Sina cha kuongeza wenye mapungufu wanajijua, wakiamua kujiaminisha hawana, kimpango wao. Wakiamisha lawama, inawasaidia kidogo lkn haiondoi tatizo, wakiamua kufuata ushauri wa watu humu ndani bado ni uamuzi wao.
Lkn kitu kingine labda ambacho hakijasemwa ni kuwa wazi na kushare tatizo lako kama unalo na mwenzi wako kuliko kusema ngoja nikajaribu kungine (nje) ambapo ndipo mnapojiaibisha zaidi; kwani kuna uwezekano mkubwa wakawatangaza na kuonekana kituko. Mkeo hawezi kutoa mapungufu yenu nje, lkn hawara will be happy kusema jinsi gani ulivyo na kwamba anachopata toka kwako ni pesa tu.
Mwisho, wewe mwanaume unajijua wewe tu; hivyo jisemee wewe. Mimi mwanamke ninaweza wajua wanaume hata 7, hivyo naweza semea wanaume. Lkn pia as mwanamke najijua mimi tu na hivyo naweza with confidence jisemea mwenyewe, na wewe mwanaume unatujua say wanawake 6 na hivyo unaweza kutusemea au kutucompare wanawake.