The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Hawa ni wanawake wenye kiwango kikubwa cha elimu, fedha, umaarufu au hata madaraka katika jamii. Hoja ya wanaume wenye mawazo haya ni ugumu wa kuwaongoza wanawake wanaowazidi.
“Mwanawake akipata kitu anakuwa jeuri sana. Hawezi kukusikiliza tena na atataka awe huru kufanya mambo yake bila kuingiliwa.” pia humfanya mwanamke asiwe na utayari wa kuwa chini ya utawala wa mwanaume. “Huwezi kuishi na mwanamke anayejiona yuko juu yako na ukabaki salama. Hatokuwa tayari kukupa nafasi ya kuwa na sauti kwenye nyumba.”
Hitaji kubwa la wanaume wengi ni mamlaka. Wanaume wanapoingia kwenye uhusiano na mwanamke wanakuwa na shauku ya kuwa na sauti inayosikika bayana kukidhi dhana ya kichwa cha familia. Ili sauti hii iweze kusikika bara bara uwezo wa kifedha, kielimu, kimadaraka na hata umaarufu unakuwa na nafasi yake.
Kwa maana hiyo inapotokea mwanamke ameshindwa kuwa chini ya mamlaka yake, mwanaume huanza kujisikia hayuko salama.