Achana na imani za kijinga zisizo na kichwa wala miguu hakuna cha kafara wala uchawi.
Muwe mnawawahisha wajawazito hospitali wapate vipimo na huduma stahiki za kiafya.
Usikae kusubiri hadi siku ama wiki ya kujifungua, kuna matatizo mengi anaweza kupata mama mjamzito kama vile presha kupanda ama kushuka na kuhatarisha uhai wa mama na kichanga kilicho tumboni.
Achana na imani zisizo na kichwa wala miguu. Sasa kama maombi yalimuokoa mama mjamzito, hayo maombi yalishindwa nini kumuokoa mtoto? Ama mungu alichagua aue mtoto abakize mama? Ama maombi ya mtoto hayakufika huko mbinguni?