Kwanini wanaume wa Dar mnakuwa hivi?

Sasa huo ushamba wenu si kila mtu anauweza we umeona wapi mtu ale "ugali mkubwa" usiku kwani unaenda kupigana??
Kwani unajua nilichokua nafanya usiku?
Au unajua nilikuwa nimefuata kushangaa mataa ya mjini?

Au wewe ndiye yule kijana aliyekuwa ananiuliza "wewe kaka umetokea Seminari?
Baada ya kuona kazi yangu niliyokuwa nafanya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili finyu kuzani uanaume ni kula ugali tena donna, hao ndio wanatembea vifua mbele kabisa[emoji23][emoji23][emoji23]
Unaweza kuta wewe umekulia bush kabisa na wazazi wako wa bush na wamekuwa wakila ugali kwa sana tu, ila umeenda mjini miaka 10 tu basi unaudharau ugali!

Mafuta ya chips mpaka yamekubadilisha akili kabisa na kujiona una big mind, kumbe empty set kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah pole sana kiongozi, kwa taarifa tu nimezaliwa muhimbili hapo, na sasa natimkia ughaibuni, inshaalah hata nikifa huku mwili wangu utarudi kuhifadhiwa kwenye jiji la mzizima washamba mnalolikurupukia.
 
Kukuongezea tu Babu na bibi yangu wote ni wazaramo wa kisarawe.😂😂
 
Bora hata chips dume... hivi MWANAUME inakuwaje kushindia kyepe yai??
 
Jamaa anakufukuza kiaina,anajua wewe ni mlafi halafu anakuletea vichips.
 

Duh ila wanaume wa dar sio siri mnahitaji maombi sio bure, wewe fikiria muwa tu wenyewe mnamenyewa ndo muweze kula, hujakaa vizuri mahindi ya kuchoma mpaka muweke ndimu na pili pili, mara hadi nazi na mihogo pia mpaka mkatiwe katiwe, sasa week iliyopita ndo wanenivunja mbavu maana nimepita hapo nimekuta sasa hivi habari ya mjini wanashindana kura mbegu za maboga,,,,, dah!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…