Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho.
Mwanamke, utazaa kwa uchungu.

Siku hizi wanawake wanakula kwa jasho na bado wanazaa kwa uchungu wakati wanaume achilia mbali kutokuzaa, hata ile kula kwa jasho inawashinda.
Labda uniambie huko vijijini..ila mjini kama daslam babu tutakuwa tunadanganyana..Wanawake ni dependants sana kwa wanaume.
 
Haya yote yanatokana na Yale maazimio mliyofanya pale Beijing sikuile! So msijifanye hamjui tatizo lilianzia wapi!
 
Kamwe sikio haliwezi zidi kichwa..

Mwanaume kutimiza majukumu yake huwa inategemea upande wapili mke, mwanaume anahitaji msaidizi(mke) anaejitambua mwenye adabu, heshima na unyeyekevu kwa mume wake, mambo ya kumtunishia kifua mwanaume usitegemee familia kuwa na amani na kuyafanya majukumu yake vizuri
 
Labda uniambie huko vijijini..ila mjini kama daslam babu tutakuwa tunadanganyana..Wanawake ni dependants sana kwa wanaume.

Hao watu wa ajabu wapo kote mjini na vijijini.

Hata mtoa mada hajasema wanaume wote, hali kadhalika wapo wanawake wenye mushkeli lakini sio wote.

JF unashuhudia wanaume wakilalamika kwa vitu vidogo au kushindwa kusimamia majukumu yao hadi unashangaa.

Huku kijijini kuna majimama ya kulea vijana? Wanawake wangapi wapo kazini wanapambana na maisha?
 
Kamwe sikio haliwezi zidi kichwa..

Mwanaume kutimiza majukumu yake huwa inategemea upande wapili mke, mwanaume anahitaji msaidizi(mke) anaejitambua mwenye adabu, heshima na unyeyekevu kwa mume wake, mambo ya kumtunishia kifua mwanaume usitegemee familia kuwa na amani na kuyafanya majukumu yake vizuri
Wewe ndio unatimiza majukumu yako yote au unamuongelea nani?

Unamaanisha mwanamke kudai haki sawa ndo kutunisha kifua? Kama mwanamke anafanya kazi kama mwanaume na kujenga familia juu kuna tatizo akidai haki zake?

Na je hawa ambao wanafanya kazi wanaoonekana na mapungufu na si wife material kwasababu wapo independent?
 
Soma kwa utulivu uelewe usirukeruke kama popcorn,

Hujaelewa nilichoandika umerukia kujibu kwa mihemko, nyie ndiyo mnafanya ndoa zenu zipitie tabu pasipokujua na kujilaani kisa mdomo mnaoengea sana,

Hakuna mwanaume atashindwa kutimiza majukumu yake kikamilifu ya kifamilia kwa mke wake kama anaejiheshimu yeye na kumheshimu mume wake,
 
SIJAKURUPUKA naona wewe ndio unajitoa fahamu!!Kwasababu unaepuka kujibu kila nilokuuliza!

Wapo kama unajizungumzia jizungumzie wewe usijumuishe wote!

Heshima sio tatizo mbona lakini je unastahiki hio heshima au uheshimiwe tu kwasababu mwanaume au umeoa?Heshima inatakiwa iwepo pande zote!
 
Unapomtaja MWANAUME unamzungumzia mtu anayejitambua na aliyekomaa kiakili.....

MVULANA ni kijana mwenye jinsia ya kiume ambaye bado hajakomaa kiakili na anayeongozwa na mihemko badala ya utashi wa akili yake.......

Safari ya kutoka kwenye UVULANA kuelekea kwenye UANAUME hapo ndipo wanapojichuja kati ya wanaume na wavulana...........na hapo panapozuka mtafaruku kwa kuwa wavulana ni wengi kuliko wanaume.......
 
Wanaume wa sasa mna matatizo gani haswa maana sielewi tatizo lenu ni kwamba hamtaki mabadiliko au akili zimeelemea kwenye mfumo dume au ni nini hasa?Hamna lilo la kheri kwenu,wanaume hamuishi malalamiko mnaongea hata kuwazidi wanawake, maana najua mwanamke ni itikadi yake kupenda kuongea.

Wanaume nyinyi wa karne hii mnataka mtu kama bibi zetu(kitabia na anavyojiweka) na wakati huohuo mnataka mwanamke aliyeelimika,mpenda maendeleo,mchapa kazi n.k ili musaidiane majukumu.
Mnasahau kama bibi zetu jukumu lake kubwa lilikuwa kujenga familia.Kama mwanamke anaingiza kipato kama ww au ikiwezekana kukuzidi wewe mwanaume usitegemee upewe treatment na mwaka 47 lazima mfumo mzima wa maisha ubadilike!
Hii ni 2021 inabidi mubadilike muendane na wakati uliopo waungwana!

Ninachojiuliza hasa ni kwamba mna hofu mkiwa na mwanamke aliyeelimika atawapa changamoto nyingi kwasababu amepambazuka akili na ana upeo wa kufikiri tofauti na ambaye hana elimu?na hamtoweza kumwambia lolote tu akubali bila kutaka kujua kwanini?
Je hilo litapunguza heshima kwenu au litaondoa uanaume wenu?

Tusisahau pia wanawake haohao wachapakazi ndo wanaozaa na kujenga familia kumaanisha wanabeba mzigo mzito kuliko hata wa mwaka 47!

Tuchukulie women empowerment ni kitu chenye manufaa kwa mwanamke na mwanaume na tuache kukandamiza wanawake kwasababu wamepata sauti na kuerevuka!

Tafadhali nahitaji michango ya watu mnaojielewa.Ahsanteni na karibuni!
Kaka mkubwa, kopi ya kupigiwa mfano, naongea kwa niaba ya wengi waliokaa kimya.

Nakuomba utuondoe wanaume tunaojua kuchukua majukumu ya kutatua matatizo ya familia, tena si immediate family tu, mpaka extended family.

Hapa ninavyoandika nimetoka kusawazisha mambo mpaka mtu kaimba pambio.
Kaamka kakuta $900 kwenye simu amalize matatizo yaliyomkaba.

Acheni tabia za kutulundika wanaume kwenye makundi bila hata ya kunyambulisha.

Wengine mnatunyanyasa na kutuonea kwa kukosa uangalifu kwenye maneno yenu.
 
Kaka mkubwa naongea kwa niaba ya wengi waliokaa kimya.

Nakuomba utuondoe wanaume tunaojua kuchukua majukumu ya kutatua matatizo ya familia, tena si immediate family tu, mpaka extended family.

Hapa ninavyoandika nimetoka kusawazisha mambo mpaka mtu kaimba pambio.

Acheni tabia za kutulundika wanaume kwenye makundi bila hata ya kunyambulisha.

Wengine mnatunyanyasa na kutuonea kwa kukosa uangalifu kwenye maneno yenu.
Hongereni sana kwa wanaume mnaotambua majukumu yenu kama wanaume katika familia zenu na jamii kwa ujumla.
Kama wewe unaona hii haikuhusu then huna haja ya kughafirika.

Ninaowaongelewa wanajitambua na washakuja wengi,wengine hata kuniuliza ka nimempikia mume wangu?😀😀 like ndo jambo la pekee wanaloliona kwa mwanamke ni kumtumikia mwanaume.
 
Back
Top Bottom