Mwanamke anakandamizwa wapi jamani! Hamna mwanaume ambaye atashindwa kumlisha na kumvisha mwanamke wa kawaida katika misingi ya asili tu ya maisha!
Ila wanawake wa kizazi cha sasa wako overcomplicated. Tamaa mbele kila kitu kismpite imefikia stage ni gharama sana kuwa na mwanamke wa kudumu kuliko kuwa na mahawara! Unapoonekana kushindwa hayo mahitaji yake ya gharama kama kitu gani sijui ndio ngonjera za tafuta helaaaa...tafteni hela muache kulia lia ndipo zinaanzia. Demu anataka fashion zote za nywele mapochi na nguo, Iphone12 pro max umpe, anatamani crown athlete umpe na kumjazia mafuta! Haya maisha ya kutapanya mali kiasi hiki sio mepesi kwa vijana wengi wa rika langu! Hapo yeye anafanya kazi MDH kwa mfano ana mshahara 2M+ ila anataka wewe mwenye kipato cha laki 7 u toil kumfanyia yote!
Hamna mwanaume atashindwa kufanya kazi kumlisha na kumvisha mwanamke kiasili maana hayo mawili sio gharama ila overcomplications za kujifanya uzungu mwingi ndio kinachotushinda wengi!
Tunapoamua kujiondoa kwenye cycle ya wanawake wa tamaa tamaa hivi msituambie tunakimbia majukumu sababu hata babu zetu hawakupitia hizi changamoto!