Naona wewe bado ni mgeni sana na ulimwengu wa mahusiano sababu umeandika kwa namna ya mtu ambaye hana experience yoyote juu ya maswala ya ndoa.
Nitakuuliza maswali kadhaa na ukiweza kuyajibu pengine tunaweza kuwa katika mlengo mzuri kujadili hii mada yako uliyoleta!
1. Una umri gani?! Nakuuliza umri ili nijue nazungumza na mtu ambaye amepita umbali gani katika utu uzima.
2. Unayajua mahitaji ya mwanaume anayotaka kutimiziwa na mwanamke?! Usiniambie mambo ambayo umesikia, nipe wewe personally unachojua na kama haujui (for the sake of honesty and goodwill) sema sijui nielimishe ila usije na hoja mitandaoni unazookota huko kuhusu wavulana ukiita ni wanaume.
3. Nani role model wako katika haya maisha kama mtoto wakike?! Tafadhali kama katika list ya role models au role model wako hawapo katika ndoa usihangaike kujibu hili swali sababu hatutakuwa na cha kujadili kama role model wako mwenyewe ni kipofu kama wewe.
4. Ni nani aliyekuambia wanaume wanataka mwanamke mjinga au anaepelekwa kama bendera?! So kwa assumption yako ni kuwa tunawatafutia watoto wetu mama ndezi?! (una mengi ya kujifunza kuhusu tofauti ya mke bora na mwanamke wa kawaida wa kisasa)
5. Kama assumption yako ni kuwa wanaume wanalalamika (of which sina uhakika kama huwa unaelewa kinachokemewa au kupigwa kelele na hao unaoita wanaume), je umeshawahi jitathimini wewe kama binti mdogo unaeuingia utu uzima mzito kwa kasi, umejitafakari juu ya uwezo wako na mapungufu yako kwa marejeo ya uhalisia wa namna mwanamke anatakiwa kuwa, yaani kwa mfano wakisema mke bora anatakiwa kuwa na vigezo 50, wewe una vingapi na je unaweza viainisha hapa tuone namna ulivyobora?!
6. Hebu tukiacha tu mijadala na mabishano ya mtandaoni baina ya wavulana na wasichana. Wewe umejipanga vipi kuingia taasisi ndoa kwa muktadha wa mchango gani utatoa kwa mumeo mtarajiwa?! Je huyu mume atapata offer gani ya thamani kutoka kwako tukiacha kumpa mwili wako kwaajiri ya kugegedana, una kipi kipya ambacho upo taayari kutoa bila manung'uniko ya kisichana.
7. Je, ndoa kwako ni jambo takatifu na muhimu?! Kama ni ndio hebu tuambie umejiandaaje kuheshimu hilo agano na maandalizi yako kuliingia, na kama hapana, hebu tueleze ni kwann tena unajihusisha na majadiliano ya mahusiano ile hali ndoa kwako si jambo muhimu.
Jibu hayo kwanza then nikuhoji zaidi.