Nikueleweshe, hii tunaita sijda au zabiba shehe wangu, na unaonekana wewe sio muislamu hufahamu lolote na acha nikueleze.
Sijda au mtende, sio kipimo cha ucha mungu au ubora wa ibada kwa waislamu, hiyo alama wanayo waislamu wachache kwa walio wengi, kakae msikitini uangalie, mimi naona wengi walionayo ni wanaume wenye ngozi nyepesi, na ambao mara kwa mara hupata msuguano wa ngozi na ardhi au zulia.
Kwa wanawake sasa, ni nadra kuona kwasababu, ngozi yao ni laini zaidi, na haiathiriki sana na msuguano.
Wanawake kusujudu kwao ni kwa upole, na sehemu kubwa ya mwili huwa tulivu, kwahyo ule msuguano huwa mdogo.
Swala la mwisho, ni yale mazoea ya kutumia kitambaa, kitenge au hijabu, tofauti na wanaume huende bila kofia wala kujifunika.
Narudia tena sijda sio kipimo cha ucha mungu shehe.
Ila jambo jingine unapata nguvu wapi kuhoji kwa kulinganisha mwanamke na mwanaume wa kiislamu kwenye kusali, are you mad? Embu acheni hivi vitu.