Ya kwanza haina ukweli.Tupe reference.
kutokana na mkanganyika katika jamii zetu kuhusu tahadhari au
madhara ya ngono kinyume na maumbile, ambayo mtaani inajulikana kama mgongo au tigo. Ni kweli kuna madhara yanayoambatana na ngono ya aina hii. Lakini haya yaliyoorodheshwa yana ukweli wowote? Tuyapitie moja badala ya nyinge:
1.Mwanamke anayefanyiwa mchezo huu hupata matatizo makubwa wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa mfululizo wakati akijaribu kumsukuma mtoto.
Tukio hili humsababishia aibu kubwa mwanamke, kiasi cha kumshushia hadhi yake mbele ya jamii.
KWELI AU SI KWELI? Si kweli. Hakuna wataalamu wowote duniani (medical professionals) waliofanya utafiti kuhusu tigo ambao wamesema hili. Na kwa wale walioulizwa,
wamekanusha.
2.Pia anaweza kumuua mtoto kwa vile kila akimsukuma atoke, pumzi hukata kutokana na misuli inayofahamika kwa jina la sphincter kulegea na kusababisha ambane mtoto.
KWELI AU SI KWELI? Kama la mwanzo, hili pia si kweli. Limetungwa mitaani tu.
3. Umri unaposonga, haja kubwa hutoka bila kizuizi kutokana na misuli ya sphincter inayobana njia ya haja kubwa kulegea.
KWELI AU SI KWELI? Kwa mujibu wa
wataalam, hii inatokea kwa wale tu wananogewa na kupenda kujiingiza vitu vikubwa na vigumu zaidi ya uume, kama matango, chupa, na vikorokoro vingine.
4. Inaweza kusababisha saratani ya eneo hilo cancer of colon.
KWELI AU SI KWELI? Wataalam
wamesema hakuna uhusiano wowote wa colon cancer na tigo. Kitu
kinachoongeza uwezekano wa kupata colon cancer ni kuambukizwa virusi vinayoitwa human papilloma virus kupitia tigo. Lakini kama mwanaume hana virusi hivyo, au ametumia mpira wa kinga, tigo haiongezi uwezekano wa kupata cancer hiyo.
5. Ugonjwa wa UTI, yaani uambukizi kwa njia ya mkojo, huwa sugu, maana akitokea mwanaume alifanya kitendo hicho kisha akafanya ngono kama kawaida, bakteria wanaoishi sehemu hiyo wanaingia na kuwa na madhara makubwa.
KWELI AU SI KWELI? Hii ni kweli kama mwanaume akiingiza uume wake ukeni baada ya kuutoa tigo.
6. Hasara yake kubwa mwanaume anayekufanyia mchezo huwa hawezi kukuoa, pia ni rahisi kukutangaza kwa jamaa zake na kuonekana kituko mbele za watu, kama umeolewa heshima yako hupungua ndani ya ndoa.
KWELI AU SI KWELI? Nawageuzieni
nyinyi swali hili. Kweli au sio kweli? Fungukeni!
7. Mwisho kabisa baada ya
kuharibiwa ni kuwa na msongo wa mawazo na kuilaumu nafsi yako.
KWELI AU SI KWELI? Si kweli. Hakuna uhusiano wowote wa tigo na msongo wa mawazo. Suala la kujilaumu nafsi ni tofauti kati ya mtu na mtu, na hakuna utafiti wowote unaoonyesha inahusiana na hili.
Madhara ya kweli yaliyoorodheshwa na wataalam, na si ya kutunga ni haya yafuatayo:
1. Uwezekano mkubwa wa
kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama HIV, na HPV(Human Papilloma
Virus, ambavyo kama nilivyosema awali, ni virusi vinavyoongeza uwezekano wa kupata colon cancer) kama mwanaume anayehusika ana virusi/bakteria wa magonjwa hayo
2. Kuchubuka ngozi ya njia kubwa, hasa kama lubricant(sirima au
vilainisho kama mafuta) havijatumika.
3. Kuumia njia ya haja kubwa, hasa kama vilainisho havijatumika, na kutumia vitu vingine vikubwa na vigumu kama uume wa bandia n.k
Nawasalisha.