Kwanini wanyama hawafanyi mapenzi kinyume na maumbile?

Ya kwanza haina ukweli.Tupe reference.
 
Mleta uzi naona kama vile una interest na mtandao wa tigo, anyway pamoja na tafiti za kisayansi ulozotuelezea (japokuwa hatuna evidences) Mungu amekataza hiyo kitu............kumbuka Sodoma na Gomola kama wewe ni Mkristo.
 

Pole ya nini wewe??? Mimi sikatazi watu kupata elimu humu jamvini.....Ninachokataa ni kule kurudiwarudiwa kwa mada ambayo imekwishajadiliwa sana tu; tena kitaalamu. sasa unapoirudiarudia unakuwa na maana gani? Hukuelewa huko nyuma ama vipi? Halafu huu mtindo wa kugeuza title wakati kitu kinachojadiliwa ni kilekile kila siku hakupelekei mada kuonekana ni mpya..... Huo ni ujinga! Tujadili vitu vyenye maendeleo au mafundisho yanayoonekana kwa macho. Kwa nini unapojadili madhara ya ngono kinyume na maumbile unamlenga mwanamke pekee eti kwamba wakati wa kujifungua hupata balaa hili ama lile...Mbona kuna wanaume kibao mtaani wanajambajamba ovyo hamsemi??? Lengo ni kuwadhalilisha wanawake au ni nini hasa? Hoja ikishajadiliwa mara mbili tatu basi inatosha kama uko interested na hayo mambo nenda kwenye mitandao ya mambo hayo, tena iko mingi sana.....Lakini usitegemee JF utakuta tunaweka video ya watu wanafanya ngono kinyume na maumbile ili kukoleza mjadala. Hilo wazo futa kabisa!!!!
 
Mimi naona kidunia watu wanaona km normal practice lkn kidini bila kubagua hili jambo la kuenenda kinyume na maumbile ya kawaida km yalivyokusudiwa na Mungu mi nakemea kabisa na ni dhambi kubwa! Tena niwachekeshe rfk yangu mmoja muslim by dini aliniambia shetani na ujanja wake wote atakushawishi ufanye dhambi ya uzinzi lkn pindi utakapoenda tofauti km mlivyosema tigo ye ukimbia ushahidi mn anajua kbs hilo ni kosa kubwa sanaa kwa Mungu. Jamani huyo jamaa asiwabadilishe kwa lolote kwa wale ambao hamjaanza msidhubutu kabisaaa.
 
Yawezekana ikawa kweli but mi nilitaka kuwasilisha baadhi ya majibu yakitaalam kuhusu swala zima la tigo mkuu

hayo ni majibu ya wahuni wala sio wataalam kama unavyodai na nadhani nao ni mbwa wanaolawiti watu wengine au kulawitiwa

jiulize kwann mtoto/mtu mzima aliyezoea kuliwa tigo hulazimika kufanyiwa operesheni kurekebisha njia ya haja kubwa

waulize manesi hospitalini watakueleza yanayotokea kwao
 
Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile:


KWA UFUPI
Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mfumo wa uzazi unaharibika

Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.

Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.

Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.

Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

Sampuli za utafiti

Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.

Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani

Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.

Imani potofu kwa wanaume

Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote. Katika utafiti huo, wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile, licha ya kwamba ni jambo linalokatazwa na dini zote.
Tanga yaongoza

“Tanga ndiyo kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo” anasema Mremi

Fikra za kulinda ubikira

Ilibainika kuwa wasichana wengine walikiri kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda ubikira wao na baadhi ni mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

Dk Mremi amekaririwa akisema “ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani. Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo”.

Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo hilo.

Dk Eliza Shayo, ambaye pia alishiriki katika utafiti huo anasema sababu ya kufanya utafiti huo ilikuwa ni kuangalia visababishi vya kusambaa kwa Ukimwi.

“Lakini pia tuliweza kujua tatizo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo lina ukubwa kiasi gani” anasema

Dk Shayo pia anasema utafiti huo uliangalia iwapo wanaofanya vitendo hivyo hutumia kondom au la. Wengi walionekana kutotumia kondom wakifikiri hawawezi kupata virusi vya Ukimwi, imani ambayo sio sahihi.

Ni changamoto

Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Kusini mwa Afrika, (GEMSAT) Dominica Haule anasema utafiti huu ni changamoto kwa serikali, watunga sera na vyombo vya sheria. “Ni wakati muafaka wa kujadiliana nini kifanyike kupunguza tatizo hili. Hii ni hatari na haikubaliki,” anasema Haule
Anasema wadau wa afya hawana budi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na kuweka wazi madhara ya vitendo hivyo.

Mhadhiri wa Masuala ya Saikolojia, Dk Kitila Mkumbo anasema suala hilo linaweza kuwa na athari kiafya.

“Kisaikolojia, kama wao wawili wamekubalina sawa, lakini kiafya lina athari kubwa,” anasema

Dk Mkumbo anasema ufanyaji wa mapenzi upo wa aina nyingi wengine hufanyia mdomoni, inategemea na makubaliano, lakini kiafya inaweza kuwa na athari.

Dk Meshack Shimwela, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Ndani ya Mwili kutoka hospitali ya Amana anasema mwanamke ambaye hufanya mapenzi kinyume na maumbile huathirika na kuacha kufurahia tendo hilo kwa njia ya kawaida.

“Lakini pia, wengi hujihisi kama wamelaaniwa na wanakosa kujiamini” anasema na kuongeza kuwa hata kama anaweza kufanya kwa mkumbo, baadae hujutia hasa anapojikuta anapata athari kubwa za kiafya kuliko furaha.

Dk Shimwela anasema kitendo hicho husababisha bakteria wasiohitajika kuingia katika sehemu ya haja kubwa na kuleta uambukizo.

“Eneo la haja kubwa limeumbwa kutoa na si kuingiza. Hivyo kitendo hicho husababisha uharibifu na kulegea kwa misuli” anasema

Anasema maradhi mengine ambayo hujitokeza katika sehemu ya haja kubwa pindi mtu anapofanya mapenzi kwa njia hiyo hayana tiba.

Anaongeza kuwa wanawake hupata madhara wakati wa kujifungua na hatari ya kupata maambukizi ya VVU ni kubwa zaidi.

Hatari kuu Jarida la Havard la afya ya Wanawake (Havard Women Health Watch) linaeleza kuwa ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya haja kubwa ni chanzo kikuu cha maradhi ya kuambukiza ukiwemo Ukimwi.Hii ina maana kuwa watu ambao wanafanya vitendo hivyo wana athari kubwa za kupata virusi vya Ukimwi.
Kwanini ni hatari?

Tishu zilizo katika njia ya haja kubwa ni laini na hazina maji maji, hivyo huchanika kwa urahisi wakati wa tendo na kuingiza vijidudu.

Utafiti kama huu ulifanywa nchini Marekani mwaka 2005 na kituo cha Kudhibiti Maradhi ya Kuambukiza (CDCP).

Katika utafiti huo asilimia 40 ya wanaume na 35 ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 na 44 walikiri kufanya tendo hilo kinyume na maumbile.

Wanatumia matambala kuziba kinyesi

Kuna athari kubwa za kufanya kitendo hicho, baadhi ya watu hujikuta wakivaa matambaza ili kuzuia kinyesi kisitoke kwa vile mfumo wa haja kubwa huwa umelegezwa.

Profesa wa Chuo Kikuu cha tiba cha Colombia, Judy Kuriansky anasema “Inashangaza kuona watu wanafanya mapenzi kwa njia hiyo wakidhani wanajikinga na Ukimwi, huko ni kujidanganya, ukweli ni kuwa njia hiyo ndio inayoweza kumfanya mtu kupata virusi kwa urahisi zaidi”. chanzo.


Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile - mwanzo - mwananchi.co.tz







 

hakuna siri ya watu wawili kati yenu kam asiyo wote ataropoka tu na ndiyo maana chochote ambacho hakifai mnapokifanya roho za wahusika huwatuma kujidhalilisha kwa maana ya kutafuta msaada waache huo uchafu!
 

kuna jamaa yangu mmoja hivi alikuwa analazimishwa na hawara yake amfanye huyu mama kinyume na maumbile akidai eti alikwisha kumaliza kuzaa! I just can't believe how far the wicked will go to justify evil!
 

Imani nyingine ni kudhani kwa kutendana hivyo basi ni uthibitisho wa kupendana! Evil knows how to twist facts...actually the contrary is true.
 

bacteria hao huzalishwa na kuongezeka kwa sababu shahawa zinawapa chakula ambacho hakipatikani ndani ya kinyesi na hivy6o kuzaliana na kusababisha madhara mengi kwa mwanamke. Pili, misuli inapolegea basi kuzuia ushuzi au kinyesi inakuwa ni vigumu kabisa.
 
Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile:


tigo husababisha michubuko na kuongeza kasi ya kuambukizana magonjwa ya aina zote ya zina hususani ukimwi.
 
Mkuu MziziMkavu salama? Umesahau kuweka source ya habari yako shekhe! Hii si umeikopi kwa "dinahicious"? Siku nyingine utakuwa unajivunjia heshima yako hapa jukwaani kwa kupuuzia mambo madogo madogo kama haya ya kuweka "source" tu!
 
Last edited by a moderator:


Mheshimiwa waziri naona umemkuna Janjaweed kwa haya uliyo yasema kwani anaonekana hajiamini hata kidogo. Sote kwa pamoja tumpe pole huyu mwenzetu.
 
Last edited by a moderator:
Na inasemekana akifanyiwa mara moja hatoacha kufanyiwa tena.
 
MziziMkavu nimesoma na nimeelewa,
kuna swali nitakuuliza nje ya hapa, samahani lakini.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…