Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Na bahati mbaya sana siku hizi kila mwanamke ana priorities zake, huyu anataka ukoloni, mwingine anataka usasa etc ilimrad tafran tu.
Inabid utuambie wewe ni aina gani ya mwanamke
 
Wanaume wa sasa mna matatizo gani haswa maana sielewi tatizo lenu ni kwamba hamtaki mabadiliko au akili zimeelemea kwenye mfumo dume au ni nini hasa?Hamna lilo la kheri kwenu,wanaume hamuishi malalamiko mnaongea hata kuwazidi wanawake, maana najua mwanamke ni itikadi yake kupenda kuongea.

Wanaume nyinyi wa karne hii mnataka mtu kama bibi zetu(kitabia na anavyojiweka) na wakati huohuo mnataka mwanamke aliyeelimika,mpenda maendeleo,mchapa kazi n.k ili musaidiane majukumu.
Mnasahau kama bibi zetu jukumu lake kubwa lilikuwa kujenga familia.Kama mwanamke anaingiza kipato kama ww au ikiwezekana kukuzidi wewe mwanaume usitegemee upewe treatment na mwaka 47 lazima mfumo mzima wa maisha ubadilike!
Hii ni 2021 inabidi mubadilike muendane na wakati uliopo waungwana!

Ninachojiuliza hasa ni kwamba mna hofu mkiwa na mwanamke aliyeelimika atawapa changamoto nyingi kwasababu amepambazuka akili na ana upeo wa kufikiri tofauti na ambaye hana elimu?na hamtoweza kumwambia lolote tu akubali bila kutaka kujua kwanini?
Je hilo litapunguza heshima kwenu au litaondoa uanaume wenu?

Tusisahau pia wanawake haohao wachapakazi ndo wanaozaa na kujenga familia kumaanisha wanabeba mzigo mzito kuliko hata wa mwaka 47!

Tuchukulie women empowerment ni kitu chenye manufaa kwa mwanamke na mwanaume na tuache kukandamiza wanawake kwasababu wamepata sauti na kuerevuka!

Tafadhali nahitaji michango ya watu mnaojielewa.Ahsanteni na karibuni!
Point yako iko wap??
Naona wewe ndo waleta malamiko
 
Jamani, si tulishakubaliana maisha ya sasa ni 50/50! Yaani hakuna kukubali kulea wala kulelewa?

Hao wanaokubali kuishi na kulea huoni nao wana shida pia coz maisha ya sasa huwezi kulinganisha na zama zile.

Kama mke unaamka alfajiri, unaacha watoto nyumbani kwenda kutafuta kipato, unarudi jioni umechoka, maana yake ni kuwa upo tayari kuchangia kifedha maendeleo ya familia yako. Usilalamike hata kidogo.

Kama mke unakaa nyumbani kuhudumia familia, hakikisha unatimiza majukumu yako kwa kulea watoto vizuri, baba atatafuta hela ili kukuhudumia wewe na watoto.

Tatizo wanawake wengi you want to eat your cake and have it.
 
Ngoja nitoke na hii nukta.

Mwanamke aliye elimika ana sifa gani,naomba uwasemee hao wadau.

Hao wanaume wa karne hii wanamuelezea vipi mwanamke mchapa kazi na mpenda maendeleo ?

Ninasema mimi Zurri ya kuwa :
Katika kitu ambacho huwa nawashangaa vijana wenzangu wa kiume ni wao kujilinganisha na watoto wa kike,wanaishi na haya mawazo ya kura veto na makongamano kwamba kusaidiana katika majukumu. Hivi tangu lini mwanamke akafanana sawa kimajukumu na sisi ? Kwanza tu kimaumbile hatufanani.

Mwanamke kiasili ni wakukaa nyumbani na kulea watoto,asubiri aletewe huu ndiyo usawa na wale waote wanao enda kinyume na hii kanuni habari wanayo,wanaugulia maumivu kimya kimya.

Nipo ....
Kwa mtazamo wako tu kama mwanamke ni mama wa nyumbani tu itakuwa tumefunga mjadala huu. Wapo wanawake walioelimika na ni mama wa nyumbani kwa sababu ni matkwa ya waume zao.

Madhali wote wameridhia na majukumu ya pande zote yanatekelezwa then hakuna shida mkuu.

Kwa uelewa wangu mimi mwanamke aliyeelimika ni yule ambaye ana elimu ya juu kumaanisha chuo n.k aidha ana bachelor degree au masterdegree n.k

Hilo kuhusu mtazamo wa mwanaume unaweza kuchangia ww!
 
Mbona ww ndio unalalama hapa akilalamika bwana wako huko unatujumuisha wote

Nowadays kujifanya kazi,usomi hata papunch mnatupangia ratiba ya kuila
 
Point nzuri.

So bibie wewe unatoa mchango kwa asilimia 50 katika Familia yako na mahusiano yako? Naomba uwape elimu hiyo wanawake wote humu JF kuwa mambo ni 50/50 hivyo wachukue mfano kwako na wasione ni wajibu/jukumu la mwanaume peke yake kutimiza mahitaji yote katika famikia/mahusiano.
Ndio nafanya hivo.Na inatusaidia wote economically tunaepuka kuelemea upande mmoja kwasababu tunasaidiana.Lakini ndio inabidi na mwenzangu asielemeze majukumu yote upande wangu ikija kwenye kazi za nyumbani mfano na malezi.Kila kitu inabidi tusaidiane...ikiwa mimi sina nafasi ya kupika yeye anapika,nikiwa kazini ye yupo nyumbani inabidi alee...nadhani umenielewa!
 
Mada kama hiz zinawapa sana kiburi wanawake

Ok ukweli mimi ni muumin wa mfumo dume km unavyouita familia yangu imenyooka heshima ndani ya familia imenyooka hamna kubishabisha ujinga nikishasema nimesema km baba watoto na mama yao lazima wafate
 
Mbona ww ndio unalalama hapa akilalamika bwana wako huko unatujumuisha wote

Nowadays kujifanya kazi,usomi hata papunch mnatupangia ratiba ya kuila
Mke akipanga muda wa kuliwa mbususus huyo sii unamuacha tuu akae na tundu lake wee unaenda kuchukuwa mwengine
 
Wanaume wa sasa mna matatizo gani haswa maana sielewi tatizo lenu ni kwamba hamtaki mabadiliko au akili zimeelemea kwenye mfumo dume au ni nini hasa?Hamna lilo la kheri kwenu,wanaume hamuishi malalamiko mnaongea hata kuwazidi wanawake, maana najua mwanamke ni itikadi yake kupenda kuongea.

Wanaume nyinyi wa karne hii mnataka mtu kama bibi zetu(kitabia na anavyojiweka) na wakati huohuo mnataka mwanamke aliyeelimika,mpenda maendeleo,mchapa kazi n.k ili musaidiane majukumu.
Mnasahau kama bibi zetu jukumu lake kubwa lilikuwa kujenga familia.Kama mwanamke anaingiza kipato kama ww au ikiwezekana kukuzidi wewe mwanaume usitegemee upewe treatment na mwaka 47 lazima mfumo mzima wa maisha ubadilike!
Hii ni 2021 inabidi mubadilike muendane na wakati uliopo waungwana!

Ninachojiuliza hasa ni kwamba mna hofu mkiwa na mwanamke aliyeelimika atawapa changamoto nyingi kwasababu amepambazuka akili na ana upeo wa kufikiri tofauti na ambaye hana elimu?na hamtoweza kumwambia lolote tu akubali bila kutaka kujua kwanini?
Je hilo litapunguza heshima kwenu au litaondoa uanaume wenu?

Tusisahau pia wanawake haohao wachapakazi ndo wanaozaa na kujenga familia kumaanisha wanabeba mzigo mzito kuliko hata wa mwaka 47!

Tuchukulie women empowerment ni kitu chenye manufaa kwa mwanamke na mwanaume na tuache kukandamiza wanawake kwasababu wamepata sauti na kuerevuka!

Tafadhali nahitaji michango ya watu mnaojielewa.Ahsanteni na karibuni!
Wanaume wa sasa ni kina nani?

Tulivyo wakabidhi nchi, mjue familia ndio wananchi. Ni jukumu lenu wamama kulea wananchi
 
Naona wewe bado ni mgeni sana na ulimwengu wa mahusiano sababu umeandika kwa namna ya mtu ambaye hana experience yoyote juu ya maswala ya ndoa.

Nitakuuliza maswali kadhaa na ukiweza kuyajibu pengine tunaweza kuwa katika mlengo mzuri kujadili hii mada yako uliyoleta!

1. Una umri gani?! Nakuuliza umri ili nijue nazungumza na mtu ambaye amepita umbali gani katika utu uzima.

2. Unayajua mahitaji ya mwanaume anayotaka kutimiziwa na mwanamke?! Usiniambie mambo ambayo umesikia, nipe wewe personally unachojua na kama haujui (for the sake of honesty and goodwill) sema sijui nielimishe ila usije na hoja mitandaoni unazookota huko kuhusu wavulana ukiita ni wanaume.

3. Nani role model wako katika haya maisha kama mtoto wakike?! Tafadhali kama katika list ya role models au role model wako hawapo katika ndoa usihangaike kujibu hili swali sababu hatutakuwa na cha kujadili kama role model wako mwenyewe ni kipofu kama wewe.

4. Ni nani aliyekuambia wanaume wanataka mwanamke mjinga au anaepelekwa kama bendera?! So kwa assumption yako ni kuwa tunawatafutia watoto wetu mama ndezi?! (una mengi ya kujifunza kuhusu tofauti ya mke bora na mwanamke wa kawaida wa kisasa)

5. Kama assumption yako ni kuwa wanaume wanalalamika (of which sina uhakika kama huwa unaelewa kinachokemewa au kupigwa kelele na hao unaoita wanaume), je umeshawahi jitathimini wewe kama binti mdogo unaeuingia utu uzima mzito kwa kasi, umejitafakari juu ya uwezo wako na mapungufu yako kwa marejeo ya uhalisia wa namna mwanamke anatakiwa kuwa, yaani kwa mfano wakisema mke bora anatakiwa kuwa na vigezo 50, wewe una vingapi na je unaweza viainisha hapa tuone namna ulivyobora?!

6. Hebu tukiacha tu mijadala na mabishano ya mtandaoni baina ya wavulana na wasichana. Wewe umejipanga vipi kuingia taasisi ndoa kwa muktadha wa mchango gani utatoa kwa mumeo mtarajiwa?! Je huyu mume atapata offer gani ya thamani kutoka kwako tukiacha kumpa mwili wako kwaajiri ya kugegedana, una kipi kipya ambacho upo taayari kutoa bila manung'uniko ya kisichana.

7. Je, ndoa kwako ni jambo takatifu na muhimu?! Kama ni ndio hebu tuambie umejiandaaje kuheshimu hilo agano na maandalizi yako kuliingia, na kama hapana, hebu tueleze ni kwann tena unajihusisha na majadiliano ya mahusiano ile hali ndoa kwako si jambo muhimu.

Jibu hayo kwanza then nikuhoji zaidi.
Umeandika vingi sana lakini asilimia kubwa ya ulivyogusia umevielemeza personally kwangu which is wrong!Sipo kwenye personal interview.Kama unataka kunijua kwa undani nitafute kwa wakati wako!

1. Umri wangu hauhusiani na hii mada.Jitahidi siku zote uheshimu watu wa rika zote.Ukiheshimu na wewe utaheshimiwa.Mimi ni veteran jamiiforums kuliko ww ,nifatilie kwenye uzi zangu tofauti ujifunze kitu acha kukurupuka,sipo hapa kuandika porojo tu!

2. Nayajua mahitaji yote wa mwanaume physically,emotionally,psychologically na spiritually.

3. Role model yangu ni mama yangu mzazi na alikuwa kwenye ndoa halali kutoka kwenye usichana wake na marehem baba mpaka alipofariki(Mungu amrehemu).

4.Mimi sio mwanamke mjinga kama ndivyo unavyoassume kwasababu nimeleta mada mezani inayoendana kinyume na utakavyo

5.Sihitaji kujitathmini au kuainisha hilo kwako najitambua mimi ni mwanamke wa aina gani na wanaonijua wanatambua ni mtu wa aina gani.

6.Mimi ni mtu ambae namsaidia mume wangu kwa kila hali na mali.Hata kwa mtazamo wa 50/50 ni kwa manufaa yake binafsi vilevile na nampunguzia mzigo na manufaa ya baadae ni kwetu zote.Maisha ni kusaidiana.
Nadhani swali la saba limejibiwa kipengele cha 6.
 
Wanaume wa sasa ni kina nani?

Tulivyo wakabidhi nchi, mjue familia ndio wananchi. Ni jukumu lenu wamama kulea wananchi
Mkuu hawa walokuwa so active kwenye huu uzi.Wenye kutambua majukumu yao wanajieleza na wametulia.

Nikupe heshima yako kwanza!
Shikamoo babu @aspirin long time no see!
 
Michell Obama ni mwanamke mwenye akili sana na elimu ya kutosha alishawai kuhojiwa akasema japo ikulu kuna wafanyakazi wengi ila ni lazma ampikie na kufanya kazi zote za mama kwa wanawe na za mke kwa mumewe. Kuna tahira mmoja uku tanzania ana ka kazi kanampa kiburi anajikuta aneshalingana na mumewe .

Ndo maana kuna wake wakutumika na wanawake wakuoa . Sio kila mwanamke anafaa kuwa mke au mama .
 
Mbona ww ndio unalalama hapa akilalamika bwana wako huko unatujumuisha wote

Nowadays kujifanya kazi,usomi hata papunch mnatupangia ratiba ya kuila
Suala hili halihusiani na unayoyaongelea.Kama unapangiwa ratiba nakupa pole!
 
aisee bora ufuge ng'ombe kuliko kuwa na wewe
yaani hadi kubeba mimba unaona unaonewa
50/50 bado unasema unamuhudumia mume
hivi unaelewa unachoandika
moja ya madhara ya demokrasia ni haya
unaandika pumba kisha unatetea mashudu
Hivi unatambua tangia nimefungua huu uzi michango yako haijaleta maslahi yoyote! Kama huna la maana lakusema tafadhali kaa upande!Nakielewa nilichoandika,ni ww ndio usiyeelewa!
 
Michell Obama ni mwanamke mwenye akili sana na elimu ya kutosha alishawai kuhojiwa akasema japo ikulu kuna wafanyakazi wengi ila ni lazma ampikie na kufanya kazi zote za mama kwa wanawe na za mke kwa mumewe. Kuna tahira mmoja uku tanzania ana ka kazi kanampa kiburi anajikuta aneshalingana na mumewe .

Ndo maana kuna wake wakutumika na wanawake wakuoa . Sio kila mwanamke anafaa kuwa mke au mama .
Hujaelewa mada tatizo sio kukataa kumpikia mume au kutimiza wajibu kama mke na mwanamke.Ni kusaidiana,hivi ww kumsaidia mkeo unaona ni shida sana kwahio umeoa mke au housegirl?
 
Wanaume wa sasa mna matatizo gani haswa maana sielewi tatizo lenu ni kwamba hamtaki mabadiliko au akili zimeelemea kwenye mfumo dume au ni nini hasa?Hamna lilo la kheri kwenu,wanaume hamuishi malalamiko mnaongea hata kuwazidi wanawake, maana najua mwanamke ni itikadi yake kupenda kuongea.

Wanaume nyinyi wa karne hii mnataka mtu kama bibi zetu(kitabia na anavyojiweka) na wakati huohuo mnataka mwanamke aliyeelimika,mpenda maendeleo,mchapa kazi n.k ili musaidiane majukumu.
Mnasahau kama bibi zetu jukumu lake kubwa lilikuwa kujenga familia.Kama mwanamke anaingiza kipato kama ww au ikiwezekana kukuzidi wewe mwanaume usitegemee upewe treatment na mwaka 47 lazima mfumo mzima wa maisha ubadilike!
Hii ni 2021 inabidi mubadilike muendane na wakati uliopo waungwana!

Ninachojiuliza hasa ni kwamba mna hofu mkiwa na mwanamke aliyeelimika atawapa changamoto nyingi kwasababu amepambazuka akili na ana upeo wa kufikiri tofauti na ambaye hana elimu?na hamtoweza kumwambia lolote tu akubali bila kutaka kujua kwanini?
Je hilo litapunguza heshima kwenu au litaondoa uanaume wenu?

Tusisahau pia wanawake haohao wachapakazi ndo wanaozaa na kujenga familia kumaanisha wanabeba mzigo mzito kuliko hata wa mwaka 47!

Tuchukulie women empowerment ni kitu chenye manufaa kwa mwanamke na mwanaume na tuache kukandamiza wanawake kwasababu wamepata sauti na kuerevuka!

Tafadhali nahitaji michango ya watu mnaojielewa.Ahsanteni na karibuni!
Nyakati za ujima na hadaa zinatoweka kwa kasi, na uhalisia wa maisha unajizihirisha, Wanawake walizoe kupora na kuchukua pesa na mali za bure kwa wanaume, na Wanaume walijijengea mawazo kuwa kuwapa manawake pesa au wakiporwa mali wananyamaza, Sasa wameamka na kuanza kusema wanayokumbana nayo.huo ni mwanzo tu, wanafunguka mengi na mengi yatajitokeza na kubadilisha mfumo mzima wa maisha.
 
Hujaelewa mada tatizo sio kukataa kumpikia mume au kutimiza wajibu kama mke na mwanamke.Ni kusaidiana,hivi ww kumsaidia mkeo unaona ni shida sana kwahio umeoa mke au housegirl?
Kumsaidia mke kufanya jambo gani . Mimi kama baba nahakikisha watoto wangu wanasoma, wanapata chakula , wanatibiwa wanapoumwa . Unataka nianze kudeki na kuosha vyombo ndo ziwe haki sawa . Yaani mwamamke akiwa hana kazi nyumba inaamani bado ila mwanaume utetereke tu kiuchumi au ufukuzwe kazi ndoa inaweza kuvunjika kabisa kama mtu anaishi na mwanamke wa type yako.

Tofautisha wewe kuchangia uchumi wa familia au kumzidi mumeo kipato kama sehemu ya wewe kuonekana mwanamke mwenye dhamani.

Kuna mwanamke hana elimu kubwa wala kazi ila dhamani yake ni kubwa kuliko mwenye elimu kubwa na kazi . Ubora wa mwanamke anayekitambua haupimwi kwa ivyo ulivyovisema
 
50/50 katika muktadha gani, maana sijaelewa point ya kuwa nusu kwa nusu. Kama mtu ana kipato kizuri why ahangaike na pesa ya mkewe.

Na kama mwanamke amepata kazi nzuri na kipato kikubwa kumshinda mume wake, why aanze kutaka kuomba kwa mumewe ampatie si asimamie tu gharama na kuendelea kuwa mke kwa mumewe?!

Mbona sisi wanaume tunalipa bili zote na hatuachi kuwa mume kwa wakd zetu?!

Nadhani mabinti wa kisasa mpo busy kuprove kuwa mnaweza kuwa kama wanaume kiasi kwamba mnajisahau kujifunza uanamke. Matokeo mnafika umri mkubwa na kujua hamuwezi kuwa wanaume sababu mliumbwa wanawake na pia hamuyawezi majukumu yenu ya kike sababu kutokea umri mdogo hadi mnakomaa jamii imewajaza ujinga kuwa ninyi na wanaume ni sawa, something which is biologically, scientifically, economically and politically impossible and not true.
Nadhani ww ndio hujui ndoa na hata majukumu ya wana ndoa.Ndoa ni mkataba wa kuwa pamoja katika kila hali na kusaidiana .Its unlogic kwamba kwasababu upande mmoja una kipato kikubwa basi ndo ubebe majukumu yote?ikiwa hivo then benefits zote zinaangukia upande mwengine.
For the sake of mens ego / pride na jinsi malezi yalivyokuwa kwa wanaume kubeba majukumu yote ni kawaida but it doesnt meant thats the only formula to the equation.
Fikiria kama mnasaidiana na mnaweka akiba kukiwa na economic complication baadae hio akiba ni suluhu kwa wote.Tatizo mmeshakaririshwa vitu so ni ngumu kuelewa hili hilo nimelitambua so far.
 
Back
Top Bottom