Kwanini wanaume mnawatoa wanawake wenu kafara?

Kwanini wanaume mnawatoa wanawake wenu kafara?

Achana na imani za kijinga zisizo na kichwa wala miguu hakuna cha kafara wala uchawi.

Muwe mnawawahisha wajawazito hospitali wapate vipimo na huduma stahiki za kiafya.

Usikae kusubiri hadi siku ama wiki ya kujifungua, kuna matatizo mengi anaweza kupata mama mjamzito kama vile presha kupanda ama kushuka na kuhatarisha uhai wa mama na kichanga kilicho tumboni.

Achana na imani zisizo na kichwa wala miguu. Sasa kama maombi yalimuokoa mama mjamzito, hayo maombi yalishindwa nini kumuokoa mtoto? Ama mungu alichagua aue mtoto abakize mama? Ama maombi ya mtoto hayakufika huko mbinguni?
Ajabu ,na ubaya wa mambo haya anaanzishaga uzushi mtunmmoja tu basi wote wanaamini huo ujinga
 
Serikali haiusiki na uchawi so kumshtaki ni ngumu analipa faini
Mimi nimesoma sheria ndugu yangu.

Sheria dhidi ya uchawi ipo na mtu anaweza kuwhtakiwa ushahidi ukiwepo.

[_______
CHAPTER 18
_______
THE WITCHCRAFT ACT
An Act to provide for the punishment of witchcraft and of certain acts connected
therewith.
[28th December, 1928]
Ords. Nos.
33 of 1928
25 of 1935
45 of 1956
Act No. 12 of 1998
Short title 1. This Act may be cited as the Witchcraft Ac...]

Ipo mkuu wangu na mtu akitithibitika anafanya shirki anaadhibiwa kisheria
 
Mimi nimesoma sheria ndugu yangu.

Sheria dhidi ya uchawi ipo na mtu anaweza kuwhtakiwa ushahidi ukiwepo.

[_______
CHAPTER 18
_______
THE WITCHCRAFT ACT
An Act to provide for the punishment of witchcraft and of certain acts connected
therewith.
[28th December, 1928]
Ords. Nos.
33 of 1928
25 of 1935
45 of 1956
Act No. 12 of 1998
Short title 1. This Act may be cited as the Witchcraft Ac...]

Ipo mkuu wangu na mtu akitithibitika anafanya shirki anaadhibiwa kisheria
Sikujua naomba Muongozo zaidi niweze kufahamu zaidi ili nijue nafanyaje
 
Nenda karipoti kwa Mwamposa hizo kafara zitakoma
Huyo tena ndio mtoa kafara haswa, alikanyagisha watu mafuta watu zaidi ya 20 wakafa. Hawa manabii wa uongo wengi watoa kafara, nabii mdogo asiye na jina kubwa monthly anatakiwa kafara sio chini ya watu 7.
 
Wanaume hivi kwa wale wanatoa wanawake kafara wanaonaje wenzio nakwanini mnatoa watu kafara?

Rafiki yangu alikuwa anatolewa na mchumba wake kafara isingekuwa maombi kweli leo hii angeenda na kichanga tumboni ila kichanga kilikufa. Mama akabaki kwa bahati nzuri.

Wanaume muwe na roho basi kuua wanawake kisa mali sio fresh.
Babu tale anaongeza sauti ya redio
 
Tatizo mnakaririshwa na kupotezwa na mitume na manabii wa uongo, maombi mengi mnayoombewa siyo ya kweli . Maombi ya kweli ni yale ya kujiombea mwenyewe.

Mimba kutoka au kuharibika ni matatizo ya kibinadamu na kimaumbile nenda hospitali ukaonane na daktari wa maswala ya wanawake / maswala ya uzazi .

Ewe mwanamke achana na imani potofu achana na tamaa za mali za wanaume pia, maisha ni kidogo kidogo, kupanda na kushuka
 
Mlijuaje kama mwanaume ametoa hio kafara?.

Siku nilioacha kuamini waganga kumuona mganga amekwenda polisi kisa mkewe anapelekewa moto na muhuni wa mtaani.

Hakuna uchawi wala nini
😂😂😂
 
Sababu ni agano la Uchawi, Mizimu, waganga..

Kwa uchawi yaweza ikawa mume ni mchawi hivyo anatakiwa atoe kafara.

Wakati mwingine ni mume anakuwa ameingia agano na waganga hivyo lazima atoe kafara ya mimba.

Upande wa mizimu inakuwa ni upande wa mume Kuna agano la kafara ya kutoa mimba hivyo ndio inatoka...

Familia ya mume pia yaweza kuwa na Uchawi, uganga, mizimu yote inataka kafara ya mimba...
Acha kuwaza ujinga na kuchonganisha watu wewe,unajua sababu za miscarriage?unajua Rhesus factor ni nini kwenye mimba?mshauri aende Kwa daktari bingwa
 
Back
Top Bottom