akifuatiwa na mumewe msaliti,ambaye mara baada ya kufika nyumbani alianza kumshambulia kwa maneno ya kejeli bila hata walau kuomba msamaha kwa usaliti alioufanya kwa siku hiyo,mke akaongezewa maumivu juu ya maumivu.(nadhani sote tunaelewa jinsi mapenzi yanavyoumiza na kwa hiyo tunaelewa vizuri kabisa jinsi mwanamke huyu alivyokuwa akihisi kwa wakati huo)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kisa hiki kilinipa maswali kadhaa kwa wanaume wenye nyumba ndogo:
1.Hivi ni nani bora zaidi kati ya mke wa ndoa na nyumba ndogo?
2.kama ni nyumba ndogo,umuhimu wake uko wapi kuushinda ule wa mke anayejua usiku umelalaje,umeamkaje na kukuzalia watoto kwa moyo mmoja licha ya uchungu mkali?
3.assume ndo wewe sasa unamfuma mkeo ana mwanamume mwingine na mkeo anaanza kukuponda na kumtetea Yule mwanaume mwingine,hiyo imekaaje?utajisikiaje?unahisi itakuwaje baada ya hapo? utachukua hatua gani mkifika nyumbani?
4.kama utaumia,unapomfanyia mkeo kisa kama hicho unafikiri yeye anahisi vipi?au unaamini kabisa hana hisia ila ni jiwe?au unaamini kuwa kwa wewe ni halali kabisa kumtenda hivyo ila sio yeye?
5.hivi nini unachokosa kwa mke na kukipata kwa nyumba ndogo?
6.kama kuna unachokikosa umewahi kujaribu kukaa chini na mkeo na kumweleza akupe unachokosa?
7.ikiwa ni wewe mwenyewe tu umejitune kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,hivi inashindikana kuonyesha heshima licha ya kuwa na nyumba ndogo?
8.ikiwa umeshindwa kuonyesha heshima na mambo yako kujulikana na mkeo kufika eneo husika ukiwa na nyumba ndogo yako,hivi unahisi kupungukiwa ikiwa utaamua kuwa upande wa mkeo walau mara moja?walau kuthibitisha yale maneno yako uliyoahidi ya kumpenda nyakati zote kwenye shida na raha siku ya ndoa yenu?
Najua wapo baadhi ya wanaume walio na nyumba ndogo na wasio nazo pia, kwa hiyo karibuni wote tuchangie mawazo yetu kuhusu hili suala kwa wale wenye nazo watupe majibu ya:
Ni nani bora wake zao majumbani au nyumba zao ndogo? na nini kinawapelekea kuwa na hizo nyumba ndogo?ikiwa nyumba ndogo ni muhimu zaidi,umuhimu zaidi wa nyumba ndogo unatokana na nini?
Na kwa wasio nazo pia nao wanakaribisha kutueleza
Wanawachukuliaje wanaume wenzao walio na nyumba ndogo na kuzithamini zadi nyumba ndogo kuliko wanavyowathamini wake zao?
Karibuni wana MMU.