Kwanini wanawake asilimia kubwa huwa hawanuki midomo?

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,659
Wakuu,

Kwa umri huu wa utu uzima wangu nimeshuhudia kuona wanaume ndio wanaoongoza kwa kunuka midomo. Asilimia kubwa ya wanawake hawanuki midomo. Mimi si mtaalamu wa mambo ya afya lakini ningependa kujua sababu.

Asanteni sana!
 
Tunapiga mswaki vizuri na dawa ya meno na tunajali na kuthamini vinywa vyetu
 
hiyo tafiti uliifanyaje mkuu

Tafiti ndio hiyo. Umri wangu unatosha kuwa ndio kipimo cha population sample yaani watu niliokutana nao wanatosha sana kupata sample ya kufanya huo utafiti.
 
wanaume wengi kupiga mswaki ni shida

Tofautisheni kunuka mdomo kwa kutopiga mswaki na kunuka mdomo kunakosababishwa na nature ya maumbile. Maumbike ya wanawake si ya kunuka mdomo kama wanaume.
 
Wakuu kwa umri huu wa utu uzima wangu nimeshuhudia kuona wanaume ndio wanaoongoza kwa kunuka midomo. Asilimia kubwa ya wanawake hawanuki midomo. Mimi si mtaalamu wa mambo ya afya lakini ningependa kujua sababu. Asanteni sana!
Hivi kinachonuka ni mdomo au ni kinywa? Ufafanuzi tafadhari FaizaFoxy.
 
Last edited by a moderator:
Mdomo ndio kinywa wakuu. Tuendelee kuchangia....
 
hata wanawake huwa wananuka sema huwa unashindwa kuisikia harufu kutokana na homoni inayoitwa libido, hii ikipanda hata mbuzi unaweza kusikia ananukia pafyum!

Ahahaaa
Mkuu ww kiboko
Yaani beberu anuke pafyum?
 
Inawezekana ni kwa sababu idadi kubwa ya wanaume si watu wa kujali sana hasa hivi vitu vidogo vidogo kama usafi wa kinywa n.k...
 
Inawezekana ni kwa sababu idadi kubwa ya wanaume si watu wa kujali sana hasa hivi vitu vidogo vidogo kama usafi wa kinywa n.k...

Kunuka ninakokuzungumzia mimi ni kunuka kwa hali ya kimaumbile. Suala la usafi wa kinywa is not applicable here.
 
Jaribu kuwasogelea wanawake wambea wanaovunja nyumba za watu ndo utajua kuwa wanaonuka midomo wapo.
 
Tatizo la kinywa kutoa harufu mbaya tunaliita kwa kitaalamu "HALITOSIS." Kwa summary tu, Kuna vichocheo vingi vinavyosababisha kinywa kutoa harufu mbaya, na hapa utaweza kujua ni gender ipi ni more prone:

1. Aina ya vyakula tunavyokula ... Women are more selective kwenye msosi kuliko wanaume. Wanaume hawabagui.
2. Life style habits eg. pombe humo & sigara nk..
3. Of course usafi wa kinywa usioridhisha ... Tofautisha men vs women
4. Kuna baadhi ya magonjwa yanaweza kupelekea kinywa kutoa harufu mbaya (hii nafikiri haibagui jinsia).

Otherwise google neno "halitosis" utapata shule ya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…