Thad
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 13,380
- 31,566
Sio kweli, sijaja hapa kuomba ushauri wa mtu kwani maamuzi nilishayafanya mwenyeweMbona unamshauri vibaya?? Mwenzio amelileta hapa ili kusudi atokee mtu amwambie arudi fasta.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kweli, sijaja hapa kuomba ushauri wa mtu kwani maamuzi nilishayafanya mwenyeweMbona unamshauri vibaya?? Mwenzio amelileta hapa ili kusudi atokee mtu amwambie arudi fasta.
Hujamwelewa ThadMbona unamshauri vibaya?? Mwenzio amelileta hapa ili kusudi atokee mtu amwambie arudi fasta.
Asante, machozi yalishaisha. Sasa hivi nacheka kihutu tuFikiri, ati mwenzie aliyeipindua serekali yake kaolewa na aliyemkimbia ati kazaa mtoto wa kiarabu.
Mpaka atamanishe mwarabu wadhani ni kapuku?? Pole sana, ulishazidiwa ki umbo na sura ukaachwa solemba hapo. Lia kimya kimya kwani ni wewe ulimpeleka mwenzio aliyekuzidi kila nyanja. Ugulia maumivu tu lakini jamaa kama alikurudia ni kukumbukia kiporo tu kabla hakija chacha.
Umejitahidi kuandika story, katika hali ya kawaida tena kwa binadamu wa kike ni ngumu sana kwenda kushuhudia MTU aliyekuwa akimpenda anafunga ndoa hafu asimame kwa ujasiri kabisa bila kuzimia, au kulia kwa machozi mengi sana, mwanamke wa hivyo kama yupo basi anauwezo wa kufanya hata tukio la mauwajiTulipendana sana, tukapanga mipango kedekede ya maisha yetu ya baadae na kuahidiana kila aina ya ahadi tamu tamu lakini yote hayo hakuyajali na kwa kuwa moyo wa mtu ni kichaka sikuweza kung'amua lolote mpaka siku ile ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu!
Kama ilivyoada aliniaga kwa mabusu moto moto, nilijua ni moja kati ya safari zake za kibiashara, nilimwombea kila la heri huko aendako. Na safari ikaanza na kuniacha mwenye majonzi kwani nilijua nitamkosa kwa muda usiopungua wiki moja, kilichoniumiza zaidi ni kujua fika kuwa baada ya masaa yapatayo 12 nisingeweza kuwasiliana naye hata kwa simu maana aliniambia kuwa huko aendako ni maporini kusiko na network. Nilimwamini pasipo shaka. Naam baada ya masaa 12 sikuweza tena kumpata kwenye simu zake zote ila haikunipa shida kwani nililijua hilo.
Siku tatu baada ya kuondoka kwake, mida ya jioni nilishtushwa sana baada ya kupigiwa simu na rafiki yangu mmoja na kunipa pole kabla ya kuniuliza imekuwaje? Badala ya kumjibu nilimwuliza kwa wasiwasi mwingi, ananipa pole ya nini? Na imekuwaje nini? Jibu lake ndilo lilinifanya mpaka leo nisiisahau hiyo siku! Alicheka kwa kejeli kisha akanijibu ina maana hujui kama fulani(alitajajina la mpenzi wangu aliyesafiri siku 3 zilizopita) kanilipia mahali leo na kesho tunaenda kuandikisha ndoa kanisani? Sikusikia kingine alichokiongea bali nakumbuka mwangwi wa maneno yale yaliendelea kujirudia masikioni mwangu kwa masaa kadhaa kabla ya kulala (sina uhakika kama nililala au nilizimia)
Nilipoamka nilikuta simu ikiwa chini huku kioo cha simu kikiwa kimevunjika na betri ya simu imedondokea upande wake, nikajua kuwa baada ya taarifa zile nilidondosha simu pasipo kujijua.
Baada ya wiki moja mpenzi wangu alirudi kama alivyoniahidi akiwa na zawadi lukuki, nilizipokea na nilijaribu kuficha hali niliyokuwa nayo lakini aligundua kuwa sikuwa sawa akaniuliza nina tatizo gani nikamwambia ninaumwa na nimeshauriwa na daktari kupumzika muda mwingi. Alinionea huruma akataka alale kwangu ila nikamkatalia, nikamwambia nahitaji kuwa mwenyewe ili niweze kutumia muda mwingi kwa kulala. Alinielewa na akaondoka.
Sikuonana naye tena kwani kesho yake asubuhi na mapema nilisafiri kwenda mkoa mwingine na nilibadilisha namba ya simu. Tulionana tena siku ya harusi yake na rafiki yangu kipenzi, ilinibidi kwenda kanisani kushuhudia ndoa yao kama nilivyoshauriwa na mwanasaikolojia wangu. Aliniambia hiyo itanisaidia kuamini kuwa yule jamaa si wangu tena. Wakati wanatoka kanisani baada ya ndoa, nilihakikisha maharusi hao tunaonana ana kwa ana, kisha nikatokomea.
Haikuwa rahisi hata kidogo kuendelea na maisha ila kwa msaada wa ushauri wa mwanasaikolojia niliweza kuendelea na maisha japo ilinibidi kubadilisha mtindo wangu wa maisha.
Miezi 6 baada ya ndoa nilipata taarifa kuwa wanandoa wale walipata mtoto wa kiume, ila mtoto mwenyewe ni mwarabu wakati wazazi wake ni Wandengereko wenzangu. Hahahahaaaaa....nacheka kama mazuri mie. Wambea ikawa kutwa kucha wananilitea habari, ile ndoa si ndoa tena bali imegeuka ndoano baada ya kuzaliwa mtoto wa kiarabu. Nikasema pole yao, wavumilie tu maana kitanda hakizai haramu.
Juzi jamaa kanifuata anasema nimsamehe, yalopita si ndwele tugange yajayo. Ameachana na mkewe (rafiki yangu) kama niko tayari tukafunge ndoa ya bomani, niwe mkewe. Ametambua kuwa alifanya kosa kubwa sana kuniacha. Nimemwambia nilishamsamehe kitambo sina kinyongo nae hata kidogo ila "PEMA NI PEMA USIPOPEMA, UKIPEMA SIO PEMA TENA"!
Nishamsamehe ila sitarudiana nayeMalipo ni hapa hapa duniani.Usimsamehe huyo wala acha ayaoge maovu aliyopanda mwenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Over my dead body!Ninacho mshukuru Mungu kawapa Moyo wa kusame wanawake ...hapo jamaa akikaza fresh atakubaliwa tu...huo ni mkwara tu ....
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasaikolojia nawaheshimu sana, alinijenga kiasi cha kusimama hivyoUmejitahidi kuandika story, katika hali ya kawaida tena kwa binadamu wa kike ni ngumu sana kwenda kushuhudia MTU aliyekuwa akimpenda anafunga ndoa hafu asimame kwa ujasiri kabisa bila kuzimia, au kulia kwa machozi mengi sana, mwanamke wa hivyo kama yupo basi anauwezo wa kufanya hata tukio la mauwaji
Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah usimrudie though wanawake mko so weak tukimwwga chozi na mahali mezani ynakuta unalainika.ha haaaa.Nishamsamehe ila sitarudiana naye
Hilo au anakufwata maana zimembana.Kwamba alioa kwasababu ya nyege?
Asante dear!Pole sana bestie,ama kweli malipo ni hapahapa duniani na hayacheleweshwi.
Msamehe na uendelee na maisha yako tu maana waweza rudi kwake akarudia yaleyale ya mara ya kwanza
Hakika aliimbaChristian Bella
Kwasasa hata asijali, azipeleke kwa mkewe wa ndoaHilo au anakufwata maana zimembana.
Hata alie machozi ya damu, hawezi kunifanya nile matapishi.Yeah usimrudie though wanawake mko so weak tukimwwga chozi na mahali mezani ynakuta unalainika.ha haaaa.
Mungu akusaidie dada yangu.chozi lenu huwa sipendi kuliona kabsa sema ndio vile mens hatusomeki saa zingine
Sent using Jamii Forums mobile app