Mahakama imezuia kazi zote za chadema, hiyo nayo inahitaji watu waumizane? Tz ni yetu sote, tufuate sheria ili tunufaike wote. Huwezi kujitokeza hadharani na kusema huwaogopi polisi, kauli kama hizo ni za kijinga kabisa, yaani unataka kusema polisi hawana maana kwako unaweza kuishi bila polisi. Matamshi kama hayo yanasababisha maumivu kwa watu wasiokuwa na hatia. Hivi ni polisi gani huyo anakubali kubezwa na raia anaemlinda usiku na mchana?. Kumbukeni jeshi la polisi ni kama mbwa lipo kwa mujibu wa sheria, na linatii mamlaka na amri kutoka kwa wamiliki wao.