Thad
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 13,380
- 31,566
Katu siwezi kujiroga kufanya huo upuuziUsije thubutu rudia tapishi hilo...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katu siwezi kujiroga kufanya huo upuuziUsije thubutu rudia tapishi hilo...
Hahahahaaaa...!Fursa hii ngoja niiwahi
Kumuumiza mwenzio hivyo halafu unasema ni wimbo?[emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli kabisa haya matukio ni mengi.Hivi visa vya marafiki kuchukuliana wachumba vipo sana tu, mi tu najua matukio manne, ukute lako ni mojawapo
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwambie wewe maana nikisema mimi ananiona sina maanaKumuumiza mwenzio hivyo halafu unasema ni wimbo?[emoji23][emoji23][emoji23]
Mwambie wewe maana nikisema mimi ananiona sina maana
Naomba uwe wakili wangu kwa kweli amininyanyasaSijui tumfungulie kesi ya unyanyasaji wa hisia?maana haiwezekani akufanyie hivi
Naomba uwe wakili wangu kwa kweli amininyanyasa
Nimekupenda mno kwa methali yako. Shika msimamo na utafanikisha mume bora. Hakufai alikuwa anakuchanganya na huyo rafiki yako. Mahusiano yao yalikuwa ya muda mrefu mno hivyo siku uliyopigiwa simu ni hitimisho tu. Acha atesekeTulipendana sana, tukapanga mipango kedekede ya maisha yetu ya baadae na kuahidiana kila aina ya ahadi tamu tamu lakini yote hayo hakuyajali na kwa kuwa moyo wa mtu ni kichaka sikuweza kung'amua lolote mpaka siku ile ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu!
Kama ilivyoada aliniaga kwa mabusu moto moto, nilijua ni moja kati ya safari zake za kibiashara, nilimwombea kila la heri huko aendako. Na safari ikaanza na kuniacha mwenye majonzi kwani nilijua nitamkosa kwa muda usiopungua wiki moja, kilichoniumiza zaidi ni kujua fika kuwa baada ya masaa yapatayo 12 nisingeweza kuwasiliana naye hata kwa simu maana aliniambia kuwa huko aendako ni maporini kusiko na network. Nilimwamini pasipo shaka. Naam baada ya masaa 12 sikuweza tena kumpata kwenye simu zake zote ila haikunipa shida kwani nililijua hilo.
Siku tatu baada ya kuondoka kwake, mida ya jioni nilishtushwa sana baada ya kupigiwa simu na rafiki yangu mmoja na kunipa pole kabla ya kuniuliza imekuwaje? Badala ya kumjibu nilimwuliza kwa wasiwasi mwingi, ananipa pole ya nini? Na imekuwaje nini? Jibu lake ndilo lilinifanya mpaka leo nisiisahau hiyo siku! Alicheka kwa kejeli kisha akanijibu ina maana hujui kama fulani(alitajajina la mpenzi wangu aliyesafiri siku 3 zilizopita) kanilipia mahali leo na kesho tunaenda kuandikisha ndoa kanisani? Sikusikia kingine alichokiongea bali nakumbuka mwangwi wa maneno yale yaliendelea kujirudia masikioni mwangu kwa masaa kadhaa kabla ya kulala (sina uhakika kama nililala au nilizimia)
Nilipoamka nilikuta simu ikiwa chini huku kioo cha simu kikiwa kimevunjika na betri ya simu imedondokea upande wake, nikajua kuwa baada ya taarifa zile nilidondosha simu pasipo kujijua.
Baada ya wiki moja mpenzi wangu alirudi kama alivyoniahidi akiwa na zawadi lukuki, nilizipokea na nilijaribu kuficha hali niliyokuwa nayo lakini aligundua kuwa sikuwa sawa akaniuliza nina tatizo gani nikamwambia ninaumwa na nimeshauriwa na daktari kupumzika muda mwingi. Alinionea huruma akataka alale kwangu ila nikamkatalia, nikamwambia nahitaji kuwa mwenyewe ili niweze kutumia muda mwingi kwa kulala. Alinielewa na akaondoka.
Sikuonana naye tena kwani kesho yake asubuhi na mapema nilisafiri kwenda mkoa mwingine na nilibadilisha namba ya simu. Tulionana tena siku ya harusi yake na rafiki yangu kipenzi, ilinibidi kwenda kanisani kushuhudia ndoa yao kama nilivyoshauriwa na mwanasaikolojia wangu. Aliniambia hiyo itanisaidia kuamini kuwa yule jamaa si wangu tena. Wakati wanatoka kanisani baada ya ndoa, nilihakikisha maharusi hao tunaonana ana kwa ana, kisha nikatokomea.
Haikuwa rahisi hata kidogo kuendelea na maisha ila kwa msaada wa ushauri wa mwanasaikolojia niliweza kuendelea na maisha japo ilinibidi kubadilisha mtindo wangu wa maisha.
Miezi 6 baada ya ndoa nilipata taarifa kuwa wanandoa wale walipata mtoto wa kiume, ila mtoto mwenyewe ni mwarabu wakati wazazi wake ni Wandengereko wenzangu. Hahahahaaaaa....nacheka kama mazuri mie. Wambea ikawa kutwa kucha wananilitea habari, ile ndoa si ndoa tena bali imegeuka ndoano baada ya kuzaliwa mtoto wa kiarabu. Nikasema pole yao, wavumilie tu maana kitanda hakizai haramu.
Juzi jamaa kanifuata anasema nimsamehe, yalopita si ndwele tugange yajayo. Ameachana na mkewe (rafiki yangu) kama niko tayari tukafunge ndoa ya bomani, niwe mkewe. Ametambua kuwa alifanya kosa kubwa sana kuniacha. Nimemwambia nilishamsamehe kitambo sina kinyongo nae hata kidogo ila "PEMA NI PEMA USIPOPEMA, UKIPEMA SIO PEMA TENA"!
Asante. Ni kweli nilikuwa nakula nao na kucheka nao nikiamini ni wema kwangu wakati walikuwa wanafiki wakubwa. Yalishapita, nilimwachia Mungu na sasa nasonga mbele katu starudi nyumaNimekupenda mno kwa methali yako. Shika msimamo na utafanikisha mume bora. Hakufai alikuwa anakuchanganya na huyo rafiki yako. Mahusiano yao yalikuwa ya muda mrefu mno hivyo siku uliyopigiwa simu ni hitimisho tu. Acha ateseke
Mara nyingi watu hulia maramoja tu kwenye mapenzi mara ya pili umejitakia mwenyewe Thad, endelea na maisha yako dada yanguKabisa sijui kama kuna maumivu ya mapenzi yatakayonitoa chozi tena
Usije tu ukamtenda rafiki yangu kama mimi nilivyotendwa! Sitakusamehe ukimuumiza carbamazepine wangu
Hongera kwa kuelewa maana ya hiyo methaliLeo ndo nimeelewa maana ya hii methali "PEMA NI PEMA USIPOPEMA, UKIPEMA SI PEMA TENA!!"
Asante kwa ushauri murua, hakika karma haijawahi kumuacha mtu salama ni vile tu wakati mwingine tunaona kama inawachelewesha wabaya wetuMara nyingi watu hulia maramoja tu kwenye mapenzi mara ya pili umejitakia mwenyewe Thad, endelea na maisha yako dada yangu
Its a very touching and sad story, having experienced it myself to a certain lady I crazily fallen in love with.
Maajabu ni kwamba mara kadhaa(sio zote) hua ina backfire kwa yule aliyemkosea mwenzie na kumuumiza, wanaita Karma
Usije tu ukamtenda rafiki yangu kama mimi nilivyotendwa! Sitakusamehe ukimuumiza carbamazepine wangu
Tena mkosaji anapokuja kutambua kwamba alichokiachia kilikua ni dhahabu na hicho alichokikimbilia ni kipande cha chupa kisicho na thamani inakua too late, huku kaachia kule hajashika!Asante kwa ushauri murua, hakika karma haijawahi kumuacha mtu salama ni vile tu wakati mwingine tunaona kama inawachelewesha wabaya wetu