Kwanini wanawake wengi wa kizazi cha sasa hawaolewi?

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
2,026
Reaction score
4,450
Hello WanaJf

Bibi yangu Rukia kuna siku aliniuliza Mjukuu wangu unajua kwa nini wanawake wengi wa kizazi cha sasa hawaolewi?

Mimi: Hapana Bibi

Bibi: Hii ndiyo sababu mjukuu wangu "Kuonja onja umeshashiba".

Mimi: Inamaana gani bibi?

Bibi: Nikimaanisha kwamba mambo yanayopatikana kwenye ndoa wanaume wa kizazi cha sasa wanayapata kabla ya kwenye ndoa . Kama vile kufuliwa, kupikiwa na mambo mengine ya ndani ya ndoa. Hii inapelekea kwa kiasi kikubwa kupoteza hamu ya ndoa na zana nzima ya ndoa kati ya wahusika hao wawili na kusababisha kushiba kwa wanaume kunakotokana na kuonja onja na kupelekea kushiba.

HUU NI MTAZAMO WA BIBI YANGU, JE WEWE UNAMTAZAMO GANI KUHUSIANA NA HILI?
 
JE WEWE UNAMTAZAMO GANI KUHUSIANA NA HILI?
Points ni zile zile

1.Hawaolewi kwasababu wanaume hawataki majukumu ya ndoa
2.Uhaba wa wanaume huku jinsia ya kiume na wavulana kuwa nyingi
3.Kujirahisisha na uhuni wa wanawake ambao unapelekea kuogopesha waowaji
4.Uhuni wa wanaume unaopelekea kupenda kuchovya chovya kuliko kuamua kutulia na ndoa

5.Kutishana,waliopo ndoani wanatisha sana ambao bado hawajaingia ndoani...usaliti

Nimesahau udomo zege....teh!
 
Nakazia point namba 1,2 na 5
 
Ahsante sana kwa maoni mazuri.
 
umemaliza kila kitu
 
Bibi yako ana akili, kuliona hilo..

Pili, ni changamoto zinazowakabili vijana wa leo. AJIRA na HARUSI

Ajira imekuwa ngumu kwa vijana iwe kujiajiri au kuajiriwa ili kukidhi mahitaji ya kifamilia, hivyo kuamua kusubiri MITANO TENA

Harusi nazo zimetisha vijana wengi.. wadada na ndugu wanategemea harusi ya kukata na shoka bila kuzingatia kuwa shoka halinyanyuki bila nguvu(pesa)
 
Pia kuna wimbi la feminists ambao badala ya kupigania haki za wanawake.

Wao wako busy kutengeneza uadui na ushindani kati ya wanawake na wanaume.
 
Bibi yako ana akili, kuliona hilo..

Pili, ni changamoto zinazowakabili vijana wa leo. AJIRA na HARUSI

Ajira imekuwa ngumu kwa vijana iwe kujiajiri au kuajiriwa ili kukidhi mahitaji ya kifamilia, hivyo kuamua kusubiri MITANO TENA

Harusi nazo zimetisha vijana wengi.. wadada na ndugu wanategemea harusi ya kukata na shoka bila kuzingatia kuwa shoka halinyanyuki bila nguvu(pesa)
Nimekuelewa mkuu, lakini mbona wazee wetu walioa na bila kuwa na ajira maalumu?
 
Point ya msingi sana

Mie huwa naona target ya feminists ni kushindana na wanaume...huwa sioni kama wapo katika kujenga
Feminists wanataka haki sawa kwa wote kati ya wanaume na wanawake. Kuondoa kabisa mfumo dume katika kila sekta zinazooperate dunia hii.
 
Point ya msingi sana

Mie huwa naona target ya feminists ni kushindana na wanaume...huwa sioni kama wapo katika kujenga
Hii dhana ya feminism binafsi huwa naona haijaeleweka kwa watu wengi.

Unamkuta mtu wanaume sijui walinfanya nini, hana mahusiano nao mazuri basi anatumia kichaka cha feminism kujenga uadui kati ya mwanaume na mwanamke.

Sasa wasichana wakiwasikikiza hawa ni ngumu sana kuishi kwenye ndoa.

Kwasababu badala ya ndoa kuwa sehemu ya kushirikiana, inakuwa sehemu ya kuoneshana nani zaidi, au nani mwamba.
 
Back
Top Bottom